Wednesday, February 29, 2012

MAHUBIRI MENGINE AAAAAA


Mahubiri


Ghafla unasikia mhubiri kwenye kituo cha daladala, nyinyi wanaume hamtaki kunisikiliza kwani mnawahi kwenda guest house kuzini, nanyi wanawake hamnisikilizi kwani neno langu linawachoma kwani mmetoa sana mimba,mna mapepo ndiyo maana mnavaa masuruali, wote mnaoitwa Asha,Amina,Abdallah,na nani sijui eti waislamu mnaenda motoni kwani mungu wenu nu Ibilisi,wakatoliki wote ni wa motoni kwani wanaabudu masanamu, wanasalia marehemu na wanakunywa pombe,hata walutheri na waanglikana wanaenda motoni kwani wanawafuata wakatoliki kwenye baadhi ya mambo.
 Njooni kwa Yesu anaokoa.mimi nilikuwa mzinzi wa wazinzi, nimewahi kuua watoto kwa kutoa mimba,sasa mnaona nilivyookoka nampenda Yesu.halafu nyinyi majina ya makabila msiyatumie yana mizimu na shetani hupenda watu wenye majina kama hayo.
Unakuta mtu anaitwa mwakalinga, malafyale sijui Rwegasira,mara huyo anitwa Otieno,manka,mara sijui mwana malunde,wote ni motoni.kwa nini msiitwe imani,furaha, ibrahimu,elshadai,asantemungunk,Mimi naitwa bwanaanaokoa,ni jina jipya, nimebatizwa kwenye kanisa la waliojitenga nao full gospel, lina upako.Acha dini haitakupeleka kokote,wazazi wako walikudanganya kukuweka dini uliyopo,mnaabudu masanamu, mnafuga majini, mtakwenda jehanamu
Nyinyi vijana mnavuta bangi na kulewa.mnajifanya mnawahi kazini wakati mnakwenda kuzii, tena nyinyi mnaovaa vizuri mnafanya ushoga na usagaji mnaniangalia nini? wengi wenu ni watoto wa nje ya ndoa, njooni kwa yesu, sisi tunaombea wagonjwa wanapona, tunawapa viza kwenda marekani, tunawapa utajiri na tunafufua misukule yote.Biblia inasema sisi wahubiri kazi yetu ni kuhubiri, mukisikia musiposikia shauri yenu,Mungu awabariki sana.
Ndugu zangu sasa haya ni mahubiri au anatafuta maneno?