Dawa mpya kwa wagonjwa wa Ukimwi
Huenda wagonjwa wa Ukimwi wakanufaika na dawa mpya
ambayo itawawezesha kutumia tembe moja kwa siku. Hii ni kwa mujibu wa
utafiti mpya nchini Marekani.
Jarida la Afya Lancet limesema tembe hiyo inajumlisha dawa zote nne
zinazokabiliana na makali ya ukimwi na kwamba ni salama.Utafiti unasema
hii itawarahisishia wagonjwa katika kuhakikisha wanafuata maagizo ya
madaktari wao.
Ukimwi hauna tiba lakini watafiti wameweza kutoa dawa za kukabiliana na maradhi nyemela.
Watafiti pamoja na kampuni za dawa wamechanganya dawa nne na
kutengeneza tembe moja ili kurahisisha utumizi wa dawa hiyo miongoni
mwa wagonjwa.
Tembe inayofanyiwa majaribio na ambayo imechanganywa dawa nne inauwezo wa kudhibiti virusi vya HIV kuongezeka mwilini.
Paul Sax mtafiti mkuum katika Hospitali ya Wanawake ya Brigham huko
Boston,Massachussetts ambaye pia ni mwanazuo wa ziada wa taasisi ya
afya ya Harvard ameelezea umuhimu wa tembe hii kwa kuimarisha afya ya
wagonjwa.
Dk. Sax ameongoza utafiti huu ambapo pia wamefanyia majaribio tembe
hii kwa wagonjwa 700 na kusema inafanya kazi, japo kulitokea matatizo
ya figo miongoni mwa waliotumia.
http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2012/06/120629_hiv_quad.shtml