Zaburi 35:1 Ee Bwana utete nao wanaoteta nami Upigane nao wanaopigana nami.
KUHUSU VILEVI KATIKA BIBLIA
Soma Waraka wa kwanza wa Petro, sura 4, kuanzia mstari wa kwanza mpaka wa mstari wa tano ( 1 Petro 04:01-05) inasomeka kama ifuatavyo:-
"
1 Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi.
2 Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani.
3 Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;
4 mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi, wakiwatukana.
5 Nao watatoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa.