Wednesday, March 28, 2012

Mwakilishi Baraza la Wakilishi Zanzibar kuapishwa leo




Mwakilishi Baraza la Wakilishi Zanzibar kuapishwa leo


MWAKILISHI  mteule wa Baraza la Wawakilishi jimbo la Uzini, Mohammed Raza Daramsi ataapishwa leo katika kikao cha Barza la Wawakilishi kitakachoanza leo mjini Zanzibar.

Raza ataapishwa kufuatia kuibuka kidedea katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, uliofanyika mapema mwaka huu na Raza kuibuka na ushindi wa asilimia 61.




WAUZA CHIPSI IRINGA WADAIWA KUCHANGANYA MAFUTA YA KULA NA YA TRANSFOMA ZA UMEME




KUMEKUWA  na tabia ya baadhi ya wauza chipsi katika maispaa ya Iringa kuchanganya mafuta ya transfoma katika mafuta ya kukaangia chipsi jambo ambalo  ni hatari kwa afya ya binadamu..

Wakizugumzia suala hilo wauzaji wa chips katika maispaa ya Iringa wamesema kuwa ni kweli suala hilo lipo, kwa baadhi ya wengi wao wamekuwa wakifanya hivyo kutokana na kutafuta faida kubwa kwani mafuta hayo yakichanganywa hayaishi haraka.

Wafanyabiashara hao wameeleza jinsi chipsi hizo zinavyokuwa baada ya kuchanganywa mafuta hayo ya kawaida na transfoma kuwa chipsi hizo huwa nyeusi na pia hupoteza radha.

Hata hivyo wamewashauri wezao wanaofanya jambo hilo kuacha mara moja kwani madhara watakayoyapata walaji ni makubwa kutokana na mafuta hayo kuwa na kemikali. na madhara hayo ni kama vile kansa ya tumbo na kupata ugonjwa wa ngozi
Aidha kwa upande wake afisa afya manispaa ya iringa DEODATA LUKUPWA amesema kuwa hajawahi kupata malalamiko kama hayo ila ametoa agizo kwa wafanyabiashara hao wa chipsi ambao wanafanya hivyo kuacha mara moja ili kuokoa afya za walaji.


 

Tuesday, March 13, 2012

Airtel yazindua mtandao wa kasi zaidi



Airtel yaja na internet ya 3.75G kutoa ubora na kasi zaidi kwa wateja.

•    Airtel yajenga mtandao bora wa data barani Afrika
•    Uzinduzi wa Airtel 3.75G Tanzania utawapatia watumiaji  wa data
huduma yenye kasi na ubora zaidi  katika simu zao
•    Kupitia internet ya 3.75 itawawezesha wateja kufanya maongezi ya
simu ukiwa unamwona mtu, kuangalia TV, kutuma na kupokea barua pepe na
kuperuzi na kupata miziki kutoka kwenye tovuti kupitia simu zao.

Jumanne 13 Machi 2011, Dar es Saalam–Airtel Tanzania leo imepiga hatua
kubwa katika kujenga na kukuza mtandao wa technoloijia ya 3.75G Africa
kwa  kuzindua rasmi  mtambo wa 3.75G nchini Tanzania,ambapo Airtel
itatoa huduma ya internet yenye ubora na kasi zaidi  kwa watumiaji
wenye simu zenye uwezo wa kutumia internet wawapo mahali popote.

Mkurungenzi Mkuu wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Sam
Elangalloor alieleza” kukua kwa technolojia hii kutakuza ufanisi
katika vyombo mbalimbali vya  mawasiliano (multimedia), kwa kuwa 3.75G
itatoa internet yenye ubora na kasi  zaidi kwa  kuwezesha wateja
kufungua tovuti mbalimbali, kufanya maongezi  ya simu kwa njia ya
video , kuangalia TV, kutuma na kupokea barua pepe na pia  kupata
muziki kutoka kwenye tovuti  kwa kutumia simu.
Teknologia ya 3.75G itatoa nafasi kwa wateja kupata mawasiliano ya
data kwa njia tofauti na ya pekee kabisa, ndio maana leo Airtel
tunajisikia fahari kuwa internet yetu ya 3.75G ni uvumbuzi na
muendelezo wa mtandao (platform) wetu ili kuwawezesha wateja wa Airtel
wote nchini kupata huduma ya internet au data yenye ubora wa hali ya
juu pamoja na kasi zaidi”

Tunafanya ubunifu wa kuleta huduma zenye ubora zaidi katika mtandao
kwa kuzingatia kuwa sasaivi dunia inauhitaji mkubwa sana wa huduma za
kimtandao hasa kupitia simu ya mkononi
Ukirejea takwimu zilizofanywa na kampuni ya McKinsey & Co.

Telecommunications zinaonyesha  mpaka sasa kuna watumiaji wa simu za
mkononi wapatao milioni 400 Afrika, na kwamba bara la  Afrika ni moja
kati ya  soko linalokuwa kwa kasi zaidi huku soko la simu za mkononi
likiendelea kukua na kupanuka zaidi na kufikia kutoa huduma za
internet, huduma za benki kwa njia simu (mobile banking)  na biashara
kwa njia ya mtandao yaani (mobile commerce) .

Hivyo basi kwa kuzingatia hili,  ndio maana Airtel tunaendelea na
mikakati kama hii ya kuwaletea wateja internet yenye kasi zaidi ya
3.75G ambayo ni sambamba  na lengo letu la kuendea kupanua mtandao
ili kutoa mwanya wa mawasiliano kuwafikia wakazi wengi wa vijijini
ambao walikuwa wamesahaulika na mapinduzi ya mawasiliano katika bara
la Afrika.

“wote tunafahamu kuwa mawasiliano ni nyenzo muhimu kwa maendeleo ya
jamii ya sasa lakini bado kunachangamoto kubwa sana katika kupata
huduma hii kwa baadhi ya sehemu barani Africa. Lakini tukumbuke
Mawasiliano ni haki ya msingi kwa kila mtu na si vinginevyo hivyo kwa
kupitia mtandao wa Airtel internet yenye kasi zaidi ya 3.75G ninaamini
tutaweza  kuunganisha idadi kubwa ya watu kwa kukuza mahusiano ndani
na nje ya ya jamii zetu, kuendeleza na kuutangaza utamaduni wetu,
pamoja na kupanua wigo wa wale wanaofanya biashara kupitia mtandao wa
internet “ Aliongeza Elangalloor.

Ikiwa tayari mteja ameunganishwa na teknologia ya 3.75G simu yake
itaonyesha 3.75G, HSDPA, WCDMA or HSPA. Hii inategemeana  na Aina ya
simu aliyonayo mtumiaji lakini kasi ya kuunganishwa ni yenye ubora
zaidi.

Airtel itaendelea kuwekeza kwenye huduma ya data katika soko lake lote
huku lengo likiwa ni kuwa mtandao mpana zaidi wa teknologia ya 3.75G
katika bara zima, na itaendelea kutoa huduma bora na inayokidhi
mahitaji ya watumiaji

WACHEZAJI WA TATU WA YANGA WAFUNGIWA


Waandishi Wetu

WACHEZAJI zaidi ya watatu wa Yanga, huenda wakafungiwa miezi mitatu kucheza soka kutoka na kitendo chao cha kumpiga mwamuzi, Israel Mujuni katika mechi yao dhidi ya Azam iliyopigwa  mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Katika mchezo huo uliomalizika kwa Yanga kulala mabao 3-1, uliingia mushkeli dakika ya 13 baada ya Haruna Niyonzima kupewa kadi nyekundu kwa kile kilichoelezwa kuzozana na mwamuzi na kumtolea lugha chafu.

Wachezaji ambao rungu la Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, ni dhahiri litawaangukia ni Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Stephano Mwasika na Nurdin Bakari wakati Jerry Tegete huenda naye akaangukiwa na hilo baada ya kutaka kuingia ndani ya uwanja kwa nia ya kumdhuru mwamuzi. Hata hivyo alizuiwa na wachezaji wenzake wa akiba.

Haruna Niyonzima atakosa mechi tatu kama kanuni zinavyosema. Hata hivyo, Kamati ya Ligi ya TFF itakayokutana wiki hii, itaamua vinginevyo.
Nahodha wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, Athumani Idd ‘Chuji’, Omega Seme na Hamisi Kiiza walifanya kazi ya ziada kuwazuia wachezaji hao pamoja na daktari wa timu, Juma Sufiani.

Wachezaji hao wanabanwa na Kanuni ya 25 ya udhibiti wa wachezaji kipengele (F) kifungu cha (iii) kinachosema, mchezaji yeyote atakayemshambulia mwamuzi au kiongozi yeyote kwa namna yoyote ile, iwe kwa matusi au kwa kumgusa, ataadhibiwa kwa kufungiwa kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu hadi 12, kufungiwa kucheza michezo kadhaa, kupigwa faini kwa mujibu wa Kanuni ya 31 au vyote kwa pamoja.

TFF kupitia msemaji wake, Boniface Wambura alisema Kamati ya Ligi inakutana katikati ya wiki hii baada ya kupokea taarifa ya kamisaa wa mchezo huo.

Wambura alisema jana kuwa tayari wamepokea taarifa hiyo kutoka kwa kamisaa wa mchezo na tayari wameiwasilisha kwa Kamati ya Ligi.

“Tayari ripoti imefika kwetu na tulichokifanya sisi ni kuipeleka kwa wahusika wa mwisho ambao ni Kamati ya Ligi chini ya Wallace Karia pamoja Godfrey Nyange na wenzake ambapo wataipitia kwa makini kabla ya kuitolea maamuzi.


“Naamini yote yatakayofanyika yataenda sambamba na adhabu kwa watu waliohusika na vurugu zile ndani na hata nje ya uwanja,” alisema Wambura.
Mbali na vurugu hizo, kulikuwepo na uharibifu wa mali za uwanja na baadhi ya mashabiki wa Yanga walikuwa wakirusha viti uwanjani ikiwa ni siku chache baada ya Serikali kuagiza Simba kulipa Shilingi5 milioni kwa kuvunja viti wakati wa pambano lao dhidi ya Kiyovu.

Ukiacha baadhi ya wachezaji hao kuadhibiwa, klabu ya Yanga italazimika kulipa gharama za uharibifu huo uliofanywa na mashabiki wake kwa kung’oa viti na miundombinu mingine.

Katika hatua nyingine, kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima amewaomba radhi mashabiki na wapenzi wa soka nchini kwa kitendo kilichotokea mwishoni mwa wiki walipocheza na timu ya Azam na kusababisha vurugu huku akidai hakumjibu lolote mwamuzi Israel Nkongo



“Nawaomba msamaha mashabiki na wadau wote wa soka hapa nchini kutokana na vitendo vya vurugu vilivyotokea kwenye mchezo ule na nawaahidi hakiwezi kutokea tena” alisema Niyonzima.

Aliongeza kusema kuwa mashabiki wasikate tamaa kwani wamekosa mchezo ule lakini bado wana michezo mingine na kikosi kipo vizuri hivyo watafanya vizuri kwenye mchezo ujao na kuhakikisha wanatete ubingwa wao.
Source: Mwananchi

KAMPENI ZA UBUNGE ARUSHA

Waandishi Wetu, Arumeru


MJI wa Usa River katika Wilaya ya Meru jana ulitikiswa na kishindo cha uzinduzi wa kampeni za CCM, ulioongozwa na Mwenyekiti wake Mstaafu, Benjamin Mkapa.Katika mkutano huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ngaresero, Mkapa alikanusha kuwa na ubia na kampuni ambazo zimewekeza katika maeneo makubwa ya ardhi ya Meru.

Suala la migogoro ya ardhi ni miongoni mwa matatizo makubwa yanayowakabili wananchi wa wilaya hii na jana Mkapa alitumia sehemu kubwa ya hotuba yake kukanusha kwamba ana ubia na wale aliowaita kuwa ni walowezi katika wilaya hiyo.

 “Kwanza kabisa nataka niweke mambo sawa, nimesikia kwamba ninahusishwa na hawa wamiliki wa ardhi, eti kina nani hawa… ndiyo Jerome sijui Jerome, huu ni uzushi na hauna ukweli wowote,” alisema Mkapa alipokuwa akimnadi mgombea wa CCM, Sioi Sumari na kuongeza:


“Mimi katika nchi hii sijawahi kumpokonya mwananchi yeyote shamba, wala kumnyanyasa Mtanzania yeyote kwa kumpokonya ardhi, nimekuwa mtetezi wa kuhakikisha kila watu wanapata haki ya matumizi yao ya ardhi, haya maneno mengine ni uzushi na upuuzi wa hali ya juu.”

Alisema amepokea taarifa za kuwapo kwa migogoro mikubwa ya ardhi inayosababishwa na baadhi ya wawekezaji kuhodhi maeneo makubwa na kusema atalifikisha kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na kumshauri achukue hatua kwa kuwawajibisha watendaji wa Serikali ambao wameshindwa kuwajibika na kuchukua hatua kwa wawekezaji waliokiuka masharti.


 “Yapo matatizo kadha wa kadha, wapo wawekezaji ambao wamehodhi maeneo makubwa wakati hawayatumii, wapo ambao wamechukua maeneo na kubadilisha matumizi yake na wapo ambao wamekiuka sheria za uendeshaji wa maeneo waliyopewa,” alisema Mkapa na kuongeza:

 “Yote haya nimeyapokea na nitayafikisha kwa Mwenyekiti wangu wa CCM ambaye pia ni Rais wangu ili ayashughulikie baada ya uchaguzi maana tukifanya sasa, hawa wenzetu (wapinzani) watasema tumewahonga wananchi.”

Aidha, Mkapa alikanusha taarifa kwamba alitoa masharti baada ya kuombwa kuongoza uzinduzi wa kampeni hizo za CCM: “Mimi ninamheshimu sana Mwenyekiti wangu wa CCM na uamuzi wa Kamati Kuu ya chama maana nimezaliwa CCM na kukulia ndani ya CCM. Kwa maana hiyo siwezi hata siku moja kuhoji au kutoa masharti pale ninapoombwa na chama kutekeleza jukumu lolote.”

Shamrashamra
Shamrashamra za CCM zilianza asubuhi kwa magari na pikipiki zilizopambwa kwa bendera za kijani na njano kupita katika mitaa mbalimbali ya Usa River, zikiwahamasisha wakazi wa mji huo kuhudhuria uzinduzi huo.

Mapema viongozi kadhaa wa chama hicho walitawanyika katika kata zote 17 za Arumeru Mashariki kulifanya mikutano ya ndani kwa lengo la kuwaweka sawa makada wao ambao wanadaiwa kuchanganywa na taarifa kwamba chama hicho kimegawanyika kuhusu mgombea wao, Sioi Sumari.

Baadaye mchana, msafara wa mgombea huyo wa CCM ulianza kuelekea katika eneo la mkutano ukitokea katika Hoteli ya Gateway ukisindikizwa kwa magari na pikipiki.

Kabla ya msafara huo kuondoka, kulikuwa na kikao cha ndani kilichofanyika hotelini hapo kikiwahusisha viongozi wa chama hicho na taarifa za ndani zinadai kwamba kilikuwa kikipanga mikakati ya mkutano huo wa uzinduzi.

Msafara huo ulitoka hotelini hapo saa 9.15 alasiri na kuingia Barabara Kuu ya Arusha-Moshi, njia ya Leganga na kuelekea moja kwa moja katika Ngarasero.

Wakati msafara huo ukiwa Barabara ya Leganga ukielekea uwanjani, ulipita karibu na kambi waliyofikia viongozi mbalimbali wa Chadema na baadhi ya makada wa chama hicho walijitokeza na kuzomea msafara huo.

Msafara huo uliwasili uwanjani hapo robo saa baadaye na viongozi wake waliungana na wanachama wao waliokuwa uwanjani hapo tayari kwa uzinduzi.

Wapinzani wa Sioi
Katika uzinduzi huo, CCM kiliwapandisha jukwaani baadhi ya wanachama wake waliokuwa wapinzani wa Sioi kwenye kura za maoni. Makada hao ni Elishilia Kaaya, Elirehema Kaaya na William Sarakikya na wote waliuthibitishia umma kumuunga mkono mgombea huyo wa CCM.

Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa aliwaomba wana Arumeru Mashariki kulinda mila na desturi iliyojengeka ndani ya taifa kuwa inapotokea kiti cha uongozi kama ubunge kinachomilikiwa na CCM inabaki wazi, mrithi atoke ndani ya chama hicho.

“Mila na desturi zinataka mrithi wa kiti kinachomilikiwa na CCM kirithiwe na mrithi kutoka CCM. Mchagueni Sioi kutekeleza hilo ili ashirikiane na wenzake bungeni kutatua matatizo yenu,” alisema.

Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama alisema tayari chama hicho kimetekeleza ahadi na deni kililokuwa nalo kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, marehemu Jeremia Sumari ambaye ni baba mzazi wa Sioi kwa kulipa Jimbo la Arumeru Mashariki hadhi ya kuwa wilaya kamili kichama.
Vijembe kwa Chadema

Meneja wa kampeni za CCM Arumeru Mashariki, Mwigulu  Nchemba aliwapiga vijembe viongozi wa Chadema akimwomba Mkapa kumsihi Rais Kikwete awateue Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi ili wasije kulalamika pale mgombea wao atakaposhindwa.

Mwigulu alitumia maneno mengi ya kejeli kwa Chadema na mgombea wake, Joshua Nassari kwa kumfananisha na vitu kama shetani, gunzi na vinyamkera huku akiwasihi wapiga kura kutomchagua mgombea huyo.


Nchemba ambaye pia ni Katibu  wa Uchumi na Fedha wa CCM, alisema CCM kina uhakika wa ushindi katika jimbo hilo kwani mgombea wake, anakubalika.
Alisema licha ya kuwepo matatizo kadhaa Arumeru, hoja si kusema kwa ukali, bali ni kuwa na mipango ya kukabiliana na matatizo hayo… “Chagueni mtu ambaye atasikilizwa na Serikali na mtakayeshirikiana naye kutatua matatizo na sio mtu ambaye anasema kwa ukali ambaye anapotosha jamii.”

Kuhusu uchangishaji wa fedha uliofanywa na Chadema wakati wa uzinduzi wa kampeni, alisema ni kejeli kwa wananchi kuwachangisha Sh50 wakati wanatumia helikopta ambayo kwa saa moja angani gharama zake ni Sh2.5 milioni na Sh15 milioni kwa siku.


Ahadi za baba
Mgombea huyo wa CCM, alisema kipaumbele cha kwanza akichaguliwa ni kutekeleza ahadi zote alizoacha baba yake…

“Najua nina deni kwenu, mkinichagua nitahakikisha ninakamilisha ahadi zote za baba kama kukamilisha Barabara ya Ngabobo, ujenzi wa nyumba ya wazee wa mila, kukamilisha ujenzi wa vyoo katika shule na kukamilisha ujenzi wa Shule ya Wasichana ya Songoto.”


Mgombea huyo pia alisema ajenda kubwa ambayo atatekeleza baada ya kuchaguliwa itakuwa ni kushughulikia matatizo ya maji na ajira kwa vijana katika jimbo hilo.
 SOURCE MWANANCHI

RAIS KIKWETE ATOA AHADI KWA MADKTARI

 SAKATA LA MADAKTARI

RAIS Jakaya Kikwete amesema atahakikisha anajenga hali ya kuaminiana katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii baada ya kubaini kuwepo kwa tatizo hilo alipokutana na viongozi wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), hivi karibuni.

Rais alikutana na madaktari hao Ijumaa iliyopita baada ya kuitisha mgomo kwa mara ya pili, safari hii wakishinikiza Waziri wa Afrika na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda na Naibu wake, Dk Lucy Nkya wajiuzulu au wawajibishwe kabla ya kuendelea na mazungumzo ambayo yalikuwa yameanza ikiwa ni utekelezaji wa kumaliza mgomo wa kwanza.

Alisema baada ya mazungumzo hayo alichobaini ni kutoaminiana na kuahidi kulifanyia kazi suala hilo kwa kutengeneza mazingira mazuri yatakayowezesha watumishi kufanya kazi kwa kushirikiana.

Akizungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alitumia muda mrefu kueleza mlolongo mzima wa mgogoro huo na jinsi Serikali ilivyoushughulikia na kisha kuelezea jinsi alivyokutana na madaktari hao.

Akielezea mazungumzo kati yake na madaktari hao, Rais alisema aliwaomba wampe sababu za msingi ambazo zimekuwa zikiwafanya wamtake awawajibishe mawaziri hao kabla ya kuendelea na mazungumzo akisema kabla ya mazungumzo hayo hakuwa ameona tuhuma za msingi za kuwang’oa mawaziri hao licha ya kuwa na mamlaka ya kufanya hivyo.

“Nikawaambia nielezeni kwa kina sababu za kutaka niwaondoe vinginevyo mtajikuta na ninyi mnaambiwa mna sababu zenu za kisiasa,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:

“Hoja yao moja ilikuwa ni kwamba wangependa kuzungumza na watu wapya, lakini mimi nikawaambia ni vizuri wakazungumzia zaidi matatizo yao ya kimfumo ili hata akija mwingine mambo yao yasiharibike.”

Alisema mawaziri ni watu wanaopita katika wizara akito mfano wa Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli kwa kusema: “Magufuli alianza Wizara ya Ardhi, baadaye akaenda wizara ya samaki na ng’ombe, sasa hivi yuko wizara ya barabara... sasa jambo la msingi ni kuzungumza matatizo yenu. Hawa ni watu wa kupita na uchaguzi ni miaka mitatu ijayo hivyo mawaziri wataondoka na madaktari watabaki. Nimewaeleza kuwa wao wapo tu.”



Awali, Rais Kikwete alielezea kusikitishwa kwake na hatua ya madaktari hao kugoma akisema hatua yao ilikuwa ni kinyume cha sheria na kanuni za utumishi ambazo licha ya kubainisha hatua zinazopaswa kuchukuliwa kabla ya wafanyakazi kugoma, watumishi wa kada hiyo hawatakiwi kisheria kuchukua hatua hiyo.

Awashukia wanaharakatiKatika hotuba hiyo Rais Kikwete aliwashukia wanaharakati wa haki za binadamu kwa kushabikia mgomo wa madaktari kwa kuishutumu Serikali badala ya kuwataka madaktari kurejea kazini kuokoa roho za binadamu akisema: “Haki ya kwanza ya binadamu ni kuishi.”

“Humu katikati ya mgomo kukajitokeza mambo mengi, adui yako muombee njaa... wakajitokeza hawa wanaojiita wanaharakati na kuanza kushabikia mgomo, hii imenishangaza sana. Nashangaa wanaharakati wa haki za binadamu kujiingiza kwenye hili.

Hivi kuna haki gani kubwa zaidi ya haki ya kuishi? Hii ndiyo haki ya kwanza.”
Rais  alisema wanaharakati wamemfedhehesha kwa kuwa hata kama wangekuwa na ajenda za kisiasa, kwenye suala la mgomo wa madaktari hawakutakiwa kutafuta umaarufu

.UteteziAkizungumzia hotuba hiyo ya Rais, Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Helen Kijo-Bisimba alisema harakati zao zililenga kuitaka Serikali iwasikilize madaktari ili wamalize mgomo na warudi kazini.

“Sisi tulikuwa tunataka Serikali iwasikilize madaktari. Vipo vingi tu ambavyo Rais hajavizungumzia ikiwemo mazingira magumu ya kazi, ukizungumza na madaktari watakwambia kuwa kuna vifaa muhimu wanakosa na wagonjwa wanawafia mikononi,” alisema na kuongeza:

“Kuna daktari aliniambia kwa siku hata wagonjwa wanane wanaweza kumfia mbele ya macho yake kwa kukosa vifaa vidogo tu ambavyo vingeweza kuokoa maisha yao. Kwa mfano, mwanamke mjamzito akikosa kuchomwa sindano ya kukata damu baada ya kujifungua yote haya hajayazungumzia.”


Alisema hoja kubwa ya wanaharakati ilikuwa ni kutaka madaktari wasikilizwe haraka na Serikali ili warudi kazini kuokoa maisha ya watu.


“Mwenyewe amekiri kuwa madaktari ni watu muhimu, sasa kwa nini walikuwa hawashughulikii matatizo yao kwa haraka? Wanayashughulikia tu kama vile ni madereva wa trekta wamegoma, kama wanajua ni muhimu ilibidi wakikohoa tu wasikilizwe, mshahara wanaosema waliongezewa Serikali ilifanya hivyo baada ya mgomo wa mwaka 2005,” alisema

SOURCE MWANANCHI

Friday, March 9, 2012

MWAKILISHWA WA PAPA AKABIDHI HATI YA UTAMBULISHO KWA KIKWETE

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

AFYA YA LOWASSA

Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa
ATHIBITISHA YUKO HOSPITALINI, ASEMA ASINGEPENDA KUELEZEA KWA UNDANI KUHUSU AFYA YAKE
Ramadhan Semtawa
UTATA umegubika afya ya Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa baada ya taarifa mbalimbali kueleza kuwa yuko hospitalini nchini Ujerumani kwa matibabu.Takriban juma moja sasa kumekuwa na taarifa mbalimbali zikizungumzia afya ya Lowassa lakini hakukuwa na taarifa rasmi kutoka chanzo chochote kati ya Serikali, familia yake au Bunge kuzungumzia afya ya Mbunge huyo wa Monduli.

Jana, Lowassa akizungumza na mwandishi wetu kwa simu alisema kwamba yuko hospitali, bila kufafanua kuwa ni nje au ndani ya nchi, wala kueleza kinachomsibu.

Mahojiano hayo kati ya Lowassa na mwandishi wetu yalikuwa kama ifuatavyo:

Swali: Asalaam alaykum Mheshimiwa Lowassa.
Jibu: Waalaykum Salaam.

Swali: Mimi naitwa... (jina la mwandishi) kutoka gazeti la Mwananchi. Kwanza pole kwa matatizo ya kiafya yanayokusumbua.
Jibu: Ahsante.

Swali: Nimekupigia pamoja na kukupa pole, nilitaka kujua unaendeleaje na matibabu?
Jibu: Niko hospitalini kwa sasa naomba niache mambo mengine tutaongea baadaye.

Swali: Lakini, ni matibabu gani hasa unayopata?
Jibu: ... (akimtaja mwandishi) naomba niache niko hospitalini sasa hivi mambo mengine tuongee baadaye.

Lowassa alitoa majibu hayo majira ya saa nane mchana na alipopigiwa tena saa 10.20 jioni, alijibu kama ifuatavyo:

Swali: Naam, Mheshimiwa Lowassa nimekupigia tena mimi... (mwandishi akajitambulisha).
Jibu: ... Unataka nikuambie nini tena? Nilishakwambia niko hospitalini niache!

Swali: Sawa, natambua uko hospitalini, lakini wewe ni kiongozi ambaye umewahi kuwa Waziri Mkuu, hivyo Watanzania wangependa kujua maendeleo ya afya yako kutokana na utata ulioibuka na kama je, umelazwa hapo hospitalini au uko katika matibabu ya kawaida?
Jibu Niache, ninachokwambia niko hospitalini sasa unataka nini tena? Nisingependa kuzungumzia afya yangu kwa undani.

Bunge

Akizungumzia suala hilo juzi, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashillilah alisema ofisi hiyo haijapata maombi rasmi ya mbunge huyo kwenda nje kwa ajili ya matibabu.

Dk Kashillilah alisema kwa utaratibu, Ofisi ya Bunge inashirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa ajili ya kuwapeleka wabunge wanaoumwa nje ya nchi baada ya kupata rufaa ambayo inatokana na ushauri wa kitaalamu wa madaktari wa ndani.

Alisema hadi juzi, hakuwa akijua aliko Lowassa na kama ana matatizo ya kiafya kama inavyozungumzwa au la: “Mimi ndiyo Ofisi ya Bunge na ndiyo nakwambia hatujapata maombi ya kutaka mheshimiwa Lowassa apelekwe nje ya nchi.”

Mtendaji huyo mkuu wa Bunge alisema wapo baadhi ya wabunge ambao huwa wanakwenda nje kwa vipindi maalumu kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kawaida wa afya baada ya matibabu lakini, katika orodha hiyo Lowassa hayumo.

“Tunao utaratibu wa baadhi ya waheshimiwa wabunge kwenda nje kwa mujibu wa ratiba zao kwa ajili ya kufanyiwa uangalizi wa kawaida wa afya zao. Lakini, hadi sasa (juzi) katika orodha hiyo mheshimiwa Lowassa hayumo,” alisema Dk Kashillilah.

Hata hivyo, kwa mujibu wa nafasi yake ya utumishi serikalini aliyokuwa nayo, Lowassa anaweza kupata matibabu nje ya nchi kwa kupitia utaratibu wa Serikali bila ya kuhusisha Bunge.

Juhudi za kupata Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda au Naibu wake, Dk Lucy Nkya zilishindikana kutokana na simu zao kufungwa na kutopatikana ofisini.Chanzo;gazeti la Mwananchi.

Thursday, March 8, 2012

KINDNESS,UPOLE



Kindness is the language which the deaf can hear and the blind can see - Mark Twain

KADI YA MWANAMKE 2012

WANAWAKE WAKIWA KATIKA SHUGHULI ,SIKU YA WANAWAKE DUNIA


WANAWAKE TUKUMBUKE SISI NI NGUZO KATIKA JAMII 
HERI SI  WANAWAKE WOTE  DUNIANI KWA WANAWAKE WOTE NA WAPENDA


isha kama umeguswa.

NOTE:Kama ni mtu wa kuchukua mambo kirahisi bila kufikiri kwa kina unaweza kuhisi ni maswali yasiyo na maana.Ila ni maswali makubwa sana unayotakiwa kujiuliza.


Body shape affects memory in older women




Study: Body shape affects memory in older women

(CNN) -- A woman's body shape may play a role in how good her memory is, according to a new study.

The more an older woman weighs, the worse her memory, according to research released this week from Northwestern Medicine at Northwestern University in Evanston, Illinois.

The effect is more pronounced in women who carry excess weight around their hips, known as pear shapes, than women who carry it around their waists, called apple shapes.

The reason pear-shaped women experienced more memory and brain function deterioration than apple-shaped women is likely related to the type of fat deposited around the hips versus the waist.

Scientists know that different kinds of fat release different cytokines -- the hormones that can cause inflammation and affect cognition.

"We need to find out if one kind of fat is more detrimental than the other, and how it affects brain function," said Dr. Diana Kerwin, the lead author of the study and an assistant professor of medicine and a physician at Northwestern Medicine. "The fat may contribute to the formation of plaques associated with Alzheimer's disease or a restricted blood flow to the brain."

The study published in Wednesday's Journal of the American Geriatric Society said, on average, there is a one-point drop in the memory score for every one-point increase in body-mass index -- a ratio of a person's height and weight. The study included 8,745 cognitively normal, post-menopausal women ages 65 to 79.

"Obesity is bad, but its effects are worse depending on where the fat is located," Kerwin said.

"The study tells us if we have a woman in our office, and we know from her waist-to-hip ratio that she's carrying excess fat on her hips, we might be more aggressive with weight loss," Kerwin said. "We can't change where your fat is located, but having less of it is better."

UNYANYASAJI WA WANAWAKE

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI NA UKATILI WA KIJINSIA

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 2012

ASHA ROZE MIGIRO

ANNA MAKINDA
TIBAIJUKA
MAMA SALMA KIKWETE


Historia ya Siku ya Wanawake Duniani

SIKU ya Wanawake Duniani ni sherehe katika nchi nyingi duniani. Ni siku ambayo wanawake hutambuliwa kwa ajili ya mafanikio yao bila kujali mgawanyiko wa Taifa, kabila, lugha, kitamaduni, kiuchumi au kisiasa.

Ni tukio ambalo hukumbusha jitihada za nyuma na mafanikio, na muhimu zaidi, kwa ajili ya kuangalia mbele kwa uwezo wa wanawake waliopita kwa kizazi kijacho.

Umoja wa Kimataifa ulianza kusherekea siku hii Machi 8 mwaka 1975, na miaka miwili baadaye, Desemba 1977, Baraza Kuu la UN lilipitisha na kutangaza Siku ya Haki za Wanawake na Amani ya Kimataifa kuadhimishwa siku yoyote ya mwaka kwa kabila la ‘medlemsstater’.

Kwa mujibu wa mila yao, walipitisha azimio la Baraza Kuu lililotambua jukumu la wanawake katika juhudi za amani na maendeleo, wito wa mwisho kwa ubaguzi na ongezeko la msaada kwa ajili ya ushiriki wa wanawake.

Siku ya Wanawake kwa mara ya kwanza iliibuka katika shughuli za harakati za kazi, karne ya ishirini, Amerika Kaskazini na Ulaya.

Mwaka 1909, wanawake walifanya mgomo kupitia chama cha kisosholisti kupinga mazingira magumu ya kazi.

Mwaka 1910, ilikuwa siku ya kimataifa ya kijamaa ambapo ulifanyika mkutano maalumu wa Copenhagen, kwa ajili kudai haki ya kupiga kura, kwa heshima ya harakati na haki za wanawake pia, kujenga msaada kwa ajili ya kufanikisha haki ya kupiga kura kwa wote.

Mkutano huo uliudhuriwa na zaidi ya wanawake 100 kutoka nchi 17 duniani pamoja na kuchagua wanawake wawakilishi wa madai yao ambapo hawakuweka saini ya siku maalumu maadhimisho ya siku hiyo.

Mwaka, 1911 matokeo ya mkutano wa Copenhagen yalitangaza Siku ya Wanawake Duniani mara ya kwanza Machi 19 katika nchi za Austria, Denmark, Ujerumani na Uswisi, ambako zaidi ya wanawake milioni moja na wanaume walihudhuria mikutano ya kampeni za uchaguzi.

Mbali na haki ya kupiga kura na kushikilia ofisi ya umma, wanaume  walidai haki za kazi kuwa sawa na za wanawake, mafunzo ya ufundi na ya mwisho ya ubaguzi kwa kazi.

Mwaka 1913 na 1914, ni kumbukumbu muhimu kwa Siku ya Kimataifa ya Wanawake  kupinga Vita ya kwanza ya dunia, kama sehemu ya harakati za amani.

Nchini Urusi husherekea siku hiyo kila jumapili ya kwanza ya mwezi februari, Ulaya mwaka uliofuata Machi 8 kwa lengo la kuanzisha kampeni maalumu ya kupinga vita na kuonyesha mshikamano na wanaharakati wengine.

Mwaka 1917 ilikuwa siku maalumu nchini Urusi kwa wanawake kupinga  kuongezeka kwa vita, iliyojulikana kwa jina la ‘mikate na amani' iliyofanyika siku ya Jumapili februari (ambayo ilikuwa ni tarehe 8 Machi kwenye kalenda ya Gregorian).

Siku nne baadaye, serikali ilianza kutoa nafasi kwa wanawake kuanza kupiga kura.

Tangu mwaka huo, Siku ya Wanawake Duniani imekuwa na mwelekeo mpya wa kimataifa kwa ajili ya wanawake katika nchi zinazoendelea na zilizoendelea.

Idadi ya wanawake wanaharakati imekuwa ikiongezeka na kuwa nguvu na mikutano ya nne ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa ya wanawake.

Wanaharakati wamesaidia kufanya maadhimisho kila hatua kwa kutegemea kujenga msaada kwa ajili ya haki za wanawake na kushiriki katika masuala ya kisiasa na kiuchumi.

Siku ya Wanawake Duniani ni wakati wa kutafakari juu ya mafanikio yaliyopatikana, kuwaita kwa ajili ya mabadiliko na kusherehekea vitendo vya hamasa na ujasiri katika shughuli za kila siku.

Umoja wa Mataifa na usawa wa jinsia

Mkataba wa Umoja wa Mataifa, uliosainiwa mwaka 1945, ulithibitisha kanuni ya usawa kati ya wanawake na wanaume.

Tangu wakati huo, UN  ilisaidia kujenga urithi wa kihistoria wa kimataifa kukubali mikakati na viwango vya mipango na malengo ya kuendeleza hali ya wanawake duniani.

Umoja wa Mataifa na mashirika yake imekuza ushiriki wa wanawake kama washirika sawa na wanaume katika kuleta maendeleo endelevu, amani, usalama, na heshima kwa ajili ya haki za binadamu.

Pia, imewawezesha kuendelea kuwa kipengele kati ya juhudi za Umoja wa Mataifa kushughulikia changamoto za kijamii, kiuchumi na kisiasa duniani kote.

Kila siku ni Siku ya Mwanamke Duniani, Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon anasema, "kila  siku ni Siku ya Wanawake duniani, kwani mwanamke ni kigezo kikubwa kuongeza pato la taifa na kukuza uchumi wa dunia basi kwa misingi hiyo kila siku muhimu kwakwe.

"Mfano mwanamke wa kijijini ana nafasi kubwa ya kuleta maendeleo  kijijini kwake na  katika taifa kwa njia ya kilimo,".

Mwanamke akipatiwa mahitaji yote muhimu kama miundo mbinu, zana bora za kilimo na muongozo basi anaweza kufanya mabadiliko ya uchumi kuanzia ngazi ya chini mpaka juu.

Hata hivyo sera na mipango iliyowekwa na serikali iweze kweli kumnufaisha mwanamke, ikiwamo mpango mkakati wa kilimo .

Hivi karibuni mawaziri wanaohusika na masuala ya maendeleo ya wanawake kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, walikutana kujadili masuala hayo  ambapo, walikubadilishana mawazo kuhusu hali ya wanawake  wa vijijini.

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Un, Dkt.Asha Roze Migiro anasema, "Ukweli ni kwamba wanawake wa vijijini wanaendelea kukabiliwa na vikwazo vingi vikiwamo ya upatikanaji wa ardhí, pembejeo za kilimo, mitaji, huduma za kijamii na teknolojia za kisasa”


Kauli mbiu ya mkutano huo ilikuwa, "Nafasi ya  wanawake wa Vijijini na Mchango wao katika Kupambana na Umaskini na Njaa,".

Lengo la pili  ni namna gani wanaweza kuwezeshwa ili wapate nguvu ya kuwa kichocheo cha maendeleo endelevu.

Kauli mbiu ya kimataifa siku ya wanawake duniani  2012 ni "Uwezeshaji wa wanawake wa kijijini utasaidia kumaliza njaa na umaskini," Nchini,  "Ushiriki wa mtoto wa kike ni chachu ya maendeleo".

Kama wanawake wa vijijini wangepewa fursa sawa  ya kupewa nyenzo za  uzalishaji, basi uzalishaji wa mazao ya kilimo ungeongezeka kwa asilimia kubwa na kiwango cha njaa kingepingua.

Bado mwanamke huchukuliwa kama msaada mkubwa wa kupunguza njaa katika mataifa mbalimbali japokuwa mchango wake hautambuliwi.

Anasema, bado wanawake wa vijijini wanaendelea kukabiliwa na  ugumu  katika upatikanaji wa  huduma za msingi zikiwano za  ulinzi wa jamii, ajira na masoko ya uhakika.

Dkt.Migiro anasema, taifa liweke  mikakati itakayowawezesha wanawake wa maeneo ya vijijini kuongeza uwezo wao kupambana na umaskini uliokithiri, njaa na kujiletea maendeleo endelevu katika familia zao.

Anasema, ili hayo yaweza kufanikiwa ni lazima jamii itambue kwamba wanawake ni mawakala muhimu wa mabadiliko.

Pia, wakisaidiwa katika jumuiya zao kutasaidia  katika kuhakikisha kwamba, matakwa na vipaumbele vya wanawake wa vijijini  yanapewa umuhimu unaostahili.

Anasema, ili sera, na mipango iliyowekwa na serikali iweze kweli kumnufaisha mwanamke, ikiwamo kaulimbiu ya kilimo kwanza, bado suala la elimu ni muhimu sana kwa wanawake.

Anasema, kupitia elimu kweli mwanamke hasa yule wa kijijini, anaweza kujitambua na nafasi yake pia, ataweza kuzitumia fursa anazo pewa kikamilifu.

Wanawake wakipata elimu ya kujitambua watakuwa na uelewa mpana wa kukabiliana na changamoto mbalimbali zikiwamo za kudhulumiwa mali zao , lakini watakuwa na fursa ya kufahamu namna bora ya kukabilina na matatizo yanayowakabili.


Mwaka 2006 hadi 2008 janga la chakula lilitokea ambao lilichangia bei ya chakula kimataifa kupanda na watu kukubwa na njaa na kukosa afya bora.

Bei ilianza kupungua na kupanda mwaka 2010 na bado hali inaendelea kuwa mbaya huku wnaoumizwa wakiwa ni watoto na wanawake.

Nchi zinazoendelea ndizo ziliathirika sana , kwani wanawake wa vijijini waliathirika kwa sababu hawakuwezeshwa .

Mazingira ya vijijini yalichangia kuachwa bila msaada kwani, walikuwa hawana mitaji, miundombinu ilikuwa mibovu , watalamu wa kilimo cha kisasa na ufahamu wa mbegu bora.

Kwa kuanzisha programu ambazo zitawasidia wanawake wa vijiji kwa kuwapa mahitaji muhimu, serikali isaidia kupunguza aza za wanawake vijijini.

Mwaka 1984 Rais wa kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Nyerere alisema, wanawake hunyimwa haki zao za msingi katika sekta ya uchumi na kumiliki mali.

Tanzania ina mchanganyiko wa tamaduni ambazo zinachangia maadili katika jamii na imani tofauti lakini nchi yetu haina dini wala ukabila.

Mila na tamaduni zilichangia kwa asilimia kubwa wanawake kunyanyaswa na kumweka katika nafasi ya kukandamizwa.

Hivi sasa nchi imepiga hatua kwa kupunguza unyanyasaji wa jinsia hali inayoonesha mwitikio mkubwa wa kuacha mawazo potofu kuwa mwanamke ni kiumbe dhaifu.

Kuna matukio ya watoto kuolewa mapema nchini , ambapo, mwaka 2004 ripoti ya Umoja wa Mataifa ilieleza kuwa, asilimia 25 ya watoto wenye miaka 15 na 19 waliolewa na luachika, na wengine ni wajane.

Kwa mujibu wa sheria, mwanamke na mwanamume wana haki sawa kwa kila kitu, lakini utamaduni  unawanyanyasa wanawake kwa kuwaona hawawezi kutoa mawazo ambayo yatawasaidia kuleta maendeleo katika jamii.

Unyanyasaji wa kijinsia katika jamii upo wa aina mbalimbali na waathirika wakubwa ni watoto na wanawake ambao hupata misukosuko.
 
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), kimekuwa kikiwakutanisha  wahariri wa vyombo mbalimbali nchini kujadili ukatili wa kijinsia kwa jamii kwa mwaka, 2011 ili kupubguza vitendo hivyo.j

Wapo wanawake waliopata vilema kutokana na unyanyasaji wanaofanyiwa na wengine kupoteza maisha, kutokana na hilo sheria zinazozuia unyanyasaji wa kijinsia na nyingine huku nyingine zikichochea.

Katika katiba kuna vipengele vingi zinavyokataza unyanyasaji wa kijinsia, lakini sio hai hali inayochangiwa na wanawake na  jamii nzima kushindwa kuelewa masuala ya ya sheria .

Ingawa hakuna sheria ya moja kwa moja inayozuia unyanyasaji wa kijinsia, vipengele vilivyokuwamo katika katiba vingefutwa hali hiyo ingepungua na pengine kutoweka.

Ibara  ya 12 ya katiba inazungumzia suala la usawa kwa binadamu wote, lakini imekuwa haifuatwi na hivyo wanawake kujiona ni watu wa chini  kutokana  na changamoto mbalimbali.

Ibara ya 15 inakataza udhalilishaji wa mtu, lakini mimi na wewe leo tunaona mama zetu  wakipigwa na kupoteza maisha hali inasikitisha katika jamii.

Bi. Lucy Mushi mwanaharakati wa masuala ya wanawake anasema, katiba iliyopo ina vipengele vizuri na ingesimamiwa na kutekelezwa, hali ya unyanyasaji ingepungua kwa kasi

Anasema, Ibara ya 14 inaeleza kuwa kila mtu ana haki ya kuishi, lakini tunashuhudia ni wanawake wangapi wanapoteza haki hiyo kutokana na ukatili wa kijinsia?

Pia ibara ya 18 inatoa uhuru wa kila mtu kutoa maoni yake na ibara ya 22 inaeleza haki ya kila mtu kufanya kazi, lakini haya yote yamekuwa hayafanyiki hasa kwa wanawake,” anasema.

Anasema kwenye sheria ya ndoa ya mwaka 1971, kifungu cha 66 kinakataza adhabu ya viboko kwa wanandoa, lakini wapo wanawake wanapigwa kutokana na sababu mbalimbali.

Pia, kuna vifungu  vinavyokataza kuambukiza magonjwa kwa makusudi, kutoroshwa, kutelekeza watoto, ajira ya shuruti, kutishia kuteketeza nyaraka, makosa ya kujamiiana, bughudha za kijinsia lakini havifuatwi.

Anasema, kifungu hicho kinalea unyanyasaji kwa watoto wa kike kuolewa katika umri mdogo, hali inayowafanya wakose haki yao ya msingi ya kupata elimu.

Pamoja na yote hayo, naishauri  serikali kuona haja ya kuwapo kwa sheria inayojitegemea ya kuzuia ukatili majumbani anayoamini itasaidia kupunguza tatizo hilo katika jamii.


Wadau wa wanasema kama mwanamke angekuwa nafasi sawa na wanaume akaweza kuongeza uzalishaji kwa asilimia 20-30 na kuokoa watu milioni 100-150 kutoka katika njaa.
 
Inakadiriwa kuwa, asilimi 60 ya waathirika wa njaa  ni wanawake na vijana. Mashirika ya chakula na kilimo yalibainisha uzalishaji utaongezeka kama kutakuwa na upatikanaji wa pembejeo na mbegu bora.


Imeandaliwa na Hyasinta Timothy kwa msaada wa mashirika

 


 HABARI



Wednesday, March 7, 2012

Polisi

Polisi wamkamata waziri bafuni


 
Na Alfred Lucas - Imechapwa 22 February 2012

POLISI mkoa wa Dar es Salaam, wameingia kwenye kashfa nyingine. Sasa wanatuhumiwa kumkamata Arcado Ntagazwa (66), mwanasiasa mashuhuri nchini akiwa mtupu bafuni, nyumbani kwake Kimara B ‘Temboni.’

Taarifa zinasema askari polisi watano wakiwa na silaha za moto, walimvamia nyumbani kwa Ntagazwa, asubuhi ya Jumatano 8 Februari 2012 na kuvunja mlango wa chumba chake kabla ya kumweka chini ya ulinzi.

Mashuhuda wa tukio hilo wanasema askari polisi wakiongozwa mkuu wa wilaya ya kipolisi ya Mbezi kwa Yusuph, wilayani Kinondoni, OC-CID Gerald, lilivuta mamia ya watu.


Mmoja wa wafanyakazi wa Ntagazwa aliyelazimishwa na polisi kuingia nao ndani alisema, “Polisi wameingia hapa kama wamekuja kukamata jambazi. Huwezi kuamini kama walikuwa wamekuja kumkamata raia, tena ambaye amewahi kuwa waziri mwandamizi serikalini.”


Anasema mara baada ya askari hao kuingia ndani, Ntagazwa alipiga kelele kwa ukali akisema “yaani unaingia ndani kuniangalia nikiwa mtupu tena naoga…

“Yule polisi akasema, nitakutia pingu. Mzee akasema nifunge hiyo pingu kama mimi ni mhaini.”

Baadaye mzee huyo alitoka bafuni na kuvaa nguo zake, lakini aligoma kuondoka nyumbani kwa sharti la kutengenezewa mlango wake.


Mlango huo ulitengenezwa, ndipo mwanasiasa huyo, alipokubali kwenda kituoni kwani alijihakikishia chumba chake kiko salama baada ya kukifunga.


OC-CID Gerald amekiri kumkamata Ntagazwa katika mazingira hayo. Lakini alisema,
“Huyu bwana alikuwa msumbufu.”


“Kwanza kuna siku mbili kabla, aliitwa kituo kikuu Dar es Salaam. Aliitikia wito, lakini baadaye alijiamulia kuondoka chini ya ulinzi. Siku hiyo ya terehe 8 Februari 2012, alifuatwa na askari tangu asubuhi saa 11 alfajiri.


“Mimi kwa cheo changu, huwa nakwenda kumkatama mtu ikibidi. Kuna askari wa kawaida na hata mgambo wanaweza kwenda kumkamata mtu. Sasa siku hiyo alipigiwa simu aamke na kwamba anahitajika kituoni. Hakutoka. Polisi walimweleza kwamba wako nje wanamsubiri hakutoka.


“Tangu saa 11, 12…saa 1 asubuhi mtu hatoki. Basi nikaenda mwenyewe na kumpitia mtendaji wa mtaa hadi nyumbani kwa huyo mzee na kugonga mlango. Hakufungua. Hivyo tukausukuma mlango kwa nguvu na kumkuta ndani.


Mara baada ya kuchukuliwa maelezo hapo kwenye kituo cha Polisi-Mbezi kwa Yusuph, Ntagazwa alipelekwa kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam ambako siku hiyo alilala rumande.


“Tulimkuta anamaliza kupiga simu, kisha akaingia bafuni. Yaani mtu anasema anaoga tangu saa 11 alfajiri. Unajua tumeingia pale ndani kama saa tatu hivi, eti muda wote anaoga. Tukaona hapana. Tukaingia ndani na kumkamata,” ameeleza.

Anasema, “Mimi nasema hata kama tungemkuta anajisaidia, tungemkamata…”

Ntagazwa ambaye alifanyakazi ya uwaziri chini ya utawala wa Mwalimu Nyerere, rais mstaafu Ali Hassani Mwinyi na Benjamin, amethibitisha kukamatwa na polisi.

“Pamoja na kwamba aliniomba radhi kwa vitendo alivyonifanyia, yule kijana aliniomba radhi. Nami nimesamehe. Lakini nimemwambia neno moja, sitasahau,” amesema Ntagazwa kwa sauti ya uchungu.

Ntagazwa ambaye ni mbunge wa zamani wa Kibondo mkoani Kigoma kwa miaka 25 mfululizo (1980-1995), aliyeshika nafasi ya naibu waziri wa fedha kati ya 1983 hadi 1985 na baadaye kuhudumu kwa nafasi tofauti katika serikali za za awamu ya pili na tatu.


Mwaka 2011 alijiunga na Chama cha Demekrsia na Maendeleo (CHADEMA) na kugombea ubunge jimboni Muhambwe.


Akizungumzia hatua hiyo, Ntagazwa anasema, “Sikushtuka kulala ndani…kuna wengi wamelala ndani bila makosa.”


“Kuna watu wanafurahia wengine wadhalilishwe. Hili ni jambo la hatari,” alisema.

Kukamatwa kwa Ntagazwa kunatokana na deni la kuchapa fulana 5,000 walizoagiza kutoka kampuni ya Visual Storm.

Alisema, akiwa mmoja wa wadhamini wa taaisi inayofahamika kwa jina la The Registered Trustees of Social and Political Development’ (AFORD), Ntagazwa anasema wa waliagiza fulana hizo kutoka nchini China kwa ajili ya kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Nyerere, kwa gharama ya sh 74 milioni.


Kazi ya michoro ‘designing’ walimpa Dk. Webhale Ntagazwa ambaye ni kijana wake wa kiume.


“Baada ya Dk. Webhale ku-design. Kazi hiyo ya tulimpa Noel Severe anayemiliki kampuni ya Visual Storm…


“Lakini kabla ya siku ya kumbukumbu ya Nyerere kufika, michoro ya T-shirt zetu za AFORD ilitolewa katika gazeti la Mtanzania likidaiwa kuwa fulana hizo zilikuwa zinahusiana na Chama cha Jamii-CCJ (sasa CCK).


“Tukio hilo lilifanya wafadhili wetu watuite na kusitisha ufadhili wao, hali iliyotufanya tushindwe kuwalipa watengeneza fulana kwa wakati,” anasema.

Akasema walichofanya AFORD ni kutoa taarifa polisi kwa hati RB No.

CD/RB/882/2010 na CD/RB/335/2010 na kwa mkuu wa jeshi hilo , Inspekta Jenerali kupitia barua ya Februari 16, 2010 iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji, Julius Miselya.


Taarifa hiyo ilikuwa ni kulalamika kupotea kwa baadhi ya fulana zetu sambamba na magazeti kuhusika kuvunja udhamini wao, kwa taarifa isiyo ya kweli.


Kwa mujibu wa Ntagazwa, IGP Mwema aliagiza uchunguzi ufanyika chini ya wapelelezi Benett na Ernest, lakini hakuona matunda ya upelelezi wao.


Wakati AFORD wakisubiri kukamilika kwa upepelezi huo kazi hiyo walipewa wapelelezi wengine, Robert na Albogast Kashaija ambao waliwageuka, wakidai walalamikaji, Ntagazwa na Miselya ni matapeli.


Alisema wapelelezi hao walidai kuwa Ntagazwa na Miselya wamejipatia mali kwa njia ya udanganyifu, hivyo wanapaswa kufunguliwa mashtaka mahakamani.


Hata hivyo, Ntagazwa hakupelewa kortini baada ya familia kuingilia kati na kufanya makubaliano ya kulipa fedha inayodaiwa na kampuni ya Visual Storm, ifikapo 27 Machi 2012.


“Kinachoshangazwa ni kwamba ninashtakiwa kama mtu binafsi wakati mimi ni mmoja wa wadhamini wa taasisi yenye uongozi wake.


“Na AFORD, inaweza kushitakiwa kwa kesi ya madai, si jinai kwa sababu kilichofanyika ni kuvunjwa kwa mkataba wa malipo.


“Sitaki kuamini kama kuhama CCM kwenda CHADEMA ndio kiini. Hapa kuna jambo ambalo polisi naona inataka kujidhalilisha kuonyesha taswira mbaya mbele ya jamii,” alisema.


Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam , Suleiman Kova alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema, “Sisi tumekubaliana nao wayamalize na wakishindwa basi sheria itafuata mkondo wake.”


Severe ambaye kampuni yake iliagiza fulana hizo, alisema, “ Kwanza nipo Mbeya kikazi. Haya mambo ni ya kiofisi. Nikija Dar nitakutafuta nikueleze hasa kilichotokea. Siwezi kuyazungumza kwenye simu.

Monday, March 5, 2012

SAKATA LA MAHAU

Balozi Mahalu amlipua JK mahakamani  
Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu
ANIKA ALIVYOSHIRIKI KATIKA MCHAKATO KIPINDI AKIWA WAZIRI MAMBO YA NJE, ASEMA ALIKUTANA NA MAMA MWENYE NYUMBA NA KUAGIZA ALIPWE DOLA MILIONI MOJA HARAKA, AKAMPA OFA KUJA MBUGA YA NGORONGORO
Tausi Ally
ALIYEKUWA Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu ameiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Rais Jakaya Kikwete wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, alifahamu kuwepo kwa rasimu mbili za mikataba ya ununuzi wa jengo la Ubalozi wa Tanzania, Italia.

Profesa Mahalu alisema hayo jana mbele ya Hakimu Mfawidhi, Ilvin  Mgeta wakati akitoa utetezi wake dhidi ya kesi inayomkabili  ya uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya Euro 2,065,827.60 pamoja na aliyekuwa Ofisa Utawala wa ubalozi huo, Grace Martin.

Akiongozwa na wakili wake, Mabere Marando, Profesa Mahalu aliitambua barua ya Februari 20, 2002 ambayo ilikuwa ikieleza kuwa matayarisho yote ya ununuzi wa jengo la ubalozi huko Italia yamekamilika ikiwa ni pamoja na rasimu mbili za mikataba.

Mahalu alidai kuwa katika mchakato wa ununuzi wa jengo hilo wakati yeye akiwa Balozi chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kulikuwa na rasimu mbili za mikataba na kwamba aliwahi kuwasiliana na wizara hiyo juu ya mikataba hiyo.

Alidai kuwa Desemba 2001, Kikwete wakati huo akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alikwenda Rome, Italia kwenye Mkutano wa SADC na alipokuwa huko, ubalozi ulifanya mpango atembelee jengo hilo lililopendekezwa kununuliwa kwa ajili ya ofisi ya ubalozi.

“Wizara ya Mambo ya Nje ya Italia ilifanya mipango yote kwa kumpa utaratibu na usalama Kikwete ambapo alikwenda kutembelea jengo hilo na kukutana na mama mwenye jengo,” alidai Profesa Mahalu.

Alidai kuwa kabla ya mazungumzo na mwenye nyumba, mtoto wa mama huyo, Alberto alimtembeza Kikwete kwenye jengo hilo ndani na nje na baadaye mazungumzo hayo yaliendelea.

Balozi Mahalu alisema baadaye mazungumzo kati ya Kikwete na mama huyo yaliendelea na Alberto alikuwa akitafsiri, kwa sababu mama yake hakufahamu lugha ya Kiingereza.

Profesa Mahalu alidai kuwa katika mazungumzo hayo, Kikwete alimwuliza mama huyo: “Hivi ni kwa nini kunakuwa na mikataba miwili?” na mama huyo alimjibu kuwa hiyo ni kawaida kwa Italia ukitaka kununua jengo kwa bei nafuu.

Profesa Mahalu aliendelea kudai kuwa baada ya kupewa jibu hilo,  Kikwete hakuzungumza tena zaidi ya kucheka na kwamba mwenye jengo alimkumbusha kuhusu malipo ya awali ya dola milioni moja za Marekani ambapo aliafiki na kuahidi kuwa zingelipwa kabla ya mwisho wa mwaka 2001.
Profesa Mahalu alidai pia kwamba Kikwete alimweleza mama huyo kuwa atalishughulikia suala hilo baada ya kurejea Dar es Salaam na kumshukuru kwa kuwauzia jengo zuri.

Baada ya kutoa maelezo hayo, Profesa Mahalu alidai kuwa baada ya Kikwete kusema maneno hayo, alimgeukia na kumwambia: “Costa ni vizuri tupate hela tumlipe huyu mama watu wengine wasije wakachukua hili jengo.”

Profesa Mahalu alidai kuwa baada ya Kikwete kumshukuru mama huyo kwa ukarimu wake, alimkaribisha Tanzania awe mgeni wa Wizara ya Mambo ya Nje yeye na mumewe na kwamba watampeleka Ngorongoro.

“Tulipokuwa njiani tukirudi hotelini alipofikia Kikwete akiwa kwenye gari alimpigia simu Kibero akimuagiza afanye utaratibu wa kulipa Dola milioni moja kama malipo ya awali ya jengo hilo,” alidai Profesa Mahalu.

Alidai kuwa baadaye alimwagiza (Profesa Mahalu) aje Dar es Salaam kufuatilia mpango huo wa malipo ya awali ya ununuzi wa jengo hilo.

Awali, Profesa Mahalu akiongozwa na Wakili Alex Mgongolwa alidai kuwa anaitambua ripoti ya uthamini wa jengo hilo la ubalozi nchini Italia uliofanywa na Kimweri kutoka Wizara ya Ujenzi  aliyekwenda Rome Julai 15 hadi 26, 2001 kwamba jengo lilikuwa na gharama ya Sh6 bilioni.

Pia alizitambua ripoti za uthamini wa jengo hilo ambazo ni ile ya mama mwenye nyumba ambayo ilionyesha kuwa jengo hilo lilikuwa na thamani Sh5.500 bilioni na ripoti ya uthamini iliyofanywa na Serikali ya Italia iliyoonyesha kuwa jengo lilikuwa na thamani ya Sh11.117 bilioni.

Hakimu Mgeta aliiahirisha kesi hiyo hadi leo itakapoendelea kwa utetezi.

Dk. Mwakyembe India: Mabingwa wafichua ‘kemikali’ hatari

Tiba ya Dk. Mwakyembe India: Mabingwa wafichua ‘kemikali’ hatari



Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe


  • Zimekuwa zikijizalisha maalumu kushambulia ngozi
WAKATI bado kukiwa na hali ya kutothibitishwa kitabibu Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ameathirika kiafya kwa kupewa sumu au la, taarifa za awali zinabainisha kuwapo kwa ‘kitu’ kwenye ute ute (bone marrow) ndani ya mifupa yake, chenye uwezo wa kuzalisha kemikali zinazoshambulia chembe hai za ngozi, Raia Mwema, limeelezwa.


Kwa mujibu wa habari za uhakika zilizotufikia kutoka vyanzo mbalimbali vya habari hospitalini Apollo, India, awali alipofikishwa nchini humo, jopo la madaktari bingwa walifanya uchunguzi na kubaini ‘kitu’ hicho kwenye ute ute ndani ya mifupa yake.

Hata hivyo, taarifa hizo zinabainisha kuwa baada ya kufanya utafiti wa kina, madaktari hao ambao miongoni mwao ni mabingwa wa kutafiti kemikali, walifanikiwa kubuni chembe nyingine za kudhibiti kemikali (kitu) zilizobainika ndani ya ute ute huo.


“Katika hali ya kushangaza, baada ya kubaini kuwapo kwa kemikali ndani ya ute ute wake na jopo la maprofesa ambao ni madaktari bingwa kufanikiwa kubuni namna ya kudhibiti hicho kilichogundulika, walishtushwa kemikali hizo kuwa na uwezo wa kuendelea kujizalisha na kuendelea kushambulia ngozi yake,” kinaeleza chanzo chetu cha habari kutoka hospitalini Apollo, nchini India ambako Dk. Mwakyembe alikwenda kutibiwa kwa mara ya kwanza.


“Kwa hiyo, walianza kazi ya kupambana na kemikali hizo zisiweze kuendelea kujizalisha na walipoona dalili za kufanikiwa walimruhusu kurejea Dar es Salaam, lakini wamechukua kemikali hizo kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Sasa ni majopo ya kitabibu yanayokusanya maprofesa kadhaa ndiyo wanaoendelea na uchunguzi wa kina kubaini ni kemikali za aina gani, zimeingizwa vipi mwilini mwake.”


“Na sasa amekuja hapa India kwa ajili pia ya kuangaliwa maendeleo yake. je, kemikali zile zimefanikiwa kuangamizwa kama bado zimepungua kwa kiasi gani au bado zina uwezo wa kuendelea kujizalisha kama ilivyokuwa awali? Kwa hiyo, uchunguzi bado haujakamilika,” kinaeleza chanzo hicho chetu cha habari kutoka Apollo.


Kwa upande mwingine, mara baada ya kurejea kutoka India kwa mara ya kwanza alikokwenda kutibiwa, mwandishi wa gazeti hili alifanikiwa kuona baadhi ya picha za hali ya Dk. Mwakyembe na namna ngozi yake ilivyokuwa imeathirika, mwili ukiwa umevimba na ngozi kuchanika na kuwa kavu na ngumu na yenye magamba mithili ya ngozi ya mamba.


Ni wakati huo ambao, Dk. Mwakyembe mwenyewe alipata kumdokeza mwandishi wetu kwamba; “Hali ilikuwa mbaya sana alipokuwa India kwa matibabu kwa mara ya kwanza.”


Lakini kwa upande mwingine, wataalamu wengine wa kemia na baiolojia nchini kwa nyakati tofauti bila kutaka majina yao yaandikwe gazeti kutokana na namna suala la Dk. Mwakyembe linavyozungumziwa na viongozi wa taasisi nyeti nchini, wameelezea uwezekano wa kurutubishwa kwa kemikali za namna hiyo ili kushambulia baadhi ya chembe hai katika mwili wa binadamu na hatimaye kusababisha kifo cha mhusika na baadaye, kifo hicho kuaminika kimetokana na ugonjwa fulani.


Katika hatua nyingine, taarifa za “internet” zinabainisha kuwa kemikali za namna hiyo huweza kutengenezwa na wakemia sambamba na wanabaiolojia kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwadhuru watu mashuhuri kwa malengo mbalimbali.


Kazi za ute-ute (bone marrow) mwilini

Kazi kubwa ya ute uliopo ndani ya mfupa wa mwanadamu (bone marrow) ambao humo ndimo inaelezwa kuwa kemikali zinazomdhuru Dk. Mwakyembe zilipo, ni kuzalisha aina tofauti za chembe hai za damu ambazo ni muhimu kwa afya ya mwanadamu kwa ujumla.

Kuna aina mbili za ute huo katika mifupa ya mwanadamu ambazo ni kwanza; ute wa njano (yellow bone marrow) ambao umesheheni kiwango kikubwa cha chembe hai zenye mafuta (fat cells).


Lakini aina ya pili ni ute mwekundu (red bone marrow) ambao hujumuisha chembe nyingine hai muhimu katika uzalishaji wa chembe damu mpya (new blood cells).


Kazi ya chembe damu na ute-ute

Ute mwekundu ndani ya mfupa (red bone marrow) na hasa katika mifupa mikubwa wajibu au kazi yake ya msingi ni uzalishaji wa shehena ya chembe damu hai mpya.

Ute ute huo unatajwa kujihifadhi katika mifupa ya mwanadamu hususan katika maeneo matano ya aina ya mifupa.


Mifupa hiyo ni; mosi, mifupa ya mkono (arm bones), pili; mifupa ya kifuani (breastbone); tatu, mifupa ya miguu (leg bones); nne, mifupa ya mbavu (ribs) na tano, uti wa mgongo (spine)


Kwa upande wa Dk. Mwakyembe, picha za mionzo zilizopata kuonwa na mmoja wa watu wake wa karibuni akiwa katika matibabu India zinadaiwa kuonyesha mifupa iliyoanza kuathiriwa kwa kuwa na alama za awali tofauti na mingine ni ya mifupa ya mikono kuelekea mifupa ya kifuani, na kwa hiyo, kama ni kitu (sumu?) kilichokuwapo kwenye ute wa mifupa yake basi kiliingia ,inawezekana kupitia viganja vya mikono yake na kupenya kwenye ute ndani ya mifupa ya mikono.


Dk. Mwakyembe na DCI Manumba

Kama vile mtu ambaye amekerwa na namna Jeshi la Polisi, kupitia kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, Dk. Mwakyembe Februari 18, wiki iliyopita, alitoa taarifa kwa vyombo vya habari kujibu kile kilichoelezwa na Manumba kuhusu afya yake.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, DCI alieleza bayana kwamba Dk. Mwakyembe hajalishwa sumu na kwamba kinachomsumbua ni ugonjwa wa ngozi tu, maelezo ambayo yamepingwa na Dk. Mwakyembe mwenyewe akisema kinachomsumbua bado hakijawekwa bayana na jopo la madaktari bingwa wanaomtibu India.


Taarifa hiyo ya Mwakyembe ilieleza : “Napenda nisisitize mapema kabisa kuwa msimamo huo wa Jeshi la Polisi umenikera sana katika hali niliyonayo ya ugonjwa, kwanza kwa kuingilia mchakato wa matibabu yangu na uchunguzi wa kina kuhusu kiini chake unaoendelea hospitali ya Apollo nchini India ambako bado sijahitimisha matibabu yangu; pili kwa ufinyu wa uelewa unaojitokeza bayana kwenye tamko la Jeshi la Polisi unaosisitiza kuwa “sikunyweshwa sumu” wakati sumu si lazima unyweshwe ili ikudhuru, inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa tu; na tatu kwa Jeshi la Polisi kujiingiza kwenye suala ambalo kwa takriban mwaka mzima halijawahi kuwa na dhamira ya dhati ya kulielewa au kulichunguza mbali na kulifanyia mzaha kupitia magazetini.


“Itakumbukwa kuwa tarehe 9 Februari, 2011 nilimwandikia barua IGP Said Mwema kumtaarifu kuhusu njama za kuondoa maisha yangu na ya viongozi wengine. Kwa kutambua kuwa Jeshi la Polisi la Tanzania daima husisitiza kuletewa ushahidi kwanza ndipo lifanyekazi, nilihakikisha nimeainisha katika barua hiyo kila ushahidi nilioupata au kupewa. (Utaratibu huu wa Jeshi la Polisi kusubiri kuletewa ushahidi mezani, kama ambavyo mahakimu wanavyosubiri ushahidi mahakamani, haupo popote pale duniani (ila Tanzania tu) kwani kazi ya msingi ya Polisi si kuletewa, ni kutafuta ushahidi. Polisi wanachohitaji duniani kote ni kupata clue au tetesi tu. Hiyo inatosha kufukua ushahidi wote unaohitajika).

Pamoja na kujitahidi kuanika kila aina ya ushahidi niliokuwa nao, mambo manne yalijitokeza ambayo yalionyesha wazi kuwa Polisi hawakuwa na dhamira ya dhati ya kupeleleza suala hilo:


  1. Siku chache baada ya kumkabidhi IGP barua hiyo, nilitumiwa timu ya “wapelelezi” ofisini kwangu kuja kuchukua maelezo yangu ya ziada. Timu hiyo ilikuwa inaongozwa na ACP Mkumbo, afisa wa polisi ambaye wiki chache zilizokuwa zimepita alikuwa miongoni mwa askari waliotuhumiwa kupokea rushwa kwa lengo la kumbambikizia madawa ya kulevya mtoto wa Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi, suala ambalo mpaka leo hii uongozi wa Polisi umeshindwa kulitolea maelezo ya kuridhisha. Kwa msingi huo, nilikuwa nimeletewa mtuhumiwa wa rushwa/ ujambazi kuendesha uchunguzi wa watuhumiwa wengine wa ujambazi! Nikatambua mara moja kuwa zoezi zima lilikuwa la mzaha, tena mzaha mkubwa!
  2. Wiki chache baada ya barua yangu kuwasilishwa kwa IGP na timu ya ACP Mkumbo “kuanza kazi”, Jeshi la Polisi likachukua hatua ya kuwapongeza na kuwazawadia askari niliowatuhumu kushirikiana na majambazi! Huhitaji kuwa profesa wa falsafa kuelewa kuwa huo ulikuwa ujumbe tosha wa kunipuuza.
  3. Hivi karibuni tuhuma za askari polisi kujihusisha na vitendo vya ujambazi mkoani Morogoro zilipopamba moto na kuwagusa askari “wale wale” niliowatuhumu kwenye barua yangu, IGP alichukua hatua ya kuwahamishia mikoa mingine!
  4. Ili kunikatisha tamaa kabisa, barua yangu ya “siri” kwa IGP ikavujishwa kwa makusudi kwenye vyombo vya habari na kuchapishwa kama habari ambayo ilikebehi na kukanusha taarifa nzima niliyotoa, sijui kwa faida ya nani! Lakini huu ni mchezo wa kawaida kwa polisi kwani hivi karibuni Mhe. Waziri Samuel Sitta alipohojiwa na ofisa mwandamizi wa Jeshi la Polisi ofisini kwake, wakiwa wawili tu, taarifa ya kikao hicho ikawa kwenye moja ya magazeti ya mafisadi ikikebehi ushahidi aliotoa Sitta! The integrity of the police force leadership is on the line.



Nimeelezea vizuri katika barua yangu kwa IGP kuwa kundi hilo la mauaji lilikuwa limeelekezwa kuniua kwa kutumia sumu, taarifa ambayo kwa karibu mwaka mzima Polisi hawakutaka kuifuatilia kwa sababu wanazozijua wenyewe. Sasa huu msukumo mpya wa Jeshi la Polisi kutaka kujua kama nilipewa sumu au la na kukurupuka kutoa tamko hata kabla ya kunichunguza nilivyo, kunihoji mimi na wasaidizi wangu ofisini na hata kuongea na mabingwa wa Kihindi wanaonifanyia uchunguzi, umetokea wapi? Si ni polisi hawahawa ambao, badala ya kushukuru, wamekuwa wakikerwa na tahadhari ambazo Waziri Sitta amekuwa akitoa ili suala hili lichunguzwe kwa kina?


Aidha napata taabu kuamini kama DCI Manumba na wenzake waliisoma taarifa halisi ya matibabu yangu au walisoma taarifa “nyingine”, na kama waliisoma taarifa hiyo wenyewe au “walisomewa”! Nasema hivyo kwa kuwa alichokisema DCI Manumba kwa wandishi wa habari hakifanani kabisa na picha iliyo kwenye taarifa halisi ya Apollo ambayo inatamka wazi kuwa kuna kitu kwenye bone marrow kinachochochea hali niliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaikia kukijua, kukidhibiti/kukiondoa huku vyombo vyetu vya dola vikipelekeshwa na mafisadi kusema bila msingi wa kisayansi wala aibu: “hakulishwa sumu”, “hakulishwa sumu”!


Nimesoma darasa moja Kitivo cha Sheria Mlimani na DCI Manumba. Baadaye IGP Mwema alikuwa mwanafunzi wangu wa sheria Mlimani. Vigogo hawa wawili wa usalama wa raia nchini hawajanitendea haki, nao wanajua. Wanajua vilevile kuwa sitakaa kimya au kumung’unya maneno come what may pale ambapo haki inakanyagwa.


Tuendelee kuombeana afya na uhai ili tutendeane haki na vilevile tuitendee nchi yetu haki kwa kuvimalizia viporo vinavyokera vya Dowans, EPA, Kagoda n.k. kwa maslahi mapana ya Taifa letu.


CHANZO: Raia Mwema
 

SAKATA LA MADAKTARI KUGOMA TENA

Madaktari kugoma Jumatano tena

  Wasema utakuwa mgomo wa kihistoria
  Washikilia madai yao hayajatekelezwa
  Wasisitiza Dk. Mponda, Nkya waondolewe



Madaktari wakiwa wameshikana mikono kuashiria mshikamano kwa kauli moja ya kuanza mgomo siku ya Jumatano ijayo wakati walipotoa tamko lao katika mkutano wa uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Madaktari wametangaza kuanza mgomo mwingine Jumatano ijayo baada ya Serikali kushindwa kuwatekelezea mahitaji yao kama walivyokubaliana katika kikao chao kilichopita.
Kati ya mahitaji yao ni kuitaka Serikali kuwaondoa madarakani Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda na Naibu wake Dk. Lucy Nkya.
Katika kikao chao cha jana wameridhia kwa pamoja kuwa endapo Serikali haitachukua hatua dhidi ya suala hilo watafanya mgomo mkubwa wa aina yake kihistoria Jumatano (Machi 7) ili madai yao yaweze kutekelezeka.
Akitangaza tamko hilo jana jijini Dar es Salaam katika mkutano wao wakiwemo madaktari wa mikoani, Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari nchini (MAT), Dk. Godbless Charles, alisema kuwa suala hilo limeridhiwa na madaktari wote.
Alisema viongozi hao wamekuwa ni kikwazo katika utekelezaji wa madai yao na kwamba wamekuwa wakichangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa mgomo huo.
Alisema kwa sasa wanaipa muda Serikali kufanyia maamuzi suala hilo na endapo itakaa kimya hadi Jumatano ijayo, wataweka vifaa vyao chini na kugoma kufanyakazi mpaka hapo kitakapoeleweka.
Dk. Charles alisema kuwa juzi walikutana na kamati iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza madai yao kwa ajili ya majadiliano ya utekelezaji wake.
Alisema walivyokutana na kamati hiyo walijua wanajadili moja kwa moja kuhusiana na madai yao ambapo waliwaambia kwamba mpaka kufikia hatua ya makubaliano ni lazima masuala matatu muhimu yafuatwe.
Waliyataja masuala hayo kuwa ni kuandaa mazingira ya utekelezaji wa hayo watakayoafikiana, kujadili madai ya madaktari pamoja na kutiliana sahihi makubaliano hayo.
Hata hivyo, Dk Charles alisema utekelezaji wa suala la pili na la tatu unakwenda sambamba na suala la kwanza ambapo linataka kuondolewa kwa viongozi hao wawili ndipo utekelezaji wa mengine ufuatwe.
Alisema madaktari hawana imani na viongozi hao kwa kuwa hawataweza kujadili mambo ya chini kwa kuwa ya juu hayajatekelezwa.
Madaktari hao walidai kuwa awali walipendekeza viongozi wa wizara hiyo kuwajibishwa lakini matokeo yake Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aliwawajibisha, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Blandina Nyoni na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Deo Mtasiwa, huku wahusika wengine wakiachwa.
Aidha, walisema Pinda aliwajulisha kuwa yeye hawezi kumwajibisha Dk. Mponda na Dk. Nkya kwa kuwa wameteuliwa na Rais.
Madaktari hao walisema kuwa mpaka sasa hawajajulishwa ni hatua gani zitachukuliwa dhidi ya viongozi hao ambao wamedai kuwa wamechangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa vifo vya wagonjwa.
Walisema kuwa wameshangazwa na kauli ya Dk. Mponda kueleza kuwa mpaka ajisikie kujiuzulu ndipo atafanya hivyo wakati yeye na wenzake wamesababisha madhara hayo kutokea.
Aidha, walisema pamoja na Rais Kikwete kutangaza kumaliza tatizo lao na kusisitiza kutokuwepo kwa mgomo huo bado wanapinga vikali jambo hilo na kueleza kuwa mgomo huo utakaoanza utakuwa ni mkubwa na wa kihistoria nchini.
"Tuliambiwa Rais hayupo, tunashindwa kuelewa mpaka sasa bado hajarudi na je ni hatua gani inachukuliwa hatuwezi kwenda mbele kujadili kabla hilo halijatekelezwa," alisema.
Aidha Dk. Charles alisema kuwa Serikali imeona kuwa madai yao makubwa ni nyongeza ya mshahara bila kuwaboreshea mazingira ya kazi kwani wanafanya kazi katika mazingira magumu.
"Hivyo vijisenti vyao hata wakituongezea tunaweza kuvikataa sasa watatuongezeaje fedha bila kutuboreshea mazingira ya kazi mgonjwa anakuja hakuna vifaa matokeo yake anafariki tumechoka kuona wagonjwa wakitufia kwa kukosa dawa ifike wakati taaluma yetu iheshimike kwani sisi sio wanasiasa," alisema.
Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya madaktari, Dk Steven Ulimboka, alisema kuwa lengo la mgomo huo ni kuishinikiza Serikali kuwapatia madai yao ya msingi ambayo waliahidiwa kufanyiwa kazi.
Alisema hiyo siku ya mgomo hawana haja ya kuendelea kufanya mkutano kila mmoja atatakiwa kufanya mambo yake mengine baada ya vifaa vyao kuwekwa chini.
Alisema kwa sasa wanakwenda hatua kwa hatua na mgomo wa sasa utakuwa mkubwa kuliko wa awali mpaka hapo madai yao yatakapotekelezwa.
Alisema umma unatakiwa kuelewa kuwa Serikali ndio inawasababishia madhara kuwepo pale wanapofanya mgomo na kwamba taaluma yao imekuwa ikidharauliwa badala ya kuheshimika.
Alisema wameshindwa kuelewa ni kwanini kamati hiyo imewacheleweshea kuwapatia majibu licha ya kwamba waliwaongezea muda wa wiki mbili ili waletewe taarifa kuhusiana na utekelezaji wa madai yao kama walivyoagizwa na Waziri Mkuu.
Wakati wakiwa kwenye kikao hicho, mmoja wa madkatari hao, alimtaka Rais wa MAT, Dk. Namala Mkopi , kuwasiliana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia, kuwajulisha kama kuna hatua zozote zilifikiwa kuhusu suala lao la kuondolewa kwa viongozi hao ili waweze kuendelea kujadili masuala mengine muhimu.
Hata hivyo, Dk. Mkopi alisema alifanikiwa kuongea na Ghasia na kumjibu kuwa hafahamu lolote kuhusiana na suala la viongozi hao na kwamba kuwajibishwa kwao kuko nje ya uwezo wake.
Aliongeza kuwa Ghasia alimwambia kwa wakati huo (jana) alikuwa ameanza likizo.
Hivi karibuni madaktari walifanya mgomo kwa nia ya kuishinikiza Serikali iwapatie madai yao ikiwemo nyongeza ya posho, posho ya mazingira hatarishi, posho ya muda wa ziada pindi wanapokuwa kazini, kupatiwa nyumba, usafiri pamoja na kadi ya bima.
Madaktari hao waliwasilisha madai nane kwa Pinda ambapo aliahidi kuyashughulikia katika kikao chao kilichopita na kuwajulisha kuwa ameunda kamati ya watu tisa kwa ajili ya kushughulikia madai yao.