Thursday, March 8, 2012

WANAWAKE WAKIWA KATIKA SHUGHULI ,SIKU YA WANAWAKE DUNIA


WANAWAKE TUKUMBUKE SISI NI NGUZO KATIKA JAMII 
HERI SI  WANAWAKE WOTE  DUNIANI KWA WANAWAKE WOTE NA WAPENDA


isha kama umeguswa.

NOTE:Kama ni mtu wa kuchukua mambo kirahisi bila kufikiri kwa kina unaweza kuhisi ni maswali yasiyo na maana.Ila ni maswali makubwa sana unayotakiwa kujiuliza.


JAMANI TUWE NA MOYO WA KUSAMEHE


HABARI KAMILI YA ILE KESI YA ASHA MKWIZU KAMA NILIVYOAHIDI

Stoy hii ilianza kwenye leo tena kama ifuatavyo,kawaida katika kipindi changu huwa napenda sana kumshirikisha msikilizaji wangu mwanafamilia wa leo tena.Nikaomba kama kuna mwenye story anataka kutushirikisha apige simu tuongee nae.Kweli akapiga simu dada mmoja kutoka Tanga akasema yeye amekuwa akitembea na mume wa mtu katika mahusiano yao mkewe wa huyo jamaa akagundua.
Baada ya kugundua kwa muda mrefu wakawa wakitukanana matusi kwenye simu lakini baadae kumbe yule mke alipoibua hoja kwa mumewe muwe akamwambia ni kweli na anataka kumuoa huyo hawara.
Mwenye mke akaanza msako kumtafuta huyo dada,muda si mrefu akamjua na akamfata mpaka kwenye duka analouza.Kufika kule akamwambia mimi sina ugomvi na wewe na mume wangu ameniambia anataka kukuoa.Mimi kilichonileta hapa nataka tuwe kitu kimoja tuwe marafiki.
Basi kweli dada akakubali na mpaka natupigia simu wamekuwa mashost pika pakua,wanatembeleana,wanasindikizana mahali,wanatumiana meseji na kupigiana simu n.k
 Sasa hili likatuacha na maswali ni kweli mke wa jamaa ana nia njema na hawara wa mumewe au la?Wakati tukijiuliza maswali kuna dada anaitwa Sharon akanitumia meseji akasema mwaka 1984 kuna mwanamke anaitwa Asha Mkwizu aliwahi kumuua hawara wa mumewe kwa ukaribu kama huo wa urafiki.Alimuua kinyama tena nyumbani kwake baada ya kumkaribisha kula na kunywa.Nikampigia simu akatupa kisa chenyewe kwa urefu ilivyokuwa.Na tukasisitiza kuwa watu wawe waangalifu na urafiki wa upande pinzani kumbuka huyo anampenda mumewe na haujui mangapi wanayapitia pamoja moyo wa mtu kichaka ni ngumu kujua anawaza nini.
Wakati tunaendelea kuna kaka akanitumia meseji akasema nijaribu kugoogle hiyo story ya kesi ilivyokwenda ipo nitaiona.Baada ya kugoogle kweli nikaiona kwenye mtandao wa jamii forums ikiwa imewekwa na mtu anayetumia jina la MTAMBUZI.Ni ndefu siwezi kuiweka yote ila naweka link yake uingie ukaisome huko.Huyo mama alihukumiwa kunyongwa wakati ule wa Nyerere lakini alipewa msamaha wakati wa Mzee Mwinyi 'ruksa'.Nasikia yupo hai na nimepewa direction alipo bado nafanya mchakato namna ya kukutana nae kama ikiwezakena.
INGIA HAPA KUISOMA
http://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/234276-asha-mkwizu-hauli-na-kesi-ya-kumuuwa-hawara-wa-mumewe-6.html#post3617175

KWA HISANI YA DINA MARIOS BLOG