Wednesday, March 28, 2012

WAUZA CHIPSI IRINGA WADAIWA KUCHANGANYA MAFUTA YA KULA NA YA TRANSFOMA ZA UMEME




KUMEKUWA  na tabia ya baadhi ya wauza chipsi katika maispaa ya Iringa kuchanganya mafuta ya transfoma katika mafuta ya kukaangia chipsi jambo ambalo  ni hatari kwa afya ya binadamu..

Wakizugumzia suala hilo wauzaji wa chips katika maispaa ya Iringa wamesema kuwa ni kweli suala hilo lipo, kwa baadhi ya wengi wao wamekuwa wakifanya hivyo kutokana na kutafuta faida kubwa kwani mafuta hayo yakichanganywa hayaishi haraka.

Wafanyabiashara hao wameeleza jinsi chipsi hizo zinavyokuwa baada ya kuchanganywa mafuta hayo ya kawaida na transfoma kuwa chipsi hizo huwa nyeusi na pia hupoteza radha.

Hata hivyo wamewashauri wezao wanaofanya jambo hilo kuacha mara moja kwani madhara watakayoyapata walaji ni makubwa kutokana na mafuta hayo kuwa na kemikali. na madhara hayo ni kama vile kansa ya tumbo na kupata ugonjwa wa ngozi
Aidha kwa upande wake afisa afya manispaa ya iringa DEODATA LUKUPWA amesema kuwa hajawahi kupata malalamiko kama hayo ila ametoa agizo kwa wafanyabiashara hao wa chipsi ambao wanafanya hivyo kuacha mara moja ili kuokoa afya za walaji.