Tuesday, April 3, 2012

CHADEMA YASHINDA ARUMERU BAADA YA MATOKEO KUTANGAZWA 3/APRILI/2012

NI CHADEMA ARUMERU

 Mbunge mteule wa jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akiwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Leganga, ambako kulifanyika mkutano wa kuwashukuru wapiga kura wa jimbo hilo leo
 Mbunge wa Arusha mjini Mh Godbless Lema akiwasili mkutanoni
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh Freeman Mbowe, akiwashirikisha wananchma na wapenzi wa chama hicho, kuitikia msemo wa ‘Peoples Power’, wakati wa mkutano wa kuwashukuru wapiga kura wa jimbo la Arumeru Mashariki, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Leganga leo.
 Mbunge wa Moshi Mjini Mzee Ndesamburo akihutubia
Mistari: Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini, Mh Joseph Mbilinyi maarufu kama Mr Sugu, akitumbiza wakati wa mkutano wa kuwashukuru wapiga kura wa jimbo la Arumeru Mashariki kwa kumchagua mbunge wa Chadema, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Leganga leo. Picha na mdau Joseph Senga

PICHA KWA HISANI YA BLOG YA MATUKIO-MICHUZI