Uhaba Wa Walimu Na Madarasa
MWALIMU MKUU WA SHULE YA MSINGI KIDUGALO-Owini Mpangala (NAMTUMBO)
mojawapo ya darasa shule ya msingi selous (Darasa la sita)-Namtumbo
Na Vicent Mnyanyika, HakiElimu-Namtumbo
UHABA
wa vyumba vya madarasa ni moja ya changamoto kubwa inayoikabili sekta
ya elimu Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma hali inayosababisha kushuka
kwa kiwango cha elimu wilayani humo.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni wilayani hapa baadhi ya
walimu wanaofundisha katika shule za msingi wilayani Namtumbo wamesema
wanatamani kuacha kazi au kuhama kutoka na changamoto nyingi
zinazowakabili kwa muda bila ya kupatiwa ufumbuzi. Wanasema kuwepo kwa
changamoto hizo za muda mrefu kuchangia kushusha kiwango cha elimu
katika shule nyingi za mjini.
Uchunguzi
uliofanywa katika shule za msingi Rwinga, Selou, Mkapa na Kidugalo zote
kutoka Kata ya Rwinga umebaini shule hizo kukabiliwa na uhaba mkubwa wa
vyumba vya madarasa hali inayowalazimu walimu kujenga vibanda vya nyasi
ili kuwaepusha wanafunzi kukosa masomo kwa sababu ya uhaba huo wa
madarasa.
Hali
hiyo pia imewalazimu walimu kutumia kutumia vyumba vichache vilivyopo
kwa kuwachanganya wanafunzi wa madarasa mawili katika chumba kimoja
hali inayotia shaka mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi.
Mwandishi
ametembelea Shule ya Msingi Kidugalo na kushuhudia zaidi ya wanafunzi
200, wa kuanzia darasa la tatu mpaka la sita wanasoma katika vyumba
viwili vya madarasa huku wakiwa wamegeuziana migongo hali ambayo
inachangia kushusha taaluma katika shule hiyo.
Halmashauri
ya Wilaya ya Namtumbo ina shule za msingi 107 kati ya hizo shule 105
zinamilikiwa na Serikali na shule mbili ni za watu binafsi na mashirika
ya dini.Jaji wa kike MTANZANIA KUTUWAKILISHANJE
Ni Jaji Eusebia Munuo amechaguliwa kuwa rais wa chama cha majaji wanawake ulimwenguni.Tunampongeza na kumtakia kazi njema
Picha Kwa Hisani ya MICHUZI