Friday, May 11, 2012

RAIS Kikwete kukabidhi nyumba waathirika wa mabomu G,mboto

Kikwete kukabidhi nyumba waathirika wa mabomu G,mboto


RAIS Jakaya Kikwete anatarajia kuwakabidhi nyumba waathirika wa  mabomu  ya  Gongolamboto,walizojengewa na Serikali katika eneo la  Yangeyange,Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Mkuu wa Mkoa huo Bw.Sadik Mecky Sadik wakati wa kuweka jiwe la msingi katika nyumba hizo.

Bw.Sadik alisema kuwa waathirika hao watakabidhiwa nyumba hizo 35 mwezi ujao baada ya ujenzi wake kukamilika.

Alisema kuwa katika ya nyumba hizo nyumba ya mwananchi mmoja imejengwa eneo la Mbweni Wilayani Kinondoni ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 65 baada mwananchi huyo kukataa kujengewa eneo hilo


"Wananchi hawa walikuwa wakilipiwa kodi ya nyumba na Serikali ambapo mara baada kukabidhiwa nyumba na serikali itakuwa imetua mzigo mkubwa iliokuwa imeubeba katika kipindi chote cha "alisema Bw.Sadik.

Alisema kuwa tathimini za malalamiko ya fidia  na tathimini ya nyumba 24 zilizokuwa katika orodha ya kujengwa upya na zikaonekana zinahitajika ukarabati zimefanyika na kuwasilishwa kwa Mthamini Mkuu wa Serikali.

Bw.Sadik alisema kuwa timu iliundwa na kuandaa tathimini ya malalamiko ya wananchi 168 na kuwasilishwa kwa mthamini mkuu wa serikali wakati  kazi ya  ulipaji fidia ikiendelea ambapo wananchi 168 waliwasilisha malalamiko ya kulipwa fidia ndogo ya ukarabati.


"Nawahakikishia waathirika wa mabomu jina la mtaa wenu mtachagua wenyewe na Mwenyekiti wa mtaa huu lakini kikubwa kabla kukabidhiwa nyumba umeme utakuwa umefika katika eneo hili na maji."alisema

Alielezea malalamiko ya madai ya milipuko ya mabomu Mbagala ya kuhusu fidia ndogo iliyolipwa kwa wananchi 2575 yaliwasilishwa na timu iliundwa kufanya tathimini hiyo taarifa ya tathimini ilikamilika na kuwasilishwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw.Gabriel Fuime alisema kuwa manispaa hiyo itashirikiana na ofisi ya mkoa kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya eneo hilo ikiwemo ujenzi wa kalavati kubwa na barabara.
mwisho