Tuesday, July 24, 2012

Waziri ajiuzulu baada ya ajali ya meli Zanzibar





Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Serikali ya Zanzibar Hamad Masoud Hamad amejiuzulu wadhifa wake, jana kufuatia ajali ya kuzama kwa meli ya MV Skagit iliotokea Julai 18, 2012.

Na Victor Robert Wile
 

 Hatuwa hiyo imefikiwa baada ya rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein amekubali ombi la Waziri Hamad Masoud kujiuzulu.


Kufuatia kujiuzulu kwa waziri huyo, Dk. Shein amemteua mwakilishi wa Jimbo la Ziwani kupitia Chama cha Wananchi, CUF, Bwana Rashid Seif Suleiman kuchukua nafasi hiyo.

Katika hatua nyingine makamu wa pili wa rais wa serikali ya Zanzibar balozi Seif ali idd ametangaza kusitisha safari zote za meli ya MV Karama ambayo inamilikiwa na Kampuni ya Sigal kufanya safari zake kati ya Zanzibar na Dar baada ya kubainika kwamba inauwezo wa kusafiri umbali wa kilometa saba pekee.

Wakati huo huo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein ameunda Tume ya kuchunguza ajali ya kuzama kwa meli ya MV Skagit.