Tuesday, January 1, 2013

SAJUKI HATUNAYE


MWIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu  Juma Kilowoko ‘Sajuki’ amefariki dunia asubuhi muda wa saa moja kasoro akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa .R.I.P


Friday, August 3, 2012

DKT. ULIMBOKA


Hali ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dkt. Steven Ulimboka, inaendelea vizuri lakini si wa kupona leo wala kesho, imeelezwa na vyanzo vyetu.

Dkt. Ulimboka anayetibiwa Afrika Kusini, yupo chini ya uangalizi mkali wa madaktari katika hospitali aliyolazwa na wanafanya kazi kubwa kuhakikisha anapona.

Chanzo chetu (gazeti la Uwazi) kimetoa taarifa kuwa, Dkt. Ulimboka anapata matibabu sahihi kwa sababu hospitali aliyolazwa ni ya uhakika.

Awali, kabla ya mazungumzo ya moja kwa moja kwenye simu, ripota wetu alimtumia SMS mtoa habari wetu kumuulizia maendeleo ya daktari huyo naye akajibu: "He's recovering slowly" (Anapona taratibu).

Alipomuuliza Watanzania wamtegemee lini daktari huyo kurudi nchini, alijibu: "Itachukua muda kupona. Muhimu kwa sasa ni Watanzania na wote wanaompenda, wamuombee kwa Mungu ili matibabu yaende sawa."

Chanzo chetu kilibainisha kuwa usalama wa Dkt. Ulimboka ni wa uhakika, kwani watu wanaomlinda hospitalini hapo wapo makini.

"Nani asiyejua mazingira ya hatari aliyonayo Steven (Dkt. Ulimboka)? Hii inasababisha maisha yake hospitalini yawe chini ya ulinzi mkali. Kwanza si kila mtu anaruhusiwa kwenda kumuona. Hospitali yenyewe aliyolazwa hatutaki itangazwe. Maisha ya Steven ni siri," alisema mtoa habari wetu na kutoa siri hii:

"Wiki iliyopita pale hospitali alipolazwa, alitokea mtu fulani hivi Mwafrika. Muonekano wake ukawafanya watu wahisi ni Mtanzania. Watu wanaohusika na usalama wa Steven walikuwa makini sana.


Kilichosababisha yule mtu aonekane ni Mtanzania ni fulana aliyovaa, kifuani ina ramani ya Tanzania. Watu wanaomlinda Steven wakaogopa sana, wakamfuatilia hatua kwa hatua bila mwenyewe kujua. Bahati nzuri naye alikuwa amekwenda kwa shughuli zake na akaondoka salama.

 Kwa kifupi, hali ilivyo pale hospitali ni kwamba ulinzi ni mkali, tena afadhali mtu awe wa taifa lingine, Watanzania ndiyo wanaogopwa zaidi, kwani huwezi kujua nani mzuri wa Steven na adui yake ni yupi."

Taarifa kwa hisani ya Mpekuzi 


Tuesday, July 24, 2012

Waziri ajiuzulu baada ya ajali ya meli Zanzibar





Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Serikali ya Zanzibar Hamad Masoud Hamad amejiuzulu wadhifa wake, jana kufuatia ajali ya kuzama kwa meli ya MV Skagit iliotokea Julai 18, 2012.

Na Victor Robert Wile
 

 Hatuwa hiyo imefikiwa baada ya rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein amekubali ombi la Waziri Hamad Masoud kujiuzulu.


Kufuatia kujiuzulu kwa waziri huyo, Dk. Shein amemteua mwakilishi wa Jimbo la Ziwani kupitia Chama cha Wananchi, CUF, Bwana Rashid Seif Suleiman kuchukua nafasi hiyo.

Katika hatua nyingine makamu wa pili wa rais wa serikali ya Zanzibar balozi Seif ali idd ametangaza kusitisha safari zote za meli ya MV Karama ambayo inamilikiwa na Kampuni ya Sigal kufanya safari zake kati ya Zanzibar na Dar baada ya kubainika kwamba inauwezo wa kusafiri umbali wa kilometa saba pekee.

Wakati huo huo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein ameunda Tume ya kuchunguza ajali ya kuzama kwa meli ya MV Skagit.
 

Thursday, July 19, 2012

Taarifa ya meli kuzama Zanzibara


Jumatano, July 18, 2012

Taarifa ya Serikali Meli iliyozama 


MAAFA YA KUZAMA KWA MELI ZANZIBAR

Meli ya Mv. Star Gate imezama karibu na Kisiwa cha Chumbe ambapo watu 12 wamefariki hadi muda huu na wengine kadhaa wamejeruhiwa.

Akitoa taarifa fupi kwa waandishi wa habari,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini alisema taarifa za kuzama kwa meli hiyo ilitolewa na Boti iendayo kasi ya Kilimanjaro III iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Zanzibar ndipo ilipoiona meli hiyo ikizama.

“Tulipata taarifa kutoka Boti ya abiria ya Kilimanjaro III saa 7:50 mchana waliporipoti kuona meli ikizama karibu na Kisiwa cha Chumbe” Alisema Waziri Mwinyihaji.

Waziri huyo alisema Meli hiyo imezama maili sita kuelekea Kisiwa cha Yasin Kusini mwa Kisiwa cha Chumbe kilichopo Unguja maili kadhaa kutoka Bandari ya Malindi.

Waziri Mwinyihaji alisema idadi ya abiria walikuwa 250 ambao ni watu wazima, watoto 31 na mabaharia 6. “Tumepeleka waokoaji, kuna boti tano zipo eneo la tukio kushirikiana na waokoaji wengine” Alisema Waziri Mwinyihaji.

Alisema maiti zote zitapelekwa viwanja vya Maisara Zanzibar kwa ajili ya ndugu na jamaa kuzitambua maiti za ndugu zao ambapo majeruhiwa wote watatibiwa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja.

Katika Bandari ya Malindi mwandishi wetu ameshuhudia maiti kadhaa zikiwemo za watoto zikishushwa, Miongoni mwa abiria waliookolewa ni raia 13 wa Mataifa mbalimbali ya nje huku raia mmoja ambaye hakuweza kutambuliwa utaifa wake amepoteza maisha.

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd alifika eneo la Bandari ya Malindi Zanzibar pamoja viongozi wengine akiwemo Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, Mawaziri na baadhi ya Wajumbe a Baraza la Wawakilishi walikuwepo kutoa msaada unaohitajika.

Katika eneo la pembezoni mwa bandari ya Malindi, makundi ya wananchi yalikuwa yamekusanyika wakisubiri taarifa za tukio hilo tangu saa 8:30 mchana.

Vikosi vya ulinzi na usalama, msalaba mwekundu na watoaji wengine wa misaada ya dharura walifika kwa haraka eneo la tukio.

Hadi sasa kazi ya uokoaji inaendelea karibu na Kisiwa cha Yasin ilikozama meli hiyo.

Meli ya Mv. Star Gate inamilikiwa na kampuni ya kizalendo ya Sea Gull Sea Transport Ltd ambayo mwaka 2009 Meli yake nyengine ya Mv. Fatih ilipinduka na kuzama katika Bandari ya Malindi Zanzibar na kua watu sita.

Mwaka jana Zanzibar ilikumbwa na maafa baada ya Meli ya Mv. Spice Islanders kuzama katika bahari ya Hindi eneo la Nungwi katika Kisiwa cha Unguja ikielekea Kisiwani Pemba ambapo taarifa rasmi ya Serikali ilisema watu 197 walipoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa.

MELI YA SKAGIT YAZAMA

Meli ya Skagit inayomilikiwa na  Kampuni ya Seagull imezama Maeneo ya Chumbe


Meli ya Mv Skagit iliyokuwa safarini kutoka Dar kuelekea Zanzibar imezama majira ya saa nane mchane hivi leo katika maeneo Pungume na Chumbe baada ya kukumbwa na upepo mkali.

Meli hiyo inayosadikiwa kuwa na abiria 250 inasemekana imepindukia upande mmoja na huku abiria wengi wakiweza kuokolewa kutokana na jitihada mbali mbali kupitia vile vile msaada wa boti za Mv Kilimanjaro, Tug ya Bandari na vyombo vyengine