Friday, May 27, 2011

YESU NDIO KIMBILIO LANGU

MAOMBI YA MWANAMKE
1. Maombi ya mwanamke yaweza kufungua familia toka kwenye vifungo vya Ibilisi .
2 Maombi ya mwanamke yaweza kufungua mpaka kizazi cha nne.


/home/majira/Desktop/girl-and-woman-praying-1[1].jpg3 Maombi ya mwanamke yaweza kuhuisha upya nafsi na roho hata palipokatika tamaa.

4. Maombi ya mwanamke ni baraka na mafanikioya familia

5. Maombi ya mwanamke ni ngao imara katika familia
6. Maombi ya mwanamke yaleta faraja ya familia

7. Maombi ya mwanamke ni ulinzi wa familia yako
8. Maombi ya mwanamke yaweza kuwa ni patanisho la familia


9. Maombi ya mwanamke yaondoa laana za kurithi
Mwanamke, usichoke kuomba maana sisi tu walinzi wa familia zetu na tena vita vyetu ni vya roho kwa hiyo yatupasa kupigana vita katika ulimwengu wa roho na si ulimwengu wa mwili. "Kesheni mkiomba"

Nimeambiwa nitume ujumbe ujumbe huu kwa kila mwanamke ninayempenda na kutaka awe na maisha mazuri na familia yenye furaha nami nimefanya hivyo hapa...DM.


WANAWAKE 48 WANABAKWA KILA SAA NCHINI CONGO


Utafiti uliofanywa na wanasayansi wa Marekani umeonyesha kuwa takriban wanawake na wasichana 48 wanabakwa kila saa katika Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.

Utafiti huo, uliochapishwa katika jarida moja la afya,umegundua kuwa wanawake 400,000 kati ya umri wa miaka 15-49 walibakwa katika muda wa miezi 12 kati ya mwaka 2006 na 2007.
Idadi hii ni kubwa ikilinganishwa na idadi ya awali ya kuonyesha kuwa wanawake 16,000 wanabakwa katika muda wa mwaka mmoja iliyotangazwa na umoja wa mataifa.
Serikali ya DRC inasema hali hii ya sasa inaonyesha kuwa wanawake wana nafasi ya kutoa taarifa zaidi juu ya matukio ya ubakaji.
Ubakaji umekuwa kama jambo la kawaida katika mapigano yanayoendelea mashariki mwa Congo.
Amber Peterman, mtafiti mkuu,anasema: "utafiti wetu umedhihirisha kuwa idadi ya matukio ya awali haionyeshi hali halisi ya matukio ya ubakaji yanayoendelea kujitokeza nchini Congo.


Amani ni muhimu jamani kwa nchi yoyote ile nikiwa kama mtanzania naomba kila mmoja aeneze ujumbe wa amani na hata kukemea pindi inapotokea uvunjwaji wa amani POPOTE pale.Wanaume badala ya kwenda kutafuta riziki mnashika silaha kupigana na kiukweli sisi wasichana/wanawakena watoto ndio kundi linaloathirika na mapigano kama hayo.Tuchukulie mfano nchi ya Rwanda wakati wa mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 nchi hiyo ilibaki na population kubwa sana ya wanawake wanaume wakiwa wamekufa kwenye mapigano.Nchi ya Congo wanawake wanabakwa sana hasa katika maendeo yenye mapigano mtu anabakwa mbele ya mumewe,watoto n,k inaogopesha kiukweli.


Arnold amewahi kunukuliwa akisema If you have the ultimate love for your wife and she has it for you, I think you have a great head start ... That's not to say it won't be difficult sometimes. You go through your ups and downs but you work through it ....sasa sijui nini kimetokea maana hawajasema