Wednesday, April 18, 2012
KAJALA ASOMEWA MAELEZO YA AWALI
Na Rehema Mohamed
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jana ilimsomea maelezo ya awali msanii wa Filamu nchini, Kajala Masanja na mumewe Faraja Mchambo baada ya upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo.
Washatakiwa hao walisomewa maelezo hayo jana na wakili wa serikali kutoka Takukuru, Leornad Swai mbele ya Hakimu Sundi Fimbo anayesikiliza kesi hiyo.
Baada ya kusomewa maelezo hao washtakiwa hao walikiri mahakamani kuuza nyumba iliyokuwa chini ya uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Leornad Swai aliwasomea maelezo hayo ambapo washtakiwa walikiri kuwa ni mume na mke halali wa ndoa na kwamba walishirikiana kuuza nyumba hiyo kwa Emiliana Rugarulila.
Mchambo alikiri kwamba nyumba hiyo ilikuwa chini ya uchunguzi wa Takukuru na kwamba kabla hajafunguliwa mashtaka hayo alikuwa mtumishi wa Benki ya NBC.
Kadhalika, Mchambo amekiri kuhusika na akaunti za Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) lakini hakufanya utakatishaji wa fedha haramu kupitia akaunti hizo.
Katika hatua nyingine , Kajala na Mchamba walikana kupokea amri (notes) kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ikiwataka kutojihusisha na chochote ikiwemo kuuza nyumba hiyo kwa sababu ilikuwa chini ya uchunguzi wa Takukuru.
Aidha, wamepinga kushirikiana kuuza nyumba hiyo iliyozuiliwa kuuzwa na kwamba hawakwenda kinyume na amri iliyotolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Wakili Swai alidai kuwa baada ya washtakiwa kukana baadhi ya maelezo hayo, upande wa mashtaka unatarajia kuita mashahidi 13 na kuwasilishwa vielelezo tisa dhidi ya mashtaka yanayowakabili washtakiwa hao.
Katika kesi hiyo, washtakiwa wanadai kula njama kinyume na kifungu cha 34 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007 ambapo washtakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo la kula njama la kuamisha umiliki wa nyumba iliyopo Kunduchi Salasala jijini Dar es Salaam.
Shtaka la pili ni kwamba Aprili 14 mwaka 2010 waliamisha isivyo halali umiliki wa nyumba hiyo kinyume na kifungu cha 34(2)A(3) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007.
Ilidai shtaka la tatu ni la kutakatisha fedha ambalo walilitenda siku hiyo ya Aprili 14 mwaka 2010 huku wakijiua ni kinyume na sheria hiyo.
Kesi hiyo itaanza kusikilizwa ushahidi wa upande wa mashtaka Aprili 30, mwaka huu.
Soma Majira
Tuesday, April 17, 2012
OLE MILLYA ATUA CHADEMA
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha atua CHADEMA
MWENYEKITI wa UVCCM, Mkoa wa
Arusha,kwa miaka mitano, James Ole Millya,ametangaza kujiuzulu nafasi
zote kuanzia Taifa hadi Mkoa na kutangaza kujiunga na Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa madai kuwa CCM imefilisika
kimawazo na haitoi matumaini kwa watanzania.
Aidha
alisema hawezi kuendelea kupanda gari lenye pancha lukuki, hivyo
ameamua kupanda gari lisilo na pancha na lenye kutoa matumaini mapya
kwa watanzania.
Hayo ameyasema leo, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Kibo Palace, iliyopo Jijini hapa.
Amesema mara nyingi alikuwa
akikemea mambo ambayo yanaweza kubomoa chama cha CCM kwa upendo, lakini
alikuwa akipuuzwa kwa sababu ya chama hicho kuwa na kikundi cha wenyewe.
“Mimi nanukuu maneneo ya
Nyerere kuwa alishawahi kusema CCM sio mama yangu na mimi pia CCM sio
mama yangu na natangaza rasmi, kuondoka ndani ya chama hiki na najiunga
na Chadema, sababu ndicho chama chenye kuleta tumaini jipya kwa
watanzania,”alisema.
Ametaja nafasi alizoachia ngazi
ni pamoja na Mjumbe kamati ya utekelezaji UVCCM Taifa, Mjumbe kamati ya
siasa Mkoa na Mjumbe Halmashauri Kuu CCM Mkoa.
Amesema kuwa inasikitisha kuona
Vijana wa UVCCM Mkoa wa Pwani, wanatoa matamko kuwa Rais ajaye 2015
hatatoka kanda ya Kaskazini na anayemfahamu ni Rais peke yake ambaye ni
Jakaya Kikwete.
Millya alisema cha kusikitisha
pale alipokemea kauli hiyo alipuuzwa na hadi sasa Ikulu haijawahi kutoa
kemeo kwa Vijana hao na wala kukataza kauli hizo kutolewa, jambo
lililompa jibu kuwa Ikulu inahusika kwa namna moja au nyingine na kauli
hiyo.
Aidha alisema kuna Vijana wengi
walioko ndani ya CCM wakiishi kwa matumaini ya kusubiri kuteuliwa
nafasi ya Mkuu wa Wilaya kama sio Mkoa, ila yeye hawezi kuishi kw
amatumaini kama muathirika wa Ukimwi.
Hata hivyo alitoa wito kwa
Vijana wote wenye nia ya dhati na mapenzi mema ya nchi yao, kumfuata
Chadema ambako kunatoa tumaini jipya la maisha ya watu.
Sunday, April 15, 2012
TUZO ZA KTMA 2012 MLIMANI CITY JANA USIKU
![]() |
| MPOKI NDANI YA NYUMBA |
![]() |
| WASHERESHAJI MC, MILAJI NA VANESSA |
KHADIJA KOPA MUME WAKE NA WATOTO WAKE
![]() |
| KHADIJA KOPA AKITUMBUIZA |
BIBI CHEKA KATIKA POZI KTMA 2012
WATOTO WA KHADIJA KOPA WAKISHUKA JUKWAANI BAADA YA KUTAMBULISHWA NA MAMA YAO
ALI KIBAA AKIPOKEA TUZO YA WIMBO BORA WA ZOUK RHUMBA KUTOKA KWA DINA MARIOS WA CLOUD RAINFRED MASAKO WA ITV
Subscribe to:
Posts (Atom)










BI 

