Hollande atazindua sera mpya Ufaransa
Hollande amedokeza mabadiliko makubwa ya sera
Rais mteule wa Ufaransa Francois Hollande ameanza utaratibu
wa kuunda serikali mpya baada ya kuwaelezea wafuasi wake kuwa ushindi
wake ni ishara ya kuwa sera za kupunguza matumizi ya serikali barani
ulaya zinakwisha.Bw Hollande ameahidi kuwa atatoa mapendekezo mapya kuhusu mikopo kati ya nchi wanachama wa umoja wa ulaya.
Mapendekezo yake yatahimiza sana kukuwa kwa uchumi wa nchi wanachama na sio kupunguza matumizi ya serikali hizo.
Mgombea huyo wa chama cha kisoshalisti alipata 52% ya kura katika duru ya pili ya uchaguzi huo.
Nicolas Sarkozy ndiye rais wa kwanza aliyekosa kuchaguliwa kwa awamu ya pili nchini Ufaransa tangu mwaka wa 1981.
Rais Sarkozy anatarajiwa kumkabidhi madaraka Bw Hollande May 15.
Bw Hollande atakuwa rais wa kwanza wa kisoshalisti nchini Ufaransa, kwa kipindi cha miaka 17.
Punde baada ya kura za awali kuonesha matokeo, Rais Sarkozy alikiri kuwa ameshindwa, na alimpigia simu Bw Hollande kumtakia heri