Wednesday, February 22, 2012

MABOMU SONGEA
22/2/2012

Mji wa Songea wachafuka

Mji wote wa songea na viunga vyake upo kimya kabisa huku polisi wakionekana wanafanya patroo na kujaribu kuwa tawanya watu ambao watakuwa katika vikundi. Maduka yote yamefungwa na watu wamejawa na hofu kubwa. mirindimo ya risasi na mabomu ya machozi yanaendelea kurushwa hapa na pale kwenye mikusanyiko ya watu. 
Mpaka tunakwenda mtambuni watu watatu wamepoteza maisha , Poleni na matatizo Songea

UTATA WA UGONJWA MWAKYEMBE, MWENYEWE ANENA

 

Mbunge Mbeya, Kyela Dkt.Harrison Mwakyembe kabla ya kuumwa

KyelaDkt. Harrison Mwakyembe.

Mwakyembe afyatuka


Dk. Harrison G. Mwakyembe (Mb), NW-UJ                                                       Dar es Salaam 18/02/12
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Nimelazimika leo Jumamosi, tarehe 18 Februari, 2012 kutoa taarifa hii kwa vyombo vya habari kufuatia mkutano wa DCI Robert Manumba na waandishi wa habari jana (17/02/12) kuongelea, pamoja na mambo mengine, hali yangu ya afya na kuhitimisha, kienyejienyeji tu kuwa “sikunyweshwa sumu” ila naumwa tu ugonjwa wa ngozi bila kufafanua ugonjwa huo wa ngozi umesababishwa na nini! 
Napenda nisisitize mapema kabisa kuwa msimamo huo wa Jeshi la Polisi umenikera sana katika hali niliyonayo ya ugonjwa, kwanza kwa kuingilia mchakato wa matibabu yangu na uchunguzi wa kina kuhusu kiini chake unaoendelea hospitali ya Apollo nchini India ambako bado sijahitimisha matibabu yangu; pili kwa ufinyu wa uelewa unaojitokeza bayana kwenye tamko la Jeshi la Polisi unaosisitiza kuwa “sikunyweshwa sumu” wakati sumu si lazima unyweshwe ili ikudhuru, inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa tu; na tatu kwa Jeshi la Polisi kujiingiza kwenye suala ambalo kwa takriban mwaka mzima halijawahi kuwa na dhamira ya dhati ya kulielewa au kulichunguza mbali na kulifanyia mzaha kupitia magazetini.
Itakumbukwa kuwa tarehe 9 Februari, 2011 nilimwandikia barua IGP Said Mwema kumtaarifu kuhusu njama za kuondoa maisha yangu na ya viongozi wengine. Kwa kutambua kuwa Jeshi la Polisi la Tanzania daima husisitiza kuletewa ushahidi kwanza ndipo lifanyekazi, nilihakikisha nimeainisha katika barua hiyo kila ushahidi nilioupata au kupewa. (Utaratibu huu wa Jeshi la Polisi kusubiri kuletewa ushahidi mezani, kama ambavyo mahakimu wanavyosubiri ushahidi mahakamani, haupo popote pale duniani (ila Tanzania tu) kwani kazi ya msingi ya Polisi si kuletewa, ni kutafuta ushahidi. Polisi wanachohitaji duniani kote ni kupata clue au tetesi tu. Hiyo inatosha kufukua ushahidi wote unaohitajika). Pamoja na kujitahidi kuanika kila aina ya ushahidi niliokuwa nao, mambo manne yalijitokeza ambayo yalionyesha wazi kuwa Polisi hawakuwa na dhamira ya dhati ya kupeleleza suala hilo:

(i) Siku chache baada ya kumkabidhi IGP barua hiyo, nilitumiwa timu ya “wapelelezi” ofisini kwangu kuja kuchukua maelezo yangu ya ziada. Timu hiyo ilikuwa inaongozwa na ACP Mkumbo, afisa wa polisi ambaye wiki chache zilizokuwa zimepita alikuwa miongoni mwa askari waliotuhumiwa kupokea rushwa kwa lengo la kumbambikizia madawa ya kulevya mtoto wa Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi, suala ambalo mpaka leo hii uongozi wa Polisi umeshindwa kulitolea maelezo ya kuridhisha. Kwa msingi huo, nilikuwa nimeletewa mtuhumiwa wa rushwa/ ujambazi kuendesha uchunguzi wa watuhumiwa wengine wa ujambazi! Nikatambua mara moja kuwa zoezi zima lilikuwa la mzaha, tena mzaha mkubwa! 

(ii) Wiki chache baada ya barua yangu kuwasilishwa kwa IGP na timu ya ACP Mkumbo “kuanza kazi”, Jeshi la Polisi likachukua hatua ya kuwapongeza na kuwazawadia askari niliowatuhumu kushirikiana na majambazi! Huhitaji kuwa profesa wa falsafa kuelewa kuwa huo ulikuwa ujumbe tosha wa kunipuuza. 

(iii) Hivi karibuni tuhuma za askari polisi kujihusisha na vitendo vya ujambazi mkoani Morogoro zilipopamba moto na kuwagusa askari “wale wale” niliowatuhumu kwenye barua yangu, IGP alichukua hatua ya kuwahamishia mikoa mingine!

(iv) ili kunikatisha tamaa kabisa, barua yangu ya “siri” kwa IGP ikavujishwa kwa makusudi kwenye vyombo vya habari na kuchapishwa kama habari ambayo ilikebehi na kukanusha taarifa nzima niliyotoa, sijui kwa faida ya nani! Lakini huu ni mchezo wa kawaida kwa polisi kwani hivi karibuni Mhe. Waziri Samuel Sitta alipohojiwa na ofisa mwandamizi wa Jeshi la Polisi ofisini kwake, wakiwa wawili tu, taarifa ya kikao hicho ikawa magazetini ikikebehi ushahidi aliotoa Sitta! The integrity of the police force leadership is on the line.
Nimeelezea vizuri katika barua yangu kwa IGP kuwa kundi hilo la mauaji lilikuwa limeelekezwa kuniua kwa kutumia sumu, taarifa ambayo kwa karibu mwaka mzima Polisi hawakutaka kuifuatilia kwa sababu wanazozijua wenyewe. Sasa huu msukumo mpya wa Jeshi la Polisi kutaka kujua kama nilipewa sumu au la na kukurupuka kutoa tamko hata kabla ya kunichunguza nilivyo, kunihoji mimi na wasaidizi wangu ofisini na hata kuongea na mabingwa wa Kihindi wanaonifanyia uchunguzi, umetokea wapi? 

Aidha napata taabu kuamini kama DCI Manumba na wenzake waliisoma taarifa halisi ya matatibabu yangu au walisoma taarifa “nyingine”, na kama waliisoma taarifa hiyo wenyewe au “walisomewa”! Nasema hivyo kwa kuwa alichokisema DCI Manumba kwa wandishi wa habari hakifanani kabisa na picha iliyo kwenye taarifa halisi ya Apollo ambayo inatamka wazi kuwa kuna kitu kwenye bone marrow kinachochochea hali niliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaikia kukidhibiti/ kukiondoa huku vyombo vyetu vya dola vikipelekeshwa na mafisadi kusema bila msingi wa kisayansi na bila aibu: “hakulishwa sumu”, “hakulishwa sumu”!
Nimesoma darasa moja Kitivo cha Sheria Mlimani na DCI Manumba. Baadaye IGP Mwema alikuwa mwanafunzi wangu wa sheria Mlimani. Vigogo hawa wawili wa usalama wa raia nchini hawajanitendea haki, nao wanajua. Wanajua vilevile kuwa sitakaa kimya au kumung’unya maneno come what may pale ambapo haki inakanyagwa.
Tuendelee kuombeana afya na uhai ili kutendeane haki na vilevile tuitendee nchi yetu haki kwa kuvimalizia viporo vinavyokera vya Dowans, EPA, Kagoda n.k. kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

Mungu Ibariki Tanzania.
habari hii kutoka facebook bofya hapa

SUGU NA RUGE WAMALIZA TOFAUTI ZAO

MBUNGE WA MBEYA MJINI JOSEPH MBILINYI 'SUGU' NA RUGE WAMALIZA TOFAUTI ZAO MBELE YA WAZIRI MCHIMBI


TAARIFA:KWANZA POLENI NA SAMAHANINI KWA HALI YA SINTOFAHAMU ILIYOTOKEA LEO KUTOKANA NA TAARIFA ZA GHAFLA ZA USULUHISHI KATI YETU NA RUGE/CLOUDS FM,NI KUTOKANA NA UNYETI WA ISSUE YENYEWE ILIBIDI TUFANYE HIVYO KWA NIA NJEMA KABISA KWANZA NAOMBA TUJIPONGEZE KWA KUWA TUKIO LA LEO NI USHINDI KWA VINEGA KWA MAANA KWAMBA MADAI YETU YOTE YA MSINGI NDIO YALIKUWA MSINGI WA MAJADILIANO NA RUGE AMEKUBALI KUYATEKELEZA YOTE KUANZIA SUALA LA STUDIO YA RAIS KURUDISHWA KWA BASATA ILI IWE YA WASANII WOTE,PIA T.F.U IJIKABIDHI KWA CHAMA HALALI CHA WASANII YAANI T.U.M.A KAMA AMBAVYO TULIKUWA TUNADAI NA MPAKA ISSUE ZA WASANII KUNYANYASWA NA KUBANIWA NA PIA SUALA LA MALIPO HAFIFU VYOTE VIMEJADILIWA NA KUKUBALIWA KWA UTEKELEZAJI HAIKUWA KAZI RAHISI,KWANZA ILIANZA KWA WAO KUMPIGIA MWENYEKITI WANGU MBOWE KUTAKA TUKAE CHINI,AMBAPO KAMANDA MBOWE ALINISHAURI TUKAE NAO CHINI KAMA KWELI WANA NIA YA KUYAMALIZAÖBAADAYE WAKAMPIGIA MR SHIGONGO AMBAYE NI WAZI KUWA NI KATI YA WATU WANGU WA KARIBU NAYE BAADA YA KUONGEA NA MR. KUSAGA TU ALINIPIGIA NA KUNISHAURI HIVYO HIVYOÖNA KAMA HAIKUTOSHA WAKALIFIKISHA HILI SUALA KWENYE KAMATI YA BUNGE AMBAYO ILINITAKA NIIPE MAELEZO YA KIINI CHA MGOGORO NA NIKAFANYA HIVYO AMBAPO PIA BAADA YA KUNIELEWA WAKASHAURI NIKAE NAO CHINI NA HATIMAYE SUALA HILI LIKAISHIA MIKONONI MWA WAZIRI NCHIMBI PAMOJA NA MHE.

TUNDU LISSU(MP) KUWA WAPATANISHI WETU WAZIRI NCHIMBI AKAANZA KWA KUMUITA RUGE DODOMA NA ALIKUJA TUKAKAA KWA HATUA YA KWANZA NA HATIMAYE LEO TUKAKAA TENA MAKAO MAKUU YA WIZARA YA UTAMADUNI CHINI YA DR NCHIMBI NA MHE TUNDU LISSU NA HATIMAYE TUKAFIKIA HATUA HII YA LEO.

VITA YETU ILIKUWA NA HOJA HATUKUWA TUNAPIGANA TU KWA CHUKI BINAFSI KAMA BAADHI YA WATU WALIVYOKUWA WANAJARIBU KUIWEKA,KWAHIYO KAMA HOJA ZETU ZIMEELEWEKA KWA SASA TUNATAKIWA KUSHUKURU NA KUFURAHIA LAKINI NAOMBA NIWAHAKIKISHIE MISIMAMO IKO PALE PALE NA NIMEWAWEKA WAZI KUWA ANTI-VIRUS ITAENDELEA KUWEPO ILI KUENDELEA KU-SCAN VIRUS WENGINE KAMA MAMENEJA MASOKO NA WENGINE WATAKAOJITOKEZA KWANI NCHI INAPOSHINDA VITA AU HATA KUFIKIA TU MAKUBALIANO YA AMANI NA NCHI ADUI YAKE HAINA MAANA NCHI HIYO INAVUNJA JESHI LAKE ASANTENI SANANI

**********************************

MDAU : MIMI NAWAPONGEZA NI MFANO MZURI KATIKA KIPINDI HIKI CHA KWARESMA

SIKU YA MAJIVU

TUMSIFU YESU KRISTO

LEO NI SIKU YA MAJIVU MIMI NAKWENDA KUSALI KAWE
TUMWOMBE MUNGU ATUSAIDIE KUTUBU DHAMBI ZETU ILI TUWEZI KUFIKA MBINGUNI .

SIKU YA LEO INATUKUMBUSHA KWAMBA SIKU MOJA TUTAKUFA TUJIANDAYE MAPEMA

TUMSIFU YESU KRISTO


 Mtoto akipakwa majivu





Waumini zaidi ya bilioni moja wa madhehebu ya katoliki na waothodox ulimwenguni kote pamoja na wakristo kwa ujumla leo wameanza mfungo wa kwaresma.


siku arobaini za kujinyima na kujitesa kwa ajili ya maandalizi ya ufufuko wa Bwana Yesu.


Hili ni jambo la imani na limedumu kwa zaidi ya milenia mbili sasa.Wakristo huombwa na Kanisa kufunga kabisa siku ya jumatano ya majivu ambayo ilikuwa leo.

Kuna theolojia kubwa na ngumu juu ya tendo hili la imani.


Kufunga chakula na kujinyima anasa na vitu tunavyovipenda ili kuungana na wenye shida wakati huu.Naam tunategemea kuona matendo mema wakati huu na kwamba yatakuwa mazoezi mema ya kiroho na yataendelea hata baada ya pasaka.


 Kuna kupakwa majivu katika paji la uso na maneno tubuni na kuiamini injili husemwa ambamo waumini hujibu amina wakikumbushwa juu ya umuhimu wa kumrudia Mungu na kwamba tumetoka katika mavumbi na tutarudi kuwa mavumbi.Rangi za Zambarau hutumika zikiwa na maana ya toba.

Naam nasi Mjengwablog tunawatakia Kwaresma njema.

WAZIRI MUU MAMA PINDA WAKIPAKA MAJIVU

Friday, February 17, 2012

ASKOFU ACHANGIA VYOMBO VYA MUZIKI


ASKOFU wa Jimbo la Mashariki (TAG), Mchungaji Lawrence Kametta ametoa mchango wa vyombo vya muziki kwa Kanisa la TAG Kitunda Kati jijini Dar es Salaam ili kuendeleza vipaji vya muziki wa injili.

Askofu Kametta alitoa mchango huo juzi wakati akizindua rasmi jengo hilo la ibada, na kuomba kushirikishwa katika hatua zote za ununuzi wa vifaa hivyo.

Alisema kuwa badala ya watu kufurahia kwenda mpirani ama katika nyumba za anasa, ni vyema wakafurahia kuingia katika nyumba za mungu kwa kuwa sehemu hiyo ndiyo pekee ya tiba mbadala kwa matatizo yote.

"Vijana sugu, majambazi, wanaotumia dawa za kulevya matatizo yao hayawezi kumalizwa na viongozi, bali nyumba za mungu za pekee, ndio maana tujitolee kwa mioyo yetu yote kuzijenga nyumba hizi.
 
"Mtapata dhambi za bure kumlaumu Kikwete au kiongozi mwingine yeyote, kwa kuwa hakuna mwenye uwezo wa kubadilisha maisha ya wanadamu, tiba ya matatizo sugu ipo katika nyumba ya mungu, na nyumba hizi zikitumika sawasawa zitabadili maisha ya watu kimwili na kiroho,"alisema Askofu huyo.

Aliongeza kuwa, nyumba ya mungu ni karakana ya kiroho, hivyo ina uwezo wa kutengeneza mwili wa binadamu na ukarudi kuwa mpya na kuongeza kuwa ni tiba ya matatizo yote sugu.

"Wakati madaktari wakigoma, watumishi wa mungu hawana mgomo, wakati watoa huduma nyingine kwenye jamii wakigoma kwa kudai maslahi bora, watumishi wa mungu wapo wakitoa huduma bila kujali maslahi, wapo siku zote kwa tiba ya uponyaji. Hivyo ni vyema jamii ikazitiilia maanani nyumba za mungu kama mkombozi wa maisha yao duniani na mbinguni,"aliongeza Askafu Kametta.

Hata hivyo, aliwataka wananchi waelewe kuwa utakatifu wa mtu si mavazi, wala muonekano mzuri bali ni hali inayotoka ndani ya moyo ikiwa ni sambamba na kujitolea kufanya kazi za mungu kwa ibada na hata nyimbo.

Sambamba na kuchangia katika vyomvo vya muziki, Askofu huyo aliahidi kutoa mchango wake kwa kanisa hilo ambalo limejengwa kwa nguvu ya wananchi.

mwisho

MREMBO HUYOOO NA POZI LAKE