Wednesday, February 29, 2012





WATU AMBAO HAWANA HURUMA NA UTU WAKIMCHOMA MOTO MTU ALIYEDAIWA NI MWIZI WA PIKIPIKI , KWELI SISI BINADAMU  IMEFIKA HATUA MTU ANAMTOA ROHO MWEZAKE , KWANINI SHERIA ZIKAWEKWA?KIJANA ANAYEMCHOMA MOTO MWEZAKE ANA FAMILIA NAJISIAKIAJE ATAPOKUTA NDUGU YAKE AU MTOTO WAKE AMEFANYIWA KITENDO HICHO KWELI MIMI KIMENIUMA MPAKA NIMELIA ,BINABAMU TUMRUDIE MUNGU JAMANI TUNAKWENDA WAPI?

























HARUSI YA MWIGIZAJI Kel Mitchell GETS HITCHED To Asia Lee!









Remember Kel Mitchell...the former teen star from "Kenan & Kel," Good Burger & "All That"? Well, he recently got hitched! Pics of him and his wife Asia Lee's beautiful wedding day .......

Asia is a female rap artist who describes herself as "Queen of Cali." Kel tweeted from his love bubble a couple of days after the wedding:
My wedding day on sunday was everything I dreamed of! My wife is so beautiful! God is so good! I thank him for blessing me with her!...I cant stop smiling! Thank you Jesus!
Awwww! More cute pics from their big day:

MAHUBIRI MENGINE AAAAAA


Mahubiri


Ghafla unasikia mhubiri kwenye kituo cha daladala, nyinyi wanaume hamtaki kunisikiliza kwani mnawahi kwenda guest house kuzini, nanyi wanawake hamnisikilizi kwani neno langu linawachoma kwani mmetoa sana mimba,mna mapepo ndiyo maana mnavaa masuruali, wote mnaoitwa Asha,Amina,Abdallah,na nani sijui eti waislamu mnaenda motoni kwani mungu wenu nu Ibilisi,wakatoliki wote ni wa motoni kwani wanaabudu masanamu, wanasalia marehemu na wanakunywa pombe,hata walutheri na waanglikana wanaenda motoni kwani wanawafuata wakatoliki kwenye baadhi ya mambo.
 Njooni kwa Yesu anaokoa.mimi nilikuwa mzinzi wa wazinzi, nimewahi kuua watoto kwa kutoa mimba,sasa mnaona nilivyookoka nampenda Yesu.halafu nyinyi majina ya makabila msiyatumie yana mizimu na shetani hupenda watu wenye majina kama hayo.
Unakuta mtu anaitwa mwakalinga, malafyale sijui Rwegasira,mara huyo anitwa Otieno,manka,mara sijui mwana malunde,wote ni motoni.kwa nini msiitwe imani,furaha, ibrahimu,elshadai,asantemungunk,Mimi naitwa bwanaanaokoa,ni jina jipya, nimebatizwa kwenye kanisa la waliojitenga nao full gospel, lina upako.Acha dini haitakupeleka kokote,wazazi wako walikudanganya kukuweka dini uliyopo,mnaabudu masanamu, mnafuga majini, mtakwenda jehanamu
Nyinyi vijana mnavuta bangi na kulewa.mnajifanya mnawahi kazini wakati mnakwenda kuzii, tena nyinyi mnaovaa vizuri mnafanya ushoga na usagaji mnaniangalia nini? wengi wenu ni watoto wa nje ya ndoa, njooni kwa yesu, sisi tunaombea wagonjwa wanapona, tunawapa viza kwenda marekani, tunawapa utajiri na tunafufua misukule yote.Biblia inasema sisi wahubiri kazi yetu ni kuhubiri, mukisikia musiposikia shauri yenu,Mungu awabariki sana.
Ndugu zangu sasa haya ni mahubiri au anatafuta maneno?

Tuesday, February 28, 2012

SUALA LA MWAKYEMBE

Monday, 27 February 2012 19

Waziri wa Mambo ya Ndani,Shamsi Vuai Nahodha
ASEMA UCHUNGUZI BADO UNAENDELEA NA MATOKEO ATATANGAZA YEYE, ATAKA MANUMBA AULIZWE MWENYEWE CHANZO CHA TAARIFA YAKE
Ramadhan Semtawa
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha amesema uchunguzi kuhusiana afya ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe bado unaendelea na ni yeye atakayetangaza matokeo ya kama alipewa sumu au la baada ya kukamilika huku akiikana ripoti iliyotolewa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Kamishna, Robert Manumba.

Hii ni mara ya kwanza kwa Nahodha kutoa tamko hilo tangu kuibuka kwa mjadala kuhusu afya ya Dk Mwakyembe hasa baada ya DCI Manumba kuutangazia umma kwamba ripoti kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inaonyesha kuwa Naibu Waziri huyo hakulishwa sumu, kauli ambayo ilipingwa na Waziri mwenye dhamana ya Afya, Dk Haji Mponda na Dk Mwakyembe mwenyewe.

Akizungumza katika mahojiano maalumu ofisini kwake Dar es Salaam jana, Nahodha alisema uchunguzi kuhusu afya ya Dk Mwakyembe ni wa kisayansi na hauwezi kufanyika ndani ya wiki mbili au mwezi.

“Ninachosema ni kwamba uchunguzi nilioutangaza bado unaendelea,” alisema na kuongeza: Sasa mimi nimetangaza matokeo ya uchunguzi? Mimi ndiyo Waziri nasema uchunguzi bado unaendelea na mimi ndiyo nitatangaza hitimisho la jambo hilo.”

Alisema suala la Dk Mwakyembe ni zito na siyo la mtu kukurupuka kwani linagusa hisia za watu na kutahadharisha baadhi ya watu wanaojaribu kulifanya jepesi wanachezea kitu hatari.

“Ndiyo maana nasema ni jambo linalohitaji weledi wa hali ya juu katika kulichunguza. Ni jambo zito la kisayansi, naomba nipewe muda ili uchunguzi nilioagiza ufanyike kwa kina. Nasisitiza ni jambo linalohitaji weledi wa kisayansi.”

Waziri Nahodha alisema uchunguzi huo unafanyika kwa kuhusisha jopo la wataalamu wa sayansi hivyo kuwataka Watanzania kutambua kwamba uchunguzi huo unaendelea na ni vigumu kutamka utakamilika lini.

Kuhusu ripoti ya DCI

Alipoulizwa ni kwa nini asimchukulie DCI Manumba hatua kwa kutoa tamko wakati uchunguzi alioagiza haujakamilika alisema: “Ndiyo maana nasema, uchunguzi wa suala hili unaendelea. Sasa hatima yote hayo unayozungumza nasema nipeni muda.”

Alipoulizwa ni wapi DCI Manumba alipata ripoti ya Dk Mwakyembe wakati mgonjwa mwenyewe na Waziri wa Afya wameikana, alijibu: “Sasa, hilo ni vyema ukamtafuta yeye mwenyewe DCI aseme. Mtafute aseme yeye na Waziri wa Afya, hao watu wawili wanaweza kuzungumzia ripoti hiyo, lakini mimi nasema uchunguzi wa jambo hili la Dk Mwakyembe ni wa kisayansi na bado unaendelea.”

Alisema alichokisema DCI Manumba kinaweza kuwa na msingi ambao anaujua mwenyewe hivyo, ni vyema akaulizwa yeye kuhusu undani wa ripoti yake huku akisisitiza: "Mimi ninavyoliangalia jambo hili la Dk Mwakyembe linahitaji umakini wa hali ya juu katika kulishughulikia. Hilo la DCI mtafute mwenyewe akueleze.”

Nahodha pia hakutaka kuzungumzia suala hilo kwa undani hata pale alipoulizwa ikiwa haoni kwamba kukanwa kwa kiwango hicho kikubwa kwa ripoti ya DCI Manumba kunawafanya wananchi waanze kutilia shaka utendaji kazi wa jeshi la polisi.

Hata hivyo, alipoulizwa jana kuhusu kukanwa kwa ripoti yake na mawaziri, akiwemo wa Mambo ya Ndani ambayo ndiyo wizara mama inayosimamia Jeshi la Polisi, DCI Manumba alisema kimsingi hawezi kujibizana na waziri yeyote kwani kufanya hivyo itakuwa ni utovu wa nidhamu katika utumishi wa umma.

Alisema alichokifanya ni kuandaa jalada ambalo tayari liko kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ambaye kwa mamlaka na utaalamu wake wa kisheria, ataamua cha kufanya baada ya kulipitia.

“Siwezi kujibizana na waziri wangu au waziri yeyote. Kama amesema uniulize mimi, ninachoweza kusema ni kwamba tayari nimeandaa jalada liko kwa DPP. Sasa nikianza kuzungumza hili au lile itakua haina maana watu watasema nimeanza kujitetea,” alisema.

DCI, Dk Mwakyembe na Dk Mponda

Akizungumza na waandishi wiki mbili zilizopita, DCI Manumba alisema: “Ukweli kuhusu kauli hiyo inayodai kuwekewa sumu, tumeupata baada ya kuwasiliana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ambayo nayo imewasiliana na hospitali aliyokuwa amelazwa Dk Mwakyembe nchini India. Taarifa zinaonyesha kuwa hakuna sumu.”

“Hatua zaidi zinachukuliwa dhidi ya jambo hilo, kwa sasa litashughulikiwa kwa kufuata misingi ya kisheria,” alisema Manumba.

Hata hivyo, siku moja baada ya kauli hiyo ya DCI Manumba, Dk Mwakyembe alitoa taarifa kwa vyombo vya habari akisema: "Napata tabu kuamini kama DCI Manumba na wenzake waliisoma taarifa halisi ya matibabu yangu au walisoma taarifa ‘nyingine’ na kama waliisoma taarifa hiyo wenyewe au ‘walisomewa!’

“Nasema hivyo kwa kuwa alichokisema DCI Manumba kwa waandishi wa habari, hakifanani kabisa na picha iliyoko kwenye taarifa halisi ya Hospitali ya Apollo inayotamka wazi kuwa kuna kitu kwenye bone marrow (uboho) kinachochochea hali niliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaikia kukijua, kukidhibiti au kukiondoa huku vyombo vyetu vya dola vikipelekeshwa na mafisadi kusema bila msingi wa kisayansi wala aibu: “Hakulishwa sumu”, “hakulishwa sumu.”

Dk Mwakyembe pia alitoa sababu kuu tatu za kupinga ripoti ya DCI Manumba: “Kwanza kwa kuingilia mchakato wa matibabu yangu na uchunguzi wa kina kuhusu kiini chake, unaoendelea katika Hospitali ya Apollo, India ambako bado sijahitimisha matibabu yangu, pili kwa ufinyu wa uelewa unaojitokeza bayana kwenye tamko la Jeshi la Polisi unaosisitiza kuwa ‘sikunyweshwa sumu’ wakati sumu si lazima unyweshwe ili ikudhuru, inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa tu.
Soma zaidi 

MFANO WA KUIGWA KWA WANAUME

 
 
 
 
 
 
JUZI TULIWEKA PICHA HAPA YA BABA AKIWA AMEBEBA MTOTO NA TUKASEMA NI JAMBO ZURI.LEO TUMEFURAHI KUONA JAMBO HILI LINAWEZEKANA KWANI WABABA WANAANZA KUBADILIKA
MAJUKUMU YA ULEZI KWA KARNE HII NI YA WOTE HAIJALISHI JINSIA ,PICHANI BWN. GIBSON MWALIBWA AKIWA AMEMBEBA MTOTO WAKE WA MWAKA MMOJA NA MIEZI 8,WAKATI MAMA MZAZI AKIPATA HUDUMA ZA MATIBABU KWENYE HOSPITALI YA MKOA WA MBEYA.
Picha kwa hisani ya Grace Michael wa NHIF

WANAUME MPO HAPO


Mwanaharakati Renatus Mkinga Alazwa Muhimbili 

Dear All, 

 
Nimepokea taarifa kuwa Comrade Renatus Mkingah, a.k.a Mkinga Mkinga
Mwanaharakati machachari na hodari, msemaji asiyeogopa, mtunza ushahidi asiyebabaika,
Amelazwa Hosipitalini Muhimbili - kibasila 1st Floor Wodi namba 11 kitanda namba 25.


Kidole gumba kimeoza kwa sababu ya diabetes [kisukari] kwa hiyo kinatakiwa kuwa amputated[kukatwa]
Anahitaji msaada wa hali, mali na sala. 

Tafaadhalini wanabidii tumsaidie. tunaoweza tumtembelee. 

namba yake ni 0642644946 - waweza kumpigia ukimfariji au ukatumbukiza kitu kwenye hiyo tigo Pesa. 

Kind regards
Sungusia

KAMA UNAMPENDA YESU KRISTO HALAFU HUMTAMBU MAMA BIKIRA MARIA HUO NI UONGO

Biblia ikisomwa kiholela na bila kuelekezwa na wajuzi, basi wengi huipotosha. Mtume Petro anatuonya katika 2 Peter 16-18.


 Uyasome aliyoyaandika mtume huyu . Ni kwa sabab...u hiyo basi wengi wanashundwa kumng’amua Bikira Maria katika Biblia.


Kwa MKRISTO yeyote, akisema anampenda YESU lakini hampendi au hamtambui Mama Bikira Maria huyo ni MWONGO.

Katika amri ya nne ya Mungu “Muheshimu Baba na Mama yako ...” tunaalikwa kuwaheshimu wazazi sasa kama wewe ni rafiki yangu unanipenda mimi ila humuheshimu wala kumpenda mama yangu, urafiki wetu utakuwa ni wa UWONGO.Yesu ndie aliyeweka amri kumi na asingekuwa wa kwanza kutokumheshimu mama yake na kumfanya BAHASHA.

Na ndio maana ukisoma biblia utaona tangu mwanzo wa salamu ya malaika mama Maria alijulikana tayari kama Malkia kwakuwa yeye ni mama wa MFALME YESU.

Maria ni malkia:-Ukisoma pale bikira Maria anamtembelea Elisabeth, utaona kuwa Elizabeth alijazwa na roho mtakatifu akasema “why should I be honoured with a visit from the mother of my lord?”- nawezaje kutembelewa na mama wa bwana wangu?
Sasa katika dini ya kiyahudi, Judaism, mama wa mfalme aliitwa malkia na hukuweza kumuita mtu yeyote “lord”- bwana isipokuwa ni mfalme. Elisabeth alivyomuita Maria “mama wa bwana wangu” alimaanisha mama Bikira Maria kuwa ni malkia. Soma Lk 1:43

MAMA maria aliambiwa na Mungu kupitia malaika gabrieli kwamba “umebarikiwa kuliko wanawake wote” sasa Yesu alipokuwa akitoa mheri nane pale Mlimani “Heri wenye moyo safi....” Heri zote hizo Mama Bikira Maria anazo kwahiyo ahadi zote ambazo Yesu amezitaja hapo, mama yetu Bikira Maria anazo. Sasa utakapomchukulia Maria kana kwamba ni aliwekwa tu kama boti ya kuzaa Yesu alafu ikatelekezwa baharini basi tunamfanya Yesu MUONGO.

Watu wanahoji mbona Bikira Maria hajatajwa sana katika biblia? Heshima aliyopewa bikira Maria ni kubwa sana na ukitaka kujua umuhimu wake uangalie matukio makubwa ya ukombozi mf.

1.Utabiri wa Ukombozi: Mwanzo 3:15 Nitaweka uadui kati yako na mwanamke na kati ya kizazi chako na cha MWANAMKE

2. Alipotenda muujiza wa kwanza: Yohane;2:4 Kisha Yesu akasema “WOMAN, what do you want from me?- MWANAMKE nina nini nawe? Kwanini Yesu hakumuita mama? Je hakumuheshimu? Hapana alikuwa anamkumbusha Maria kwamba “Muda wangu wa kufanya miujiza bado, kwani nitakapoanza kufanya miujiza, hutakuwa tena mam yangu peke yangu bali mama wa wanadamu wote wanaosubiria ukombozi.

Alimkumbusha kwamba yeye ni mwanamke wa Mwanzo 3:15 ambae ana uadui na nyoka”. Mama Bikira Maria hali akitambua hayo alimruhusu mwanae kwenda public ilihali akijua kwamba nay eye mateso kwake yanaanza.

3.Katika kilele cha ukombozi (At the climax of God’s ministry) John 19:26 “Woman, this is your son”- MWANAMKE, tazama mwanao. Hapa katika kilele cha ukombozi, Yesu kupitia john anaitambulisha dunia kwamba huyu ndie mwanamke aliyetajwa toka mwanzo na toka katika harusi ya Kana.

 Ndugu zanguni, Yesu anampenda mama yake kuliko nini sijui. Ukitaka kumjua Yesu zaidi, muombe mama yake akufundishe, kwani yeye anamfahamu mwanae vizuri.

 Alimogesha, alimfulia nguo, alimbembeleza alipolia, alishuhudia mwanae akisulibiwa uchi wa mnyama, na pia aliipokea maiti ya mwanae ikiwa imepondwapondwa na haitamaniki

.Kama unadhani Mungu ni katili kuoana huyu mama alivyoteseka alafu amuache aozee kaburini, basi utakuwa haumfahamu MUNGU vizuri.

AHADI ZA YESU KWA WAFUASI WAKE
1.Kushiriki ushindi wake(kifo), 2. Kushiriki utukufu wake(ufufuko)
Mama Bikira Maria alikuwa ni mfuasi wa kwanza wa Yesu

SIKU YA MAMA DUNIA 2012

Kwa maoni yako ,mtazamo  na mifano mbalimbali taja jina la mama ambaye ni mfano wa kuigwa , kuanzia ngazi ya kaya, kijiji,kata tarafa ,wilaya,mkoa,nchi, dunia nzima

Mawazo yako tuma katika enzihanse.2011@gmail.com

Monday, February 27, 2012

MGOMBEA ARUMERU

KURA ZA MAONI MGOMBEA UBUNGE ARUMERU MASHARIKI KUFANYIKA TENA

Kamati Kuu ya CCM imeamua upigaji kura za maoni kumpata mgombea wake katika uchaguzi mdogo jimbo la Arumeru Mashariki urudiwe.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema leo jijini Dar es Salaam, kwamba kikao hicho chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kimeamua upigaji kura huo urudiwe kwa kuwa katika matokeo ya upigaji kura uliopita, hakuna mgombea aliyepata kura zinazovuka asilimia 50 ya kura zote.
Nape alisema, watachuana kwenye marudio hayo ni wagombea wawili, Wiliam Sarakikya na Sioi Solomon ambao waliwashinda wenzao wote katika kura za maoni za awali.
Kulingana na kumbukumbu ambazo mtandao huu unazo ni kwamba katika kura za maoni zilizopita, Sioi aliongoza kwa kura 361 wakati Sarakikya aliyeshika nafasi ya pili akipata kura 259 huku watatu Elishilia Kaaya akipata kura 176.
Nape alisema uchaguzi huo wa kura za maoni utarudiwa Machi 1, 2012 yaani Alhamisi wiki hii, na wapigakura ni wale wale wa Mkutano Mkuu wa jimbo walioshiriki uchaguzi wa kura za maoni uliopita.
Alisema, uchaguzi huo utasimamiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mzee Pius Msekwa , Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Kapteni Mstaafu, John Chiligati na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera, Costancia Buhiye.
Nape alisema siku itakayofuata yaani Machi 2, 2012, (Ijumaa), Kamati ya siasa ya wilaya itapitisha majina ya wagombea hao na baadaye siku hiyo hiyo jioni kamati ya siasa ya mkoa itapitia mapendekezo ya wilaya kabla Kamati Kuu kupitisha rasmi jina la mgombea Machi 3, 2012.
Akijibu maswali ya waaandishi wa habari, Nape alisema, hatua hiyo ya Kamati kuu ni ya utaratibu wa kawaida na haikuchukuliwa kwa dharura yoyote lakini ni katika kutekeleza moja ya kanuni za uchaguzi ndani ya CCM na umewahi kutumika.
Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, uchaguzi mdogo jimbo la Arumeru Mashariki utafanyika Aprili Mosi mwaka huu, baada ya vyama vitakavyoshiriki kwenye uchaguzi huo kuchuana katika kampeni ambazo kipyenga chake kitapulizwa rasmi Machi 9, mwaka huu.
Uchaguzi huo unafanyika kufuatia jimbo hilo kubaki wazi baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Jeremiah Sumari kufariki dunia hivi karibuni.

SHETANI ANAMJARIBU YESU MWANA WA MUNGU

INJILI YA JUMAPILI YA KWANZA YA KWARESMA ILINIGUSA SANA
26/2/2012

SHETANI ALISHINDWA PALE ALIPOMFUTA YESU WAKATI AMEFUNGA NA KUMWAMBIA WEWE SI MWANA WA MUNGU GEUZA MAWE KUWA MIKATE
NA YESU AKAMJIBU


Luka





AYA 4


1

Yesu alitoka katika mto Yordani akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akaongozwa na Roho mpaka jangwani.

2

Huko alijaribiwa na Ibilisi kwa muda wa siku arubaini. Wakati huo wote hakula chochote, na baada ya siku hizo akasikia njaa.

3

Ndipo Ibilisi akamwambia, "Kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru jiwe hili liwe mkate."

4

Yesu akamjibu, "Imeandikwa: `Mtu haishi kwa mkate tu."`

5

Kisha Ibilisi akamchukua hadi mahali pa juu, akamwonyesha kwa mara moja falme zote za ulimwengu. Huyo Shetani akamwambia,

6

"Nitakupa uwezo juu ya falme zote hizi na fahari zake, kwa maana nimepewa hivi vyote; nikitaka kumpa mtu ninaweza.

7

Hivi vyote vitakuwa mali yako wewe, kama ukiniabudu."

8

Yesu akamjibu, "Imeandikwa: `Utamwabudu Bwana Mungu wako, na utamtumikia yeye peke yake."`

9

Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, kwenye mnara wa Hekalu, akamwambia, "Kama wewe ni Mwana wa Mungu,

10

kwa maana imeandikwa: `Atawaamuru malaika wake wakulinde,`

11

na tena, `Watakuchukua mikononi mwao usije ukajikwaa mguu wako kwenye jiwe."`

12

Lakini Yesu akamjibu, "Imeandikwa: `Usimjaribu Bwana Mungu wako."`

13

Ibilisi alipokwishamjaribu kwa kila njia, akamwacha kwa muda.

14

Yesu alirudi Galilaya akiwa amejaa nguvu za Roho Mtakatifu, na habari zake zikaenea katika sehemu zote za jirani.

15

Naye akawa anawafundisha watu katika masunagogi yao, akasifiwa na wote.

16

Basi, Yesu alikwenda Nazareti, mahali alipolelewa, na siku ya Sabato, aliingia katika sunagogi, kama ilivyokuwa desturi yake. Akasimama ili asome Maandiko Matakatifu kwa sauti.

17

Akapokea kitabu cha nabii Isaya, akakifungua na akakuta mahali palipoandikwa:

18

"Roho wa Bwana yu juu yangu, kwani amenipaka mafuta niwahubirie maskini Habari Njema. Amenituma niwatangazie mateka watapata uhuru, vipofu watapata kuona tena; amenituma niwakomboe wanaoonewa,

19

na kutangaza mwaka wa neema ya Bwana."

20

Baada ya kusoma, akafunga kile kitabu, akampa mtumishi, kisha akaketi; watu wote wakamkodolea macho.

21

Naye akaanza kuwaambia, "Andiko hili mlilosikia likisomwa, limetimia leo."

22

Wote wakavutiwa sana naye, wakastaajabia maneno mazuri aliyosema. Wakanena, "Je, huyu si mwana wa Yosefu?"

23

Naye akawaambia, "Bila shaka mtaniambia msemo huu: `Mganga jiponye mwenyewe`, na pia mtasema: `Yote tuliyosikia umeyafanya kule Kafarnaumu, yafanye hapa pia katika kijiji chako."`

24

Akaendelea kusema, "Hakika nawaambieni, nabii hatambuliwi katika kijiji chake.

25

Lakini, sikilizeni! Kweli kulikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli nyakati za Eliya. Wakati huo mvua iliacha kunyesha kwa muda wa miaka mitatu na nusu; kukawa na njaa kubwa katika nchi yote.

26

Hata hivyo, Eliya hakutumwa kwa mjane yeyote ila kwa mwanamke mjane wa Sarepta, Sidoni.

27

Tena, katika nchi ya Israeli nyakati za Elisha kulikuwa na wenye ukoma wengi. Hata hivyo, hakuna yeyote aliyetakaswa ila tu Naamani, mwenyeji wa Siria."

28

Wote waliokuwa katika lile sunagogi waliposikia hayo walikasirika sana.

29

Wakasimama, wakamtoa nje ya mji wao uliokuwa umejengwa juu ya kilima, wakampeleka mpaka kwenye ukingo wa kilima hicho ili wamtupe chini.

30

Lakini Yesu akapita katikati yao, akaenda zake.

31

Kisha Yesu akashuka mpaka Kafarnaumu katika mkoa wa Galilaya, akawa anawafundisha watu siku ya Sabato.

32

Wakastaajabia uwezo aliokuwa nao katika kufundisha.

33

Na katika lile sunagogi kulikuwa na mtu aliyekuwa amepagawa na roho ya pepo mchafu; akapiga ukelele wa kuziba masikio:

34

"We! Yesu wa Nazareti! Kwa nini unatuingilia? Je, umekuja kutuangamiza? Ninakufahamu wewe ni nani. Wewe ni mjumbe Mtakatifu wa Mungu!"

35

Lakini Yesu akamkemea huyo pepo akisema: "Nyamaza! Mtoke mtu huyu!" Basi, huyo pepo baada ya kumwangusha yule mtu chini, akamtoka bila kumdhuru hata kidogo.

36

Watu wote wakashangaa, wakawa wanaambiana, "Hili ni jambo la ajabu, maana kwa uwezo na nguvu anawaamuru pepo wachafu watoke, nao wanatoka!"

37

Habari zake zikaenea mahali pote katika mkoa ule.

38

Yesu alitoka katika lile sunagogi, akaenda nyumbani kwa Simoni. Mama mmoja, mkwewe Simoni, alikuwa na homa kali; wakamwomba amponye.

39

Yesu akaenda akasimama karibu naye, akaikemea ile homa, nayo ikamwacha. Mara yule mama akainuka, akawatumikia.

40

Jua lilipokuwa linatua, wote waliokuwa na wagonjwa wao mbalimbali waliwaleta kwake; naye akaweka mikono yake juu ya kila mmoja wao, akawaponya wote.

41

Pepo waliwatoka watu wengi, wakapiga kelele wakisema: "Wewe u Mwana wa Mungu!" Lakini Yesu akawakemea, wala hakuwaruhusu kusema, maana walimfahamu kwamba yeye ndiye Kristo.

42

Kesho yake asubuhi Yesu aliondoka akaenda mahali pa faragha. Watu wakawa wanamtafuta, na walipofika mahali alipokuwa, wakajaribu kumzuia ili asiondoke kwao.

43

Lakini yeye akawaambia, "Ninapaswa kuhubiri Habari Njema za Ufalme wa Mungu katika miji mingine pia, maana nilitumwa kwa ajili hiyo."

44

Akawa anahubiri katika masunagogi ya Yudea.

Thursday, February 23, 2012

Njia ya msalaba inaanza leo , hamna jambo jema kuungana na waumini wengine kuubeba msalaba wa Yesu  Kristo , kwa kushiriki mateso ya Bwana Yesu Kristo







Bwana Yesu ndio kimbilio letu , na amini katika hilo ,natumaini katika hilo
BWANA YESU ASIFIWE
AMENI

MAANA YA JINA HYASINTA

Why names matter

Your First Name of: Hyasinta
Why Names Matter.



Below is a brief analysis of the first name only. For an analysis of your full name and destiny, see our full free Name and Birth Date Report service for further details.

    * Your name of Hyasinta contributes sensitive, creative, and idealistic qualities to your nature that could be expressed in a variety of literary or artistic fields.
      
    * You desire harmony and refinement in your environment and in all your personal associations.
      
    * Although mentally quick and intuitive in recognizing the thoughts and feelings of others, you experience a lack of fluency in verbal expression in responding.

    * Although the name Hyasinta creates the urge to understand others, we stress that it limits self-expression and self-confidence causing moods.
      
    * This name, when combined with the last name, can frustrate happiness, contentment, and success, as well as cause health weaknesses in the fluid systems, heart, lungs and bronchial area.

MLIMA KILIMANJARO JUU KILELENI

JAMANI MENDE

NINAPOAMUA KUTANGAZA MAHABA YANGU YA DHATI KWA "MENDE"...SEBASTIAN MAGANGA

Kusema ukweli leo hii katika pita pita zangu kwenye mtandao wa jamii (facebook) nimekutana na hiki na nimeamua kumnukuu bwana seba kwani kuna kikubwa cha kujifunza...tafadhali pitia..


TAMKO HILI LINAWEZA KUNIHUSISHA KWA KARIBU NA "UGONJWA WA AKILI"  KWANI KATIKA HALI YA KAWAIDA, NI JAMBO LA KUSTAAJABISHA PINDI AMBAPO, BINADAMU ANATAMKA BILA UOGA KWAMBA ANAMPENDA MENDE, UKITILIA MANAANI KWAMBA, KIDESTURI WADUDU HAWA WANAHUSISHWA NA UCHAFU.
 LAKINI KAMA WASEMAVYO WASWAHILI, A.KA. WAHENGA "HAKUNA UJINGA ULIOUJINGA MTUPU' TENA KAMA TUNGELIJUA KUTHUBUTU KUIGA MAISHA YA MENDE NI KUTHUBUTU KUCHUKUA MAARIFA AMBAYO YANAWEZA KUTUSAIDIA KATIKA MAISHA YA KILA SIKU,
KWA MFANO:

A] MENDE ANAUWEZO WA KUISHI KATIKA MAZINGIRA YEYOTE, IWE BARIDI KAAAALIIII AU JOTO LILILOKITHIRI, YEYE HUJIWEKA TAYARI KUTOKANA NA MAZINGIRA, KWANINI NA SISI TUSIJIANDAE KWA MIKIKI YA KIMAISHA? IL HALI MAISHA YETU YANAWEZA KUBADILIKA WAKATI WOWOTE? .

B] MENDE ANAWEZA KUISHI BILA KULA KWA MWEZI MZIMA, ANAWEZA PIA KUISHI BILA KUNYWA MAJI KWA WIKI NZIMA, KAMA VILE HAITOSHI HATA UKIMKATA KICHWA ANADUNDA HAI KWA SIKU 7....HAYO KWA BINADAMU HAYAWEZEKANI LAKINI KWA MIFANO HIYO CHA KUANGALIA HAPO NI KIWANGO CHA UVUMILIVU NA USHUPAVU WA MENDE, KWA KUIGA USHUPAVU NA UVUMILIVU  WAKATI TUNATAFUTA NJIA YA KUTIMIZA NDOTO ZETU, KUTATUSAIDIA SAANA KWANI  TUTALAZIMIKA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU NA KUBADILISHA MFUMO WETU WA KIMAISHA, NA JAPOKUWA ILE HALI ITUTUPA MATESO LAKINI, FARAJA YA MIPANGO YETU NA UVUMILIVU WETU, ITAZAA MATUNDA, WAINGEREZA WANASEMA WAZI WAZI NAMI SIBISHI "HARD WORK PAYS".

C] MACHO YA MENDE YANA LENSI KAMA 4000 HIVI, HIVYO KUMFANYA AWEZE KUONA PANDE ZOOOTE WAKATI MMOJA, ANTENNA ZAKE (ZIKO KAMA ZILE ANTENNA ZA TV ZILIZOPEWA JINA LA CHADEMA) INAWEZA KUWASAKA MENDE WENZAKE KWA URAHISI HATA KAMA WAMEJIFICHA FUTI SITA CHINI YA ARDHI, KWA MFUMO HUO TUNAWEZA KUJIFUNZA NAMNA YA KUTUMIA TEKNOLOJIA TULIOKUWA NAYO KWA MINAJILI YA KUTUPA TIJA ZAIDI KATIKA MAISHA YETU BINAFSI NA KIKAZI.
MWISHO KABISA NI KWAMBA MENDE ANA PAIR MBILI ZA MENO, YALE YA MDOMONI NA TUMBONI...SOMO KWETU HAPO NI LA MUHIMU SAANA , LAZIMA TUWE NA MPANGO WA AWALI NA MPANGO SAIDIZI IWAPO MPANGO WA AWALI UTAFELI TUTACHAGUA KUTMIA MPANGO SAIDIZI...KWA MIFANO HII NADHANI UTAJUINGA NAMI KATIKA KUELEKEZA MAHABA YA DHATI KWA MDUDU "MENDE"
(NYONGEZA NI KWAMBA MENDE NI KITOWEO SAAAFI KATIKA NCHI NYINGINE)

Wednesday, February 22, 2012

MABOMU SONGEA
22/2/2012

Mji wa Songea wachafuka

Mji wote wa songea na viunga vyake upo kimya kabisa huku polisi wakionekana wanafanya patroo na kujaribu kuwa tawanya watu ambao watakuwa katika vikundi. Maduka yote yamefungwa na watu wamejawa na hofu kubwa. mirindimo ya risasi na mabomu ya machozi yanaendelea kurushwa hapa na pale kwenye mikusanyiko ya watu. 
Mpaka tunakwenda mtambuni watu watatu wamepoteza maisha , Poleni na matatizo Songea

UTATA WA UGONJWA MWAKYEMBE, MWENYEWE ANENA

 

Mbunge Mbeya, Kyela Dkt.Harrison Mwakyembe kabla ya kuumwa

KyelaDkt. Harrison Mwakyembe.

Mwakyembe afyatuka


Dk. Harrison G. Mwakyembe (Mb), NW-UJ                                                       Dar es Salaam 18/02/12
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Nimelazimika leo Jumamosi, tarehe 18 Februari, 2012 kutoa taarifa hii kwa vyombo vya habari kufuatia mkutano wa DCI Robert Manumba na waandishi wa habari jana (17/02/12) kuongelea, pamoja na mambo mengine, hali yangu ya afya na kuhitimisha, kienyejienyeji tu kuwa “sikunyweshwa sumu” ila naumwa tu ugonjwa wa ngozi bila kufafanua ugonjwa huo wa ngozi umesababishwa na nini! 
Napenda nisisitize mapema kabisa kuwa msimamo huo wa Jeshi la Polisi umenikera sana katika hali niliyonayo ya ugonjwa, kwanza kwa kuingilia mchakato wa matibabu yangu na uchunguzi wa kina kuhusu kiini chake unaoendelea hospitali ya Apollo nchini India ambako bado sijahitimisha matibabu yangu; pili kwa ufinyu wa uelewa unaojitokeza bayana kwenye tamko la Jeshi la Polisi unaosisitiza kuwa “sikunyweshwa sumu” wakati sumu si lazima unyweshwe ili ikudhuru, inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa tu; na tatu kwa Jeshi la Polisi kujiingiza kwenye suala ambalo kwa takriban mwaka mzima halijawahi kuwa na dhamira ya dhati ya kulielewa au kulichunguza mbali na kulifanyia mzaha kupitia magazetini.
Itakumbukwa kuwa tarehe 9 Februari, 2011 nilimwandikia barua IGP Said Mwema kumtaarifu kuhusu njama za kuondoa maisha yangu na ya viongozi wengine. Kwa kutambua kuwa Jeshi la Polisi la Tanzania daima husisitiza kuletewa ushahidi kwanza ndipo lifanyekazi, nilihakikisha nimeainisha katika barua hiyo kila ushahidi nilioupata au kupewa. (Utaratibu huu wa Jeshi la Polisi kusubiri kuletewa ushahidi mezani, kama ambavyo mahakimu wanavyosubiri ushahidi mahakamani, haupo popote pale duniani (ila Tanzania tu) kwani kazi ya msingi ya Polisi si kuletewa, ni kutafuta ushahidi. Polisi wanachohitaji duniani kote ni kupata clue au tetesi tu. Hiyo inatosha kufukua ushahidi wote unaohitajika). Pamoja na kujitahidi kuanika kila aina ya ushahidi niliokuwa nao, mambo manne yalijitokeza ambayo yalionyesha wazi kuwa Polisi hawakuwa na dhamira ya dhati ya kupeleleza suala hilo:

(i) Siku chache baada ya kumkabidhi IGP barua hiyo, nilitumiwa timu ya “wapelelezi” ofisini kwangu kuja kuchukua maelezo yangu ya ziada. Timu hiyo ilikuwa inaongozwa na ACP Mkumbo, afisa wa polisi ambaye wiki chache zilizokuwa zimepita alikuwa miongoni mwa askari waliotuhumiwa kupokea rushwa kwa lengo la kumbambikizia madawa ya kulevya mtoto wa Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi, suala ambalo mpaka leo hii uongozi wa Polisi umeshindwa kulitolea maelezo ya kuridhisha. Kwa msingi huo, nilikuwa nimeletewa mtuhumiwa wa rushwa/ ujambazi kuendesha uchunguzi wa watuhumiwa wengine wa ujambazi! Nikatambua mara moja kuwa zoezi zima lilikuwa la mzaha, tena mzaha mkubwa! 

(ii) Wiki chache baada ya barua yangu kuwasilishwa kwa IGP na timu ya ACP Mkumbo “kuanza kazi”, Jeshi la Polisi likachukua hatua ya kuwapongeza na kuwazawadia askari niliowatuhumu kushirikiana na majambazi! Huhitaji kuwa profesa wa falsafa kuelewa kuwa huo ulikuwa ujumbe tosha wa kunipuuza. 

(iii) Hivi karibuni tuhuma za askari polisi kujihusisha na vitendo vya ujambazi mkoani Morogoro zilipopamba moto na kuwagusa askari “wale wale” niliowatuhumu kwenye barua yangu, IGP alichukua hatua ya kuwahamishia mikoa mingine!

(iv) ili kunikatisha tamaa kabisa, barua yangu ya “siri” kwa IGP ikavujishwa kwa makusudi kwenye vyombo vya habari na kuchapishwa kama habari ambayo ilikebehi na kukanusha taarifa nzima niliyotoa, sijui kwa faida ya nani! Lakini huu ni mchezo wa kawaida kwa polisi kwani hivi karibuni Mhe. Waziri Samuel Sitta alipohojiwa na ofisa mwandamizi wa Jeshi la Polisi ofisini kwake, wakiwa wawili tu, taarifa ya kikao hicho ikawa magazetini ikikebehi ushahidi aliotoa Sitta! The integrity of the police force leadership is on the line.
Nimeelezea vizuri katika barua yangu kwa IGP kuwa kundi hilo la mauaji lilikuwa limeelekezwa kuniua kwa kutumia sumu, taarifa ambayo kwa karibu mwaka mzima Polisi hawakutaka kuifuatilia kwa sababu wanazozijua wenyewe. Sasa huu msukumo mpya wa Jeshi la Polisi kutaka kujua kama nilipewa sumu au la na kukurupuka kutoa tamko hata kabla ya kunichunguza nilivyo, kunihoji mimi na wasaidizi wangu ofisini na hata kuongea na mabingwa wa Kihindi wanaonifanyia uchunguzi, umetokea wapi? 

Aidha napata taabu kuamini kama DCI Manumba na wenzake waliisoma taarifa halisi ya matatibabu yangu au walisoma taarifa “nyingine”, na kama waliisoma taarifa hiyo wenyewe au “walisomewa”! Nasema hivyo kwa kuwa alichokisema DCI Manumba kwa wandishi wa habari hakifanani kabisa na picha iliyo kwenye taarifa halisi ya Apollo ambayo inatamka wazi kuwa kuna kitu kwenye bone marrow kinachochochea hali niliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaikia kukidhibiti/ kukiondoa huku vyombo vyetu vya dola vikipelekeshwa na mafisadi kusema bila msingi wa kisayansi na bila aibu: “hakulishwa sumu”, “hakulishwa sumu”!
Nimesoma darasa moja Kitivo cha Sheria Mlimani na DCI Manumba. Baadaye IGP Mwema alikuwa mwanafunzi wangu wa sheria Mlimani. Vigogo hawa wawili wa usalama wa raia nchini hawajanitendea haki, nao wanajua. Wanajua vilevile kuwa sitakaa kimya au kumung’unya maneno come what may pale ambapo haki inakanyagwa.
Tuendelee kuombeana afya na uhai ili kutendeane haki na vilevile tuitendee nchi yetu haki kwa kuvimalizia viporo vinavyokera vya Dowans, EPA, Kagoda n.k. kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

Mungu Ibariki Tanzania.
habari hii kutoka facebook bofya hapa

SUGU NA RUGE WAMALIZA TOFAUTI ZAO

MBUNGE WA MBEYA MJINI JOSEPH MBILINYI 'SUGU' NA RUGE WAMALIZA TOFAUTI ZAO MBELE YA WAZIRI MCHIMBI


TAARIFA:KWANZA POLENI NA SAMAHANINI KWA HALI YA SINTOFAHAMU ILIYOTOKEA LEO KUTOKANA NA TAARIFA ZA GHAFLA ZA USULUHISHI KATI YETU NA RUGE/CLOUDS FM,NI KUTOKANA NA UNYETI WA ISSUE YENYEWE ILIBIDI TUFANYE HIVYO KWA NIA NJEMA KABISA KWANZA NAOMBA TUJIPONGEZE KWA KUWA TUKIO LA LEO NI USHINDI KWA VINEGA KWA MAANA KWAMBA MADAI YETU YOTE YA MSINGI NDIO YALIKUWA MSINGI WA MAJADILIANO NA RUGE AMEKUBALI KUYATEKELEZA YOTE KUANZIA SUALA LA STUDIO YA RAIS KURUDISHWA KWA BASATA ILI IWE YA WASANII WOTE,PIA T.F.U IJIKABIDHI KWA CHAMA HALALI CHA WASANII YAANI T.U.M.A KAMA AMBAVYO TULIKUWA TUNADAI NA MPAKA ISSUE ZA WASANII KUNYANYASWA NA KUBANIWA NA PIA SUALA LA MALIPO HAFIFU VYOTE VIMEJADILIWA NA KUKUBALIWA KWA UTEKELEZAJI HAIKUWA KAZI RAHISI,KWANZA ILIANZA KWA WAO KUMPIGIA MWENYEKITI WANGU MBOWE KUTAKA TUKAE CHINI,AMBAPO KAMANDA MBOWE ALINISHAURI TUKAE NAO CHINI KAMA KWELI WANA NIA YA KUYAMALIZAÖBAADAYE WAKAMPIGIA MR SHIGONGO AMBAYE NI WAZI KUWA NI KATI YA WATU WANGU WA KARIBU NAYE BAADA YA KUONGEA NA MR. KUSAGA TU ALINIPIGIA NA KUNISHAURI HIVYO HIVYOÖNA KAMA HAIKUTOSHA WAKALIFIKISHA HILI SUALA KWENYE KAMATI YA BUNGE AMBAYO ILINITAKA NIIPE MAELEZO YA KIINI CHA MGOGORO NA NIKAFANYA HIVYO AMBAPO PIA BAADA YA KUNIELEWA WAKASHAURI NIKAE NAO CHINI NA HATIMAYE SUALA HILI LIKAISHIA MIKONONI MWA WAZIRI NCHIMBI PAMOJA NA MHE.

TUNDU LISSU(MP) KUWA WAPATANISHI WETU WAZIRI NCHIMBI AKAANZA KWA KUMUITA RUGE DODOMA NA ALIKUJA TUKAKAA KWA HATUA YA KWANZA NA HATIMAYE LEO TUKAKAA TENA MAKAO MAKUU YA WIZARA YA UTAMADUNI CHINI YA DR NCHIMBI NA MHE TUNDU LISSU NA HATIMAYE TUKAFIKIA HATUA HII YA LEO.

VITA YETU ILIKUWA NA HOJA HATUKUWA TUNAPIGANA TU KWA CHUKI BINAFSI KAMA BAADHI YA WATU WALIVYOKUWA WANAJARIBU KUIWEKA,KWAHIYO KAMA HOJA ZETU ZIMEELEWEKA KWA SASA TUNATAKIWA KUSHUKURU NA KUFURAHIA LAKINI NAOMBA NIWAHAKIKISHIE MISIMAMO IKO PALE PALE NA NIMEWAWEKA WAZI KUWA ANTI-VIRUS ITAENDELEA KUWEPO ILI KUENDELEA KU-SCAN VIRUS WENGINE KAMA MAMENEJA MASOKO NA WENGINE WATAKAOJITOKEZA KWANI NCHI INAPOSHINDA VITA AU HATA KUFIKIA TU MAKUBALIANO YA AMANI NA NCHI ADUI YAKE HAINA MAANA NCHI HIYO INAVUNJA JESHI LAKE ASANTENI SANANI

**********************************

MDAU : MIMI NAWAPONGEZA NI MFANO MZURI KATIKA KIPINDI HIKI CHA KWARESMA

SIKU YA MAJIVU

TUMSIFU YESU KRISTO

LEO NI SIKU YA MAJIVU MIMI NAKWENDA KUSALI KAWE
TUMWOMBE MUNGU ATUSAIDIE KUTUBU DHAMBI ZETU ILI TUWEZI KUFIKA MBINGUNI .

SIKU YA LEO INATUKUMBUSHA KWAMBA SIKU MOJA TUTAKUFA TUJIANDAYE MAPEMA

TUMSIFU YESU KRISTO


 Mtoto akipakwa majivu





Waumini zaidi ya bilioni moja wa madhehebu ya katoliki na waothodox ulimwenguni kote pamoja na wakristo kwa ujumla leo wameanza mfungo wa kwaresma.


siku arobaini za kujinyima na kujitesa kwa ajili ya maandalizi ya ufufuko wa Bwana Yesu.


Hili ni jambo la imani na limedumu kwa zaidi ya milenia mbili sasa.Wakristo huombwa na Kanisa kufunga kabisa siku ya jumatano ya majivu ambayo ilikuwa leo.

Kuna theolojia kubwa na ngumu juu ya tendo hili la imani.


Kufunga chakula na kujinyima anasa na vitu tunavyovipenda ili kuungana na wenye shida wakati huu.Naam tunategemea kuona matendo mema wakati huu na kwamba yatakuwa mazoezi mema ya kiroho na yataendelea hata baada ya pasaka.


 Kuna kupakwa majivu katika paji la uso na maneno tubuni na kuiamini injili husemwa ambamo waumini hujibu amina wakikumbushwa juu ya umuhimu wa kumrudia Mungu na kwamba tumetoka katika mavumbi na tutarudi kuwa mavumbi.Rangi za Zambarau hutumika zikiwa na maana ya toba.

Naam nasi Mjengwablog tunawatakia Kwaresma njema.

WAZIRI MUU MAMA PINDA WAKIPAKA MAJIVU

Friday, February 17, 2012

ASKOFU ACHANGIA VYOMBO VYA MUZIKI


ASKOFU wa Jimbo la Mashariki (TAG), Mchungaji Lawrence Kametta ametoa mchango wa vyombo vya muziki kwa Kanisa la TAG Kitunda Kati jijini Dar es Salaam ili kuendeleza vipaji vya muziki wa injili.

Askofu Kametta alitoa mchango huo juzi wakati akizindua rasmi jengo hilo la ibada, na kuomba kushirikishwa katika hatua zote za ununuzi wa vifaa hivyo.

Alisema kuwa badala ya watu kufurahia kwenda mpirani ama katika nyumba za anasa, ni vyema wakafurahia kuingia katika nyumba za mungu kwa kuwa sehemu hiyo ndiyo pekee ya tiba mbadala kwa matatizo yote.

"Vijana sugu, majambazi, wanaotumia dawa za kulevya matatizo yao hayawezi kumalizwa na viongozi, bali nyumba za mungu za pekee, ndio maana tujitolee kwa mioyo yetu yote kuzijenga nyumba hizi.
 
"Mtapata dhambi za bure kumlaumu Kikwete au kiongozi mwingine yeyote, kwa kuwa hakuna mwenye uwezo wa kubadilisha maisha ya wanadamu, tiba ya matatizo sugu ipo katika nyumba ya mungu, na nyumba hizi zikitumika sawasawa zitabadili maisha ya watu kimwili na kiroho,"alisema Askofu huyo.

Aliongeza kuwa, nyumba ya mungu ni karakana ya kiroho, hivyo ina uwezo wa kutengeneza mwili wa binadamu na ukarudi kuwa mpya na kuongeza kuwa ni tiba ya matatizo yote sugu.

"Wakati madaktari wakigoma, watumishi wa mungu hawana mgomo, wakati watoa huduma nyingine kwenye jamii wakigoma kwa kudai maslahi bora, watumishi wa mungu wapo wakitoa huduma bila kujali maslahi, wapo siku zote kwa tiba ya uponyaji. Hivyo ni vyema jamii ikazitiilia maanani nyumba za mungu kama mkombozi wa maisha yao duniani na mbinguni,"aliongeza Askafu Kametta.

Hata hivyo, aliwataka wananchi waelewe kuwa utakatifu wa mtu si mavazi, wala muonekano mzuri bali ni hali inayotoka ndani ya moyo ikiwa ni sambamba na kujitolea kufanya kazi za mungu kwa ibada na hata nyimbo.

Sambamba na kuchangia katika vyomvo vya muziki, Askofu huyo aliahidi kutoa mchango wake kwa kanisa hilo ambalo limejengwa kwa nguvu ya wananchi.

mwisho

MREMBO HUYOOO NA POZI LAKE