Kiboko Kinaweza Kuondolewa Kwenye Malezi Ya Mtoto?
Charles Taylor Alifadhili Vita Sierra Leone
Charles taylor akiwa mahakamani |
Majaji
katika mahakama maalum ya kimataifa wamempata na hatia Rais wa zamani
nchini Liberia Charles Taylor na hatia ya kufadhili vita nchini Sierra
Leone.
Taylor ameshtakiwa mbele ya mahakama maalum inayochunguza uhalifu wa kibinadamu nchini Sierra Leone.Kesi dhidi ya kiongozi huyu imechukua takriban miaka mitano.
Taylor alituhumiwa kwa kuwaunga mkono waasi ambao waliwaua maelfu ya raia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone kati ya mwaka 1991-2002.
Hata hivyo mahakama haijampata na hatia ya kuamrisha kutekelezwa kwa uhalifu wowote.
Jaji mwandamizi wa kesi ya Charles Taylor Richard Lussick amesema mahakama inao ushahidi kwamba Taylor alifadhili kwa hali na mali maasi ya nchi jirani ya Sierra Leone.
chanzo:BBC