JAMII NA MAISHA
Tuesday, January 1, 2013
SAJUKI HATUNAYE
MWIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ amefariki dunia asubuhi muda wa saa moja kasoro akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa .R.I.P
Tuesday, September 4, 2012
Friday, August 3, 2012
DKT. ULIMBOKA
Hali ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dkt. Steven Ulimboka, inaendelea vizuri lakini si wa kupona leo wala kesho, imeelezwa na vyanzo vyetu.
Dkt. Ulimboka anayetibiwa Afrika Kusini, yupo chini ya uangalizi mkali wa madaktari katika hospitali aliyolazwa na wanafanya kazi kubwa kuhakikisha anapona.
Chanzo chetu (gazeti la Uwazi) kimetoa taarifa kuwa, Dkt. Ulimboka anapata matibabu sahihi kwa sababu hospitali aliyolazwa ni ya uhakika.
Awali, kabla ya mazungumzo ya moja kwa moja kwenye simu, ripota wetu alimtumia SMS mtoa habari wetu kumuulizia maendeleo ya daktari huyo naye akajibu: "He's recovering slowly" (Anapona taratibu).
Alipomuuliza Watanzania wamtegemee lini daktari huyo kurudi nchini, alijibu: "Itachukua muda kupona. Muhimu kwa sasa ni Watanzania na wote wanaompenda, wamuombee kwa Mungu ili matibabu yaende sawa."
Chanzo chetu kilibainisha kuwa usalama wa Dkt. Ulimboka ni wa uhakika, kwani watu wanaomlinda hospitalini hapo wapo makini.
"Nani asiyejua mazingira ya hatari aliyonayo Steven (Dkt. Ulimboka)? Hii inasababisha maisha yake hospitalini yawe chini ya ulinzi mkali. Kwanza si kila mtu anaruhusiwa kwenda kumuona. Hospitali yenyewe aliyolazwa hatutaki itangazwe. Maisha ya Steven ni siri," alisema mtoa habari wetu na kutoa siri hii:
"Wiki iliyopita pale hospitali alipolazwa, alitokea mtu fulani hivi Mwafrika. Muonekano wake ukawafanya watu wahisi ni Mtanzania. Watu wanaohusika na usalama wa Steven walikuwa makini sana.
Kilichosababisha yule mtu aonekane ni Mtanzania ni fulana aliyovaa, kifuani ina ramani ya Tanzania. Watu wanaomlinda Steven wakaogopa sana, wakamfuatilia hatua kwa hatua bila mwenyewe kujua. Bahati nzuri naye alikuwa amekwenda kwa shughuli zake na akaondoka salama.
Kwa kifupi, hali ilivyo pale hospitali ni kwamba ulinzi ni mkali, tena afadhali mtu awe wa taifa lingine, Watanzania ndiyo wanaogopwa zaidi, kwani huwezi kujua nani mzuri wa Steven na adui yake ni yupi."
Taarifa kwa hisani ya Mpekuzi

Tuesday, July 24, 2012
Waziri ajiuzulu baada ya ajali ya meli Zanzibar
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Serikali ya Zanzibar Hamad Masoud Hamad amejiuzulu wadhifa wake, jana kufuatia ajali ya kuzama kwa meli ya MV Skagit iliotokea Julai 18, 2012. |
Hatuwa
hiyo imefikiwa baada ya rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein amekubali ombi la Waziri Hamad Masoud
kujiuzulu.
Kufuatia kujiuzulu kwa waziri huyo, Dk. Shein amemteua mwakilishi wa Jimbo la Ziwani kupitia Chama cha Wananchi, CUF, Bwana Rashid Seif Suleiman kuchukua nafasi hiyo.
Katika hatua nyingine makamu wa pili wa rais wa serikali ya Zanzibar balozi Seif ali idd ametangaza kusitisha safari zote za meli ya MV Karama ambayo inamilikiwa na Kampuni ya Sigal kufanya safari zake kati ya Zanzibar na Dar baada ya kubainika kwamba inauwezo wa kusafiri umbali wa kilometa saba pekee.
Wakati huo huo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein ameunda Tume ya kuchunguza ajali ya kuzama kwa meli ya MV Skagit.
Thursday, July 19, 2012
Taarifa ya meli kuzama Zanzibara
Jumatano, July 18, 2012
Taarifa ya Serikali Meli iliyozama
MAAFA YA KUZAMA KWA MELI ZANZIBAR
Meli ya Mv. Star Gate imezama
karibu na Kisiwa cha Chumbe ambapo watu 12 wamefariki hadi muda huu na
wengine kadhaa wamejeruhiwa.
Akitoa taarifa fupi kwa
waandishi wa habari,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi,Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini alisema taarifa za
kuzama kwa meli hiyo ilitolewa na Boti iendayo kasi ya Kilimanjaro III
iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Zanzibar ndipo ilipoiona meli
hiyo ikizama.
“Tulipata taarifa kutoka Boti
ya abiria ya Kilimanjaro III saa 7:50 mchana waliporipoti kuona meli
ikizama karibu na Kisiwa cha Chumbe” Alisema Waziri Mwinyihaji.
Waziri huyo alisema Meli hiyo
imezama maili sita kuelekea Kisiwa cha Yasin Kusini mwa Kisiwa cha
Chumbe kilichopo Unguja maili kadhaa kutoka Bandari ya Malindi.
Waziri Mwinyihaji alisema idadi
ya abiria walikuwa 250 ambao ni watu wazima, watoto 31 na mabaharia 6.
“Tumepeleka waokoaji, kuna boti tano zipo eneo la tukio kushirikiana na
waokoaji wengine” Alisema Waziri Mwinyihaji.
Alisema maiti zote zitapelekwa
viwanja vya Maisara Zanzibar kwa ajili ya ndugu na jamaa kuzitambua
maiti za ndugu zao ambapo majeruhiwa wote watatibiwa Hospitali Kuu ya
Mnazi Mmoja.
Katika Bandari ya Malindi
mwandishi wetu ameshuhudia maiti kadhaa zikiwemo za watoto zikishushwa,
Miongoni mwa abiria waliookolewa ni raia 13 wa Mataifa mbalimbali ya
nje huku raia mmoja ambaye hakuweza kutambuliwa utaifa wake amepoteza
maisha.
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar,
Balozi Seif Ali Idd alifika eneo la Bandari ya Malindi Zanzibar pamoja
viongozi wengine akiwemo Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir
Kificho, Mawaziri na baadhi ya Wajumbe a Baraza la Wawakilishi
walikuwepo kutoa msaada unaohitajika.
Katika eneo la pembezoni mwa
bandari ya Malindi, makundi ya wananchi yalikuwa yamekusanyika
wakisubiri taarifa za tukio hilo tangu saa 8:30 mchana.
Vikosi vya ulinzi na usalama, msalaba mwekundu na watoaji wengine wa misaada ya dharura walifika kwa haraka eneo la tukio.
Hadi sasa kazi ya uokoaji inaendelea karibu na Kisiwa cha Yasin ilikozama meli hiyo.
Meli ya Mv. Star Gate
inamilikiwa na kampuni ya kizalendo ya Sea Gull Sea Transport Ltd
ambayo mwaka 2009 Meli yake nyengine ya Mv. Fatih ilipinduka na kuzama
katika Bandari ya Malindi Zanzibar na kua watu sita.
Mwaka jana Zanzibar ilikumbwa
na maafa baada ya Meli ya Mv. Spice Islanders kuzama katika bahari ya
Hindi eneo la Nungwi katika Kisiwa cha Unguja ikielekea Kisiwani Pemba
ambapo taarifa rasmi ya Serikali ilisema watu 197 walipoteza maisha na
wengine wengi kujeruhiwa.
MELI YA SKAGIT YAZAMA
Meli ya Skagit inayomilikiwa na Kampuni ya Seagull imezama Maeneo ya Chumbe
Meli hiyo inayosadikiwa kuwa na abiria 250 inasemekana imepindukia upande mmoja na huku abiria wengi wakiweza kuokolewa kutokana na jitihada mbali mbali kupitia vile vile msaada wa boti za Mv Kilimanjaro, Tug ya Bandari na vyombo vyengine
Subscribe to:
Posts (Atom)