Tuesday, May 8, 2012
LULU MAHAKAMANI TENA 3
Msanii wa filamu za maigizo nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, leo amepandishwa tena kizimbani mara ya tatu katika kesi ya mauaji ya Kanumba inayomkabili ambapo mawakili wanaomtetea wakiongozwa na Kennedy Fungamtama waliwasilisha ombi la kurekebisha umri wa mshitakiwa huyo kuwa miaka 17 na si 18 kama ilivyowasilishwa mahakamani hapo.
Fungamtama na jopo lake walisema mteja wao ni mtoto mdogo hivyo kesi hiyo ipelekwe mahakama ya watoto na kuwasilisha cheti kinachoonesha ana umri wa miaka 17.
Upande wa mashitaka umetupilia mbali ombi hilo na kudai cheti kilichowasilishwa kina mapungufu kadhaa likiwemo jina la Dyana ambalo halijawahi kusikika likitumiwa na mshitakiwa huyo.
MKAPA MAHAKANI KISUTU
| ||
|
Friday, May 4, 2012
KIKWETE APANGUA BARAZA LA MAWAZIRI SURA MPYA ZATAWALA
Friday, May 04, 2012
Baraza La Mawaziri
Wassira anaendelea na nafasi yake
Celina Kombani kabadilishiwa Wizara
Nagu anaendelea
Lukuvi anaendelea na wizara yake
Ghasia kabadilishiwa Wizara
Sitta anaendelea na Afrika Mashariki
Nahodha anahamia Wizara ya Ulinzi
Magufuli anaendelea na nafasi yake
Hussein Mwinyi kahamishiwa Afya
Kawambwa anaendelea na ElimuS
Membe anaendelea na Mambo ya Nje
Chikawe anarudi Katiba na Sheria
Sofia Simba na nafasi yake
Nchimbi - Mambo ya ndani
Mathayo David anaendelea
Kabaka anaendelea na nafasi yake
Mbalawa anaendelea na nafasi yake
Tibaijuka anaendelea na nafasi yake
Chizza anakuwa Waziri wa Kilimo chakula na ushirika
Maghembe - Maji
Mwakyembe anakuwa Waziri wa Uchukuzi
Celina Kombani kabadilishiwa Wizara
Nagu anaendelea
Lukuvi anaendelea na wizara yake
Ghasia kabadilishiwa Wizara
Sitta anaendelea na Afrika Mashariki
Nahodha anahamia Wizara ya Ulinzi
Magufuli anaendelea na nafasi yake
Hussein Mwinyi kahamishiwa Afya
Kawambwa anaendelea na ElimuS
Membe anaendelea na Mambo ya Nje
Chikawe anarudi Katiba na Sheria
Sofia Simba na nafasi yake
Nchimbi - Mambo ya ndani
Mathayo David anaendelea
Kabaka anaendelea na nafasi yake
Mbalawa anaendelea na nafasi yake
Tibaijuka anaendelea na nafasi yake
Chizza anakuwa Waziri wa Kilimo chakula na ushirika
Maghembe - Maji
Mwakyembe anakuwa Waziri wa Uchukuzi
Mkuchika- Utawala bora
Samia suluhu – Muungano
Huviza – Mazingira
Mery nagu – Uwekezaji
Lukuvi – Uratibu na sera
Hawa gasia – TAMISEMI
Samweli sita- East Africa
Shamsi nahodha- ulinzi
Magufuli- ujenzi
Hussen mwinyi- Afya na ustawi
Shukuru kawambwa- Elimu na Mafunzo
Sofia – Maendeleo ya jamii
Membe – Nje
Mathia Chikawe – katiba na Sheria
Emmanuel Nchimbi – Ndani
David Matayo – Mifugo
Kabaka – Kazi na Ajira
Prof marawa- Mawasiliano
Prof Tibaijuka – Nyumba
Cristopher chizza – kilimo
Magembe – Maji
Mwakyembe – uchukuzi
Dr fenela mkangara – Habari vijana na michezo
Kaigasheki – Maliasili na utalii
Kidogo – Viwanga na Biashara
Fedha – William
Sospter – Madini
Mwandyosa – Asiye na wizara maalumu – Ikulu
Samia suluhu – Muungano
Huviza – Mazingira
Mery nagu – Uwekezaji
Lukuvi – Uratibu na sera
Hawa gasia – TAMISEMI
Samweli sita- East Africa
Shamsi nahodha- ulinzi
Magufuli- ujenzi
Hussen mwinyi- Afya na ustawi
Shukuru kawambwa- Elimu na Mafunzo
Sofia – Maendeleo ya jamii
Membe – Nje
Mathia Chikawe – katiba na Sheria
Emmanuel Nchimbi – Ndani
David Matayo – Mifugo
Kabaka – Kazi na Ajira
Prof marawa- Mawasiliano
Prof Tibaijuka – Nyumba
Cristopher chizza – kilimo
Magembe – Maji
Mwakyembe – uchukuzi
Dr fenela mkangara – Habari vijana na michezo
Kaigasheki – Maliasili na utalii
Kidogo – Viwanga na Biashara
Fedha – William
Sospter – Madini
Mwandyosa – Asiye na wizara maalumu – Ikulu
Kombani -Utumishi
Mkuchika -Utawala bora
Samia -anaendele na Muungano
Tereza- anaendelea na Maziria
Nagu -anaendelea
Lukuvi -anaendelea
Ghasia -Tamisemi
Sitta anaendelea
Nahodha -Ulinzi
Magufuli- anaendelea
Mwinyi -Afya
Kawambwa enaendelea
Simba -anaendelea
Membe- anaendelea
Chikawe- Katiba na Sheria
Nchimbi -Mambo ya Ndani
Mathayo anaendelea
Kabaka anaendelea
Mbarawa anaendelea
Tubaijuka anaendelea
Chiza -Kilimo
Mahembe- Maji
Mwakyembe -Uchukuzi
Mkungara -Habari
Kagasheki -Maliasili
Kigoda- Viwanda
Mgimwa -Fedha
Muhongo -Nishati
Mwandosya hana wizara maalumu
Mnaibu:
Kitwanga VP
PM office Majaliwa na Mwanri
Kazi Makongoro- Naibu
Malima- Chakula
Home- Silima
Teu -Viwanda
Nagoro -anaendelea
Lwenge -Ujenzi
Mahadhi -Nje
Medeye -Ardhi
Ummy- Jamii
Mulugo -Elimu
Juma- EA
Nyalandu -Maliasili
Rashid- Afya
Simbachawene -Nishati
Mkuya -Fedha
Makambo- Sayansi
Tizeba -Uchukuzi
Makala- Habari
Mahenge- Maji
Masele- Nishati Madini
Kairuki -Sheria
Mbene -Fedha
KEKI YA CCM
Keki Yenye Rangi Za CCM Yakataliwa
Halima Mdee Mbunge wa Kawe akigeukia pembeni na kuonyesha ishara ya kukataa kuigusa keki ya Shay Rose Banji huku akicheka.
Wabunge
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi
waliangua Vicheko pale wenzao wa CHADEMA walipoikwepa kuigusa nakuila
Keki ya Birthday ya Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Shy Rose Banji
wakati wa tafrija yake iliyofanyika Nyumbani Longe Jijini Dar es Salaam.
Wabunge
hao wa CHADEMA ni Halima Mdee (Kawe) ambaye anaonekana picha ya juu
akiikataa keki hiyo iliyotolewa na Wakurugenzi wa Nyumbani Longe, Gadna
G Habash na Mkewe Lady Jay Dee, huku Mbunge wa Viti Maalum, Lucy Kiwelu
picha ya chini nae akijificha asiitazame kwa karibu.
Wabunge hao waliigwaya Keki hiyo kutokana na jinsi ilivyopambwa rangi za CCM.
Huku
Wabunge wa CCM wakishangilia wakimtaka Halima Mdee aongoze Ukataji wa
Keki hiyo ambayo ilitolewa baada ya keki ya awali iliyoandaliwa na Baby
Girl Shy Rose kuliwa, ilishindikana kuliwa na kuhifadhiwa.
RAIS KIKWETE AMTEUA JAMES MBATI KUWA MBUNGE
JK ampa ubunge James Mbatia
*Wamo Profesa Muhongo, Bi. Janet Mbene
*Watabiriwa kuwemo kwenyea baraza jipya
*Nchimbi awaomba Watanzania wamuombee
*Tibaijuka, Magufuli nyota zao zang'aa
WAKATI Rais Kikwete anatarajia kufanya mabadiliko katika baraza kake la mawaziri wakati wowote sasa, jana amemteua Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Bw. James Mbatia, kuwa mbunge.
Mbali na Bw. Mbatia, Rais Kikwete amemteua Profesa safi Profesa Sospeter Muhongo, Bi. Janet Mbene, kuwa wabunge. Taarifa iliyotolewa kwenye vyombo vya habari jana Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu, ilieleza kuwa Rais Kikwete amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa mamlaka ya uteuzi aliyopewa.
"Rais Kikwete amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa mamlaka ya uteuzi aliyo nayo chini ya Ibara ya 66(i) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Uteuzi huo umetafsiriwa na wachambuzi wa masuala ya kisiasa kuwa watu hao wanaandaliwa kuwa mawaziri, hasa ikizingatiwa kuwa Rais anatarajiwa kufanya mabadiliko ya baraza lake wakati wowote kuanzia sasa.
Profesa Muhongo ambaye ni mtaalam wa masuala ya madini Geology anatabiriwa kukabidhiwa kuongoza Wizara Nishati na Madini, huku nafasi za wengine walioteuliwa zikiwa bado kitendawili.
Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana Mhadhiri wa Kitivo cha Sayansi za Siasa katika Chuo Kikuu cha SAUT, Profesa Mwesiga Baregu, kuhusu uteuzi huo, alisema; "Anawaandaa kwa ajili ya kuwaweke katika baraza lake la mawaziri."
Profesa Baregu alisema alisema baraza la mawaziri la sasa limepwa ndiyo maana ameamua kuchukua watu kutoka nje ya CCM. Alimshauri Rais Kikwete, kuteua baraza la mawaziri lenye sura mpya na watu wachache na wenye uwezo wa kufanyakazi.
Alitaja sifa nyingine ambazo anataka mawaziri wapya kuwa nazo kuwa ni uaminifu, wawajibikaji, uadilifu na wenye kuleta tija kwa wananchi wanaowatumikia.
"Akichagua wale wale wa zamani hakutakuwa na mabadiliko yoyote," alisema Profesa Baregu. Alishauri mabadiliko hayo ya baraza yafanyike haraka kwani kuwaacha wanaotuhumiwa kwa kushindwa kuwajibika kuendelea kuwepo ofisini kunaweza kuwapa mwanya wa kupoteza vielelezo pindi watakapofikishwa kwenye vyombo vya sheria.
"Mimi namshauri rais kufanya mabadiliko haraka iwezekanavyo, kwani kuendelea kuwepo ofisini kwa mawaziri hao ni tatizo na mambo yanaweza kuharibika kwa kuwa wana uwezo wa kuchukua vielelezo na kupoteza ushahidi," alisema.
Hata hivyo alisema kufanya mabadiliko pekee hakutasaidia bali kinachotakiwa ni kuwatendea haki mawaziri hao kwa kuwafikisha mahakamani ili watakaobainika.
Alisema mbali na kubadilisha baraza la mawaziri, pia anatakiwa kuwachukulia hatua wote waliohusika wakiwemo makatibu wakuu wa wizara kama wanahusika.
Alisema upotevu wa fedha ni matokeo ya kukosekana kwa uwajibikaji miongoni mwa mawaziri hao. Alipoulizwa ni mawaziri wapi wanafaa kubaki kwenye safu mpya itakayoundwa, alisema atatoa maoni yake baada ya uteuzi.
Naye, Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Dkt. Helen Kijo- Bisimba, alisema kubadilisha mawaziri si suluhuhisho kukabiliana na tatizo la viongozi kutowajibika.
Alisema kuwa suluhu ni kuwawajibisha wale wote waliohusika na kwa kuwfaikisha mahakamani ili haki itendeke.
Kuhusu makatibu wakuu wambao ndio watendaji, Dkt. Kijo-Bisimba alisema kuwa mawaziri hao walitakiwa kuwawajibisha makatibu wakuu pale wanapoona kwamba hawarishishwi na utendani wao wa kazi kwa kuwa wao ndio wapo nafasi za juu kiutendaji.
Mwenyekiti wa Chama cha PPT-Maendeleo, Bw. Peter Mziray, alisema wabunge wamemweka Rais Kikwete kwenye kona mbaya, hivyo ni lazima afanye mabadiliko kwa kuteua mawaziri ambao wananchi wanawaamini.
Pia alishauri baraza atakalounda Rais Kikwete, liwe dogo, kwani la sasa ni kubwa kiasi kwamba inawezaka wakati mwingine akashindwa kuwafahamu.
"Ndiyo maana waziri anaweza kuwa na mali nyingi, lakini akashindwa kufahamu kwa sababu hana muda wa kuwafuatilia," alisema Bw.Mziray.
Aliwataja mawaziri wanaofaa kuwemo kwenye baraza hilo kuwa ni Profesa Anna Tibaijuka, Dkt. John Magufuli, Dkt. David Matayo, Bw. Bernard Membe na Bw. Shamsa Vuai Nahodha.
Wakati huo huo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emanuel Nchimbi, amewaomba Watanzania kumuombea ili aweze kuteuliwa tena kurudi kwenye baraza la mawaziri.
Alisema bado ana moyo wa kuwatetea Watanzania katika mambo mbalimbali ili kuijenga nchi hii.
"Bado ninahitaji kuwasaidia Watanzania wenzangu na ninawapenda, ndiyo maana leo hii tena muda kama huu ambapo mawaziri wengi wapo katika sala za kumuomba Mungu wao ili waweze kupita tena, lakini mimi nimeamua kuja kwenu kwa ajili ya upendo wangu na ni moja ya kazi yangu,"alisema, Dkt. Nchimbi.
Aliongeza kusema kuwa angeweza kumtuma hata mwakilishi wake ili afike katika hafla ya uzinduzi wa mwongozi wa wamiliki na mameneja wa vyombo vya habari, lakini kwa kuwa anafahamu maana yake, ndiyo maana ameamua kufika mwenyewe.
Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) Bw. Regnald Mengi alimpongeza Dkt. Nchimbi kwa ujasiri wake wa kufika katika uzinduzi huo wakati mawaziri wengine hadi hivi sasa wapo matumbo joto wakiangaika huku na kule ili majina yao yaweze kupitishwa.
"Nakupongeza Dkt. Nchimbi kwa ushujaa ulioonesha ni mkubwa na mawaziri wengi sasa hivi matumbo joto kwa ajili ya kusikiliza kitakachotokea, tunakuona ni jasiri, "alisema Bw. Mengi.
SOURCE MAJIRA
Subscribe to:
Posts (Atom)



