ASHA ROZE MIGIRO |
ANNA MAKINDA |
TIBAIJUKA |
MAMA SALMA KIKWETE |
Historia ya Siku ya Wanawake Duniani
SIKU ya Wanawake Duniani ni sherehe katika nchi nyingi duniani. Ni siku ambayo wanawake hutambuliwa kwa ajili ya mafanikio yao bila kujali mgawanyiko wa Taifa, kabila, lugha, kitamaduni, kiuchumi au kisiasa.
Ni tukio ambalo hukumbusha jitihada za nyuma na mafanikio, na muhimu zaidi, kwa ajili ya kuangalia mbele kwa uwezo wa wanawake waliopita kwa kizazi kijacho.
Umoja wa Kimataifa ulianza kusherekea siku hii Machi 8 mwaka 1975, na miaka miwili baadaye, Desemba 1977, Baraza Kuu la UN lilipitisha na kutangaza Siku ya Haki za Wanawake na Amani ya Kimataifa kuadhimishwa siku yoyote ya mwaka kwa kabila la ‘medlemsstater’.
Kwa mujibu wa mila yao, walipitisha azimio la Baraza Kuu lililotambua jukumu la wanawake katika juhudi za amani na maendeleo, wito wa mwisho kwa ubaguzi na ongezeko la msaada kwa ajili ya ushiriki wa wanawake.
Siku ya Wanawake kwa mara ya kwanza iliibuka katika shughuli za harakati za kazi, karne ya ishirini, Amerika Kaskazini na Ulaya.
Mwaka 1909, wanawake walifanya mgomo kupitia chama cha kisosholisti kupinga mazingira magumu ya kazi.
Mwaka 1910, ilikuwa siku ya kimataifa ya kijamaa ambapo ulifanyika mkutano maalumu wa Copenhagen, kwa ajili kudai haki ya kupiga kura, kwa heshima ya harakati na haki za wanawake pia, kujenga msaada kwa ajili ya kufanikisha haki ya kupiga kura kwa wote.
Mkutano huo uliudhuriwa na zaidi ya wanawake 100 kutoka nchi 17 duniani pamoja na kuchagua wanawake wawakilishi wa madai yao ambapo hawakuweka saini ya siku maalumu maadhimisho ya siku hiyo.
Mwaka, 1911 matokeo ya mkutano wa Copenhagen yalitangaza Siku ya Wanawake Duniani mara ya kwanza Machi 19 katika nchi za Austria, Denmark, Ujerumani na Uswisi, ambako zaidi ya wanawake milioni moja na wanaume walihudhuria mikutano ya kampeni za uchaguzi.
Mbali na haki ya kupiga kura na kushikilia ofisi ya umma, wanaume walidai haki za kazi kuwa sawa na za wanawake, mafunzo ya ufundi na ya mwisho ya ubaguzi kwa kazi.
Mwaka 1913 na 1914, ni kumbukumbu muhimu kwa Siku ya Kimataifa ya Wanawake kupinga Vita ya kwanza ya dunia, kama sehemu ya harakati za amani.
Nchini Urusi husherekea siku hiyo kila jumapili ya kwanza ya mwezi februari, Ulaya mwaka uliofuata Machi 8 kwa lengo la kuanzisha kampeni maalumu ya kupinga vita na kuonyesha mshikamano na wanaharakati wengine.
Mwaka 1917 ilikuwa siku maalumu nchini Urusi kwa wanawake kupinga kuongezeka kwa vita, iliyojulikana kwa jina la ‘mikate na amani' iliyofanyika siku ya Jumapili februari (ambayo ilikuwa ni tarehe 8 Machi kwenye kalenda ya Gregorian).
Siku nne baadaye, serikali ilianza kutoa nafasi kwa wanawake kuanza kupiga kura.
Tangu mwaka huo, Siku ya Wanawake Duniani imekuwa na mwelekeo mpya wa kimataifa kwa ajili ya wanawake katika nchi zinazoendelea na zilizoendelea.
Idadi ya wanawake wanaharakati imekuwa ikiongezeka na kuwa nguvu na mikutano ya nne ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa ya wanawake.
Wanaharakati wamesaidia kufanya maadhimisho kila hatua kwa kutegemea kujenga msaada kwa ajili ya haki za wanawake na kushiriki katika masuala ya kisiasa na kiuchumi.
Siku ya Wanawake Duniani ni wakati wa kutafakari juu ya mafanikio yaliyopatikana, kuwaita kwa ajili ya mabadiliko na kusherehekea vitendo vya hamasa na ujasiri katika shughuli za kila siku.
Umoja wa Mataifa na usawa wa jinsia
Mkataba wa Umoja wa Mataifa, uliosainiwa mwaka 1945, ulithibitisha kanuni ya usawa kati ya wanawake na wanaume.
Tangu wakati huo, UN ilisaidia kujenga urithi wa kihistoria wa kimataifa kukubali mikakati na viwango vya mipango na malengo ya kuendeleza hali ya wanawake duniani.
Umoja wa Mataifa na mashirika yake imekuza ushiriki wa wanawake kama washirika sawa na wanaume katika kuleta maendeleo endelevu, amani, usalama, na heshima kwa ajili ya haki za binadamu.
Pia, imewawezesha kuendelea kuwa kipengele kati ya juhudi za Umoja wa Mataifa kushughulikia changamoto za kijamii, kiuchumi na kisiasa duniani kote.
Kila siku ni Siku ya Mwanamke Duniani, Ban Ki-moon
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon anasema, "kila siku ni Siku ya Wanawake duniani, kwani mwanamke ni kigezo kikubwa kuongeza pato la taifa na kukuza uchumi wa dunia basi kwa misingi hiyo kila siku muhimu kwakwe.
"Mfano mwanamke wa kijijini ana nafasi kubwa ya kuleta maendeleo kijijini kwake na katika taifa kwa njia ya kilimo,".
Mwanamke akipatiwa mahitaji yote muhimu kama miundo mbinu, zana bora za kilimo na muongozo basi anaweza kufanya mabadiliko ya uchumi kuanzia ngazi ya chini mpaka juu.
Hata hivyo sera na mipango iliyowekwa na serikali iweze kweli kumnufaisha mwanamke, ikiwamo mpango mkakati wa kilimo .
Hivi karibuni mawaziri wanaohusika na masuala ya maendeleo ya wanawake kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, walikutana kujadili masuala hayo ambapo, walikubadilishana mawazo kuhusu hali ya wanawake wa vijijini.
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Un, Dkt.Asha Roze Migiro anasema, "Ukweli ni kwamba wanawake wa vijijini wanaendelea kukabiliwa na vikwazo vingi vikiwamo ya upatikanaji wa ardhí, pembejeo za kilimo, mitaji, huduma za kijamii na teknolojia za kisasa”
Kauli mbiu ya mkutano huo ilikuwa, "Nafasi ya wanawake wa Vijijini na Mchango wao katika Kupambana na Umaskini na Njaa,".
Lengo la pili ni namna gani wanaweza kuwezeshwa ili wapate nguvu ya kuwa kichocheo cha maendeleo endelevu.
Kauli mbiu ya kimataifa siku ya wanawake duniani 2012 ni "Uwezeshaji wa wanawake wa kijijini utasaidia kumaliza njaa na umaskini," Nchini, "Ushiriki wa mtoto wa kike ni chachu ya maendeleo".
Kama wanawake wa vijijini wangepewa fursa sawa ya kupewa nyenzo za uzalishaji, basi uzalishaji wa mazao ya kilimo ungeongezeka kwa asilimia kubwa na kiwango cha njaa kingepingua.
Bado mwanamke huchukuliwa kama msaada mkubwa wa kupunguza njaa katika mataifa mbalimbali japokuwa mchango wake hautambuliwi.
Anasema, bado wanawake wa vijijini wanaendelea kukabiliwa na ugumu katika upatikanaji wa huduma za msingi zikiwano za ulinzi wa jamii, ajira na masoko ya uhakika.
Dkt.Migiro anasema, taifa liweke mikakati itakayowawezesha wanawake wa maeneo ya vijijini kuongeza uwezo wao kupambana na umaskini uliokithiri, njaa na kujiletea maendeleo endelevu katika familia zao.
Anasema, ili hayo yaweza kufanikiwa ni lazima jamii itambue kwamba wanawake ni mawakala muhimu wa mabadiliko.
Pia, wakisaidiwa katika jumuiya zao kutasaidia katika kuhakikisha kwamba, matakwa na vipaumbele vya wanawake wa vijijini yanapewa umuhimu unaostahili.
Anasema, ili sera, na mipango iliyowekwa na serikali iweze kweli kumnufaisha mwanamke, ikiwamo kaulimbiu ya kilimo kwanza, bado suala la elimu ni muhimu sana kwa wanawake.
Anasema, kupitia elimu kweli mwanamke hasa yule wa kijijini, anaweza kujitambua na nafasi yake pia, ataweza kuzitumia fursa anazo pewa kikamilifu.
Wanawake wakipata elimu ya kujitambua watakuwa na uelewa mpana wa kukabiliana na changamoto mbalimbali zikiwamo za kudhulumiwa mali zao , lakini watakuwa na fursa ya kufahamu namna bora ya kukabilina na matatizo yanayowakabili.
Mwaka 2006 hadi 2008 janga la chakula lilitokea ambao lilichangia bei ya chakula kimataifa kupanda na watu kukubwa na njaa na kukosa afya bora.
Bei ilianza kupungua na kupanda mwaka 2010 na bado hali inaendelea kuwa mbaya huku wnaoumizwa wakiwa ni watoto na wanawake.
Nchi zinazoendelea ndizo ziliathirika sana , kwani wanawake wa vijijini waliathirika kwa sababu hawakuwezeshwa .
Mazingira ya vijijini yalichangia kuachwa bila msaada kwani, walikuwa hawana mitaji, miundombinu ilikuwa mibovu , watalamu wa kilimo cha kisasa na ufahamu wa mbegu bora.
Kwa kuanzisha programu ambazo zitawasidia wanawake wa vijiji kwa kuwapa mahitaji muhimu, serikali isaidia kupunguza aza za wanawake vijijini.
Mwaka 1984 Rais wa kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Nyerere alisema, wanawake hunyimwa haki zao za msingi katika sekta ya uchumi na kumiliki mali.
Tanzania ina mchanganyiko wa tamaduni ambazo zinachangia maadili katika jamii na imani tofauti lakini nchi yetu haina dini wala ukabila.
Mila na tamaduni zilichangia kwa asilimia kubwa wanawake kunyanyaswa na kumweka katika nafasi ya kukandamizwa.
Hivi sasa nchi imepiga hatua kwa kupunguza unyanyasaji wa jinsia hali inayoonesha mwitikio mkubwa wa kuacha mawazo potofu kuwa mwanamke ni kiumbe dhaifu.
Kuna matukio ya watoto kuolewa mapema nchini , ambapo, mwaka 2004 ripoti ya Umoja wa Mataifa ilieleza kuwa, asilimia 25 ya watoto wenye miaka 15 na 19 waliolewa na luachika, na wengine ni wajane.
Kwa mujibu wa sheria, mwanamke na mwanamume wana haki sawa kwa kila kitu, lakini utamaduni unawanyanyasa wanawake kwa kuwaona hawawezi kutoa mawazo ambayo yatawasaidia kuleta maendeleo katika jamii.
Unyanyasaji wa kijinsia katika jamii upo wa aina mbalimbali na waathirika wakubwa ni watoto na wanawake ambao hupata misukosuko.
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), kimekuwa kikiwakutanisha wahariri wa vyombo mbalimbali nchini kujadili ukatili wa kijinsia kwa jamii kwa mwaka, 2011 ili kupubguza vitendo hivyo.j
Wapo wanawake waliopata vilema kutokana na unyanyasaji wanaofanyiwa na wengine kupoteza maisha, kutokana na hilo sheria zinazozuia unyanyasaji wa kijinsia na nyingine huku nyingine zikichochea.
Katika katiba kuna vipengele vingi zinavyokataza unyanyasaji wa kijinsia, lakini sio hai hali inayochangiwa na wanawake na jamii nzima kushindwa kuelewa masuala ya ya sheria .
Ingawa hakuna sheria ya moja kwa moja inayozuia unyanyasaji wa kijinsia, vipengele vilivyokuwamo katika katiba vingefutwa hali hiyo ingepungua na pengine kutoweka.
Ibara ya 12 ya katiba inazungumzia suala la usawa kwa binadamu wote, lakini imekuwa haifuatwi na hivyo wanawake kujiona ni watu wa chini kutokana na changamoto mbalimbali.
Ibara ya 15 inakataza udhalilishaji wa mtu, lakini mimi na wewe leo tunaona mama zetu wakipigwa na kupoteza maisha hali inasikitisha katika jamii.
Bi. Lucy Mushi mwanaharakati wa masuala ya wanawake anasema, katiba iliyopo ina vipengele vizuri na ingesimamiwa na kutekelezwa, hali ya unyanyasaji ingepungua kwa kasi
Anasema, Ibara ya 14 inaeleza kuwa kila mtu ana haki ya kuishi, lakini tunashuhudia ni wanawake wangapi wanapoteza haki hiyo kutokana na ukatili wa kijinsia?
Pia ibara ya 18 inatoa uhuru wa kila mtu kutoa maoni yake na ibara ya 22 inaeleza haki ya kila mtu kufanya kazi, lakini haya yote yamekuwa hayafanyiki hasa kwa wanawake,” anasema.
Anasema kwenye sheria ya ndoa ya mwaka 1971, kifungu cha 66 kinakataza adhabu ya viboko kwa wanandoa, lakini wapo wanawake wanapigwa kutokana na sababu mbalimbali.
Pia, kuna vifungu vinavyokataza kuambukiza magonjwa kwa makusudi, kutoroshwa, kutelekeza watoto, ajira ya shuruti, kutishia kuteketeza nyaraka, makosa ya kujamiiana, bughudha za kijinsia lakini havifuatwi.
Anasema, kifungu hicho kinalea unyanyasaji kwa watoto wa kike kuolewa katika umri mdogo, hali inayowafanya wakose haki yao ya msingi ya kupata elimu.
Pamoja na yote hayo, naishauri serikali kuona haja ya kuwapo kwa sheria inayojitegemea ya kuzuia ukatili majumbani anayoamini itasaidia kupunguza tatizo hilo katika jamii.
Wadau wa wanasema kama mwanamke angekuwa nafasi sawa na wanaume akaweza kuongeza uzalishaji kwa asilimia 20-30 na kuokoa watu milioni 100-150 kutoka katika njaa.
Inakadiriwa kuwa, asilimi 60 ya waathirika wa njaa ni wanawake na vijana. Mashirika ya chakula na kilimo yalibainisha uzalishaji utaongezeka kama kutakuwa na upatikanaji wa pembejeo na mbegu bora.
Imeandaliwa na Hyasinta Timothy kwa msaada wa mashirika
HABARI