Friday, April 27, 2012

SHULE NA VIBOKO

Kiboko Kinaweza Kuondolewa Kwenye Malezi Ya Mtoto?

Reactions::

Wasikilize Wabunge Walioanguka Saini Za Kumng'oa Pinda!

video


Charles Taylor Alifadhili Vita Sierra Leone

Charles taylor akiwa mahakamani
Majaji katika mahakama maalum ya kimataifa wamempata na hatia Rais wa zamani nchini Liberia Charles Taylor na hatia ya kufadhili vita nchini Sierra Leone.
Taylor ameshtakiwa mbele ya mahakama maalum inayochunguza uhalifu wa kibinadamu nchini Sierra Leone.
Kesi dhidi ya kiongozi huyu imechukua takriban miaka mitano.
Taylor alituhumiwa kwa kuwaunga mkono waasi ambao waliwaua maelfu ya raia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone kati ya mwaka 1991-2002.
Hata hivyo mahakama haijampata na hatia ya kuamrisha kutekelezwa kwa uhalifu wowote.
Jaji mwandamizi wa kesi ya Charles Taylor Richard Lussick amesema mahakama inao ushahidi kwamba Taylor alifadhili kwa hali na mali maasi ya nchi jirani ya Sierra Leone.
chanzo:BBC