Thursday, April 19, 2012

JAMANI TUMSADIE WASTARA


Nakumbuka rafiki yangu Gerald Hando aliniambia Dina ukisikiliza sana matatizo ya watu unaweza ukaogopa maisha.Yaani leo nimealia na nimehuzunika sana nilipokutana na Wastara na kunipa hadithi nzima ya kinachomkabili sasa.Na mpaka naandika hapa bado namfikiria sana.Ni mwanamke aliyepitia mengi na anendelea kupitia mitihani mingi akiongea analia kiasi cha kunifanya hata mimi nilie.Kweli binadamu hatujafa hatujaumbika tumshukuru Mungu kwa kila jambo unaweza kudhani wewe una mitihani hapa duniani kumbe kuna aliyekuzidi.
Najua nilikuahidi kuwa nitaruka leo na Wastara live katika leo tena ila nilichofanya nimerekodi kipindi kizima ambacho kitaruka hivi karibuni.Huyu mwanamke anahitaji msaada sana wa mumewe kutibiwa mwezi ujao anatakiwa kusafiri kwenda India kwa hayo matibabu ambayo yanaweza kugharimu zaidi ya ml 25 hela ambayo hata robo yake hawana.Nitakuomba sana mtanzania ushirikiane nami na hii familia hata kama hatutafikia pesa yote angalau ifike nusu.Hapa nimeshaanza kufanya mazungumzo na watu kadhaa ninao wajue ili tuhamasishane kuchangia haya matibabu.Wasanii tunaowaona kwenye movie wakiendesha magari ya kifahari na majumba yale sio maisha yao halisi hata kidogo ni watu na shida zao.
Kuna ac namba nitaitoa pamoja na tigo pesa ili kwa unaeweza kuchangia kwa huko.


 Kwa habari zaidi soma Dina Marios blog