Tuesday, March 13, 2012

Airtel yazindua mtandao wa kasi zaidi



Airtel yaja na internet ya 3.75G kutoa ubora na kasi zaidi kwa wateja.

•    Airtel yajenga mtandao bora wa data barani Afrika
•    Uzinduzi wa Airtel 3.75G Tanzania utawapatia watumiaji  wa data
huduma yenye kasi na ubora zaidi  katika simu zao
•    Kupitia internet ya 3.75 itawawezesha wateja kufanya maongezi ya
simu ukiwa unamwona mtu, kuangalia TV, kutuma na kupokea barua pepe na
kuperuzi na kupata miziki kutoka kwenye tovuti kupitia simu zao.

Jumanne 13 Machi 2011, Dar es Saalam–Airtel Tanzania leo imepiga hatua
kubwa katika kujenga na kukuza mtandao wa technoloijia ya 3.75G Africa
kwa  kuzindua rasmi  mtambo wa 3.75G nchini Tanzania,ambapo Airtel
itatoa huduma ya internet yenye ubora na kasi zaidi  kwa watumiaji
wenye simu zenye uwezo wa kutumia internet wawapo mahali popote.

Mkurungenzi Mkuu wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Sam
Elangalloor alieleza” kukua kwa technolojia hii kutakuza ufanisi
katika vyombo mbalimbali vya  mawasiliano (multimedia), kwa kuwa 3.75G
itatoa internet yenye ubora na kasi  zaidi kwa  kuwezesha wateja
kufungua tovuti mbalimbali, kufanya maongezi  ya simu kwa njia ya
video , kuangalia TV, kutuma na kupokea barua pepe na pia  kupata
muziki kutoka kwenye tovuti  kwa kutumia simu.
Teknologia ya 3.75G itatoa nafasi kwa wateja kupata mawasiliano ya
data kwa njia tofauti na ya pekee kabisa, ndio maana leo Airtel
tunajisikia fahari kuwa internet yetu ya 3.75G ni uvumbuzi na
muendelezo wa mtandao (platform) wetu ili kuwawezesha wateja wa Airtel
wote nchini kupata huduma ya internet au data yenye ubora wa hali ya
juu pamoja na kasi zaidi”

Tunafanya ubunifu wa kuleta huduma zenye ubora zaidi katika mtandao
kwa kuzingatia kuwa sasaivi dunia inauhitaji mkubwa sana wa huduma za
kimtandao hasa kupitia simu ya mkononi
Ukirejea takwimu zilizofanywa na kampuni ya McKinsey & Co.

Telecommunications zinaonyesha  mpaka sasa kuna watumiaji wa simu za
mkononi wapatao milioni 400 Afrika, na kwamba bara la  Afrika ni moja
kati ya  soko linalokuwa kwa kasi zaidi huku soko la simu za mkononi
likiendelea kukua na kupanuka zaidi na kufikia kutoa huduma za
internet, huduma za benki kwa njia simu (mobile banking)  na biashara
kwa njia ya mtandao yaani (mobile commerce) .

Hivyo basi kwa kuzingatia hili,  ndio maana Airtel tunaendelea na
mikakati kama hii ya kuwaletea wateja internet yenye kasi zaidi ya
3.75G ambayo ni sambamba  na lengo letu la kuendea kupanua mtandao
ili kutoa mwanya wa mawasiliano kuwafikia wakazi wengi wa vijijini
ambao walikuwa wamesahaulika na mapinduzi ya mawasiliano katika bara
la Afrika.

“wote tunafahamu kuwa mawasiliano ni nyenzo muhimu kwa maendeleo ya
jamii ya sasa lakini bado kunachangamoto kubwa sana katika kupata
huduma hii kwa baadhi ya sehemu barani Africa. Lakini tukumbuke
Mawasiliano ni haki ya msingi kwa kila mtu na si vinginevyo hivyo kwa
kupitia mtandao wa Airtel internet yenye kasi zaidi ya 3.75G ninaamini
tutaweza  kuunganisha idadi kubwa ya watu kwa kukuza mahusiano ndani
na nje ya ya jamii zetu, kuendeleza na kuutangaza utamaduni wetu,
pamoja na kupanua wigo wa wale wanaofanya biashara kupitia mtandao wa
internet “ Aliongeza Elangalloor.

Ikiwa tayari mteja ameunganishwa na teknologia ya 3.75G simu yake
itaonyesha 3.75G, HSDPA, WCDMA or HSPA. Hii inategemeana  na Aina ya
simu aliyonayo mtumiaji lakini kasi ya kuunganishwa ni yenye ubora
zaidi.

Airtel itaendelea kuwekeza kwenye huduma ya data katika soko lake lote
huku lengo likiwa ni kuwa mtandao mpana zaidi wa teknologia ya 3.75G
katika bara zima, na itaendelea kutoa huduma bora na inayokidhi
mahitaji ya watumiaji