Mweneyikiti wa Jumuia ya Madaktari nchini Dk Stephen Ulimboka, jana alipigwa na kujeruhiwa vibaya na watu wasiofahamika.
Dkt
Ulimboka anadaiwa kuvunjwa mbavu, miguu yote miwili, kung’olewa meno
yote ya mbele na kuumizwa vibaya katika sehemu mbalimbali za mwili wake.
Tukio
hilo la kikatili na kusikitisha lilitokea usiku wa kuamkia jana jijini
Dar es Salaam, na linadaiwa kufanywa na watu wa sio julikana ambapo
kabla ya kufanya unyama huo walidaiwa kumteka na kumpiga kabla ya
kumtelekeza katika eneo la msitu wa Pande Mabwepande.
DKT. ULIMBOKA ASIMULIA TUKIO
Akisumulia
tukio hilo Dkt Ulimboka alisema kuwa jana usiku alipigiwa simu na mtu
aliyejitambulusha kwake kuwa anaitwa Hemed, aliyemwambia kuwa
anahitaji kuongea naye, na ndipo walipopanga kuonana katika eneo la
Leaders Kinondoni.
Dk
Ulimboka aliyekuwa akiongea kwa tabu, aliendelea kusimulia kuwa wakati
akiongea na mtu huyo anayekiri kuwa alikuwa akifahamiana naye kabla,
alikuwa na wasiwasi kwani kila mara alikuwa akipokea simu na kuwasiliana
na watu wengine ambao hawakuwapo eneo hilo.
Alisema
baada ya muda alishangaa kuona wanaongezeka watu wengine watano wakiwa
na silaha, kisha wakamwambia kuwa anahitajika kituo cha Polisi na
kumvuta na kumuangusha barabarani kabla ya kumuingiza katika gari lenye
rangi nyeusi na kuondoka naye.
Dkt
Ulimboka alisema kuwa wakiwa njiani walimpiga, na kumfikisha katika
msitu huo wa pande na kuendelea kumpiga mpaka alipoteza fahamu.
MADAKTARI NAO WALONGA
Akisimulia
mkasa huo mmoja wa madaktari wenzie aliyefahamika kwa jina moja la Dkt
Deo, alisema kuwa alipigiwa simu na mtu hasiyemfahamu na kumfahamisha
tukio hilo.
Alisema
alipofika katika kituo cha Polisi cha Bunju, alimkuta akiwa katika
hali mbaya na ilikuwa ngumu kumtambua kwakuwa alikuwa na majeraha mengi
eneo la usoni.
Aliongeza kuwa akiwa na wenzie waliamua kumchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwaajili ya matibabu.
"Hali
yake kwakweli ni mbaya sana, amepigwa mno na ameumizwa kwakweli
tumemleta hapa hili aweze kupata matibabu, lakini mimi nilivyomkuta mara
ya kwanza nilishindwa hata kumtambua kwa jinsi alivyokuwa
ameumizwa"alisema Dkt Deo
Alisema
kuwa alisimuliwa na Dkt Ulimboka kwamba watu hao waliomteka na kumpiga
walikuwa na silaha na kwamba alishindwa kuwatambua.
Aliongeza
kuwa Dkt Ulimboka alidai kuwa wakati akiwa katika halimbaya alikuwa
akisikia mazungumzo yao, wakibishana juu ya kumuua wengine wakisisitiza
achomwe sindano, na wengine wakitaka kumpiga risasi.
Alisema
wakati mabishano yakiendelea kati yao, Dkt Ulimboka aliinuka akiwa na
lengo la kukimbia lakini watu hao walipiga risasi hewani iliyomshtua na
kuangua chini.
Kwa
upande wake Dkt Cathbeth Mcharo ambaye ndiye aliyempokea Dkt Ulimboka
Hospitalini hapo, alisema kuwa hali yake ni mbaya na kwamba
wanajitahidi kumpatia huduma za haraka.
Alisema kuwa kwa hatua za awali amefanyiwa vipimo mbalimbali, ili iweze kufahamika aina ya matibabu anayotakiwa kupatiwa.
POLISI
Kamanda
wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova
amezungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo la utekaji nyara na
kujeruhi lililompata kiongozi mgomo wa Madaktari Steven Ulimboka
anayedaiwa kutekwa na watu watano wakati akipata kinwaji katika klabu ya
Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam.
Kamanda
Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka
kumtaja jina lake kiusalama na kutoharibu upelelezi kuwa msamaria mwema
huyo alimuokota Ulimboka katika msitu wa Mabwepande na kutoa taarifa
kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu alichukua
maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa katika hospitali ya taifa
ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Kamanda
Kova amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum limeunda jopo maalum kwa
ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara, kwani ni
tukio la kwanza kutoke nchini, ameongeza kwamba wahusika wote
watakaobainika kuhusika na tukio hilo wachukuliwa hatua za kisheria na
sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha matukio mengine kama hayo
MUHIMBILI
Wakati
hayo yakitokea inadaiwa kuwa Askari Kanzu mmoja alikumbana na kipigo
kikali kutoka kwa madaktari hapo Muhimbili kwa kile kilochodaiwa
kutambuliwa na Dkt Ulimboka kuwa mmoja wa watu walio mjeruhi.
Pia
inadaiwa kuwa Askari huyo aliingia chooni na kufanya mawasiliano na
wenzake huku Madaktari hao wakimsikiliza na kutokana na alichokua
akiongea chooni humo ndipo alipotoka aliambulia kichapo kikali.
Pia
baadhi ya madkatari na wauguzi walikuwa wakisukuma gari alilokuwa
amepanda Dkt Ulimboka huku wakiimba nyimbo za Umoja na Mshikamano Daima
miongoni mwao.
Hali ya ulinzi ilikuwa kali Hospitalini hapo kwani Picha zilikuwa haziruhusiwi kupigwa.
HABARI KWA HISANI YA MPEKUZI