Wednesday, May 16, 2012

UPENDO NA HISIA NI KITU KINGINE

NIPO KWENYE NDOA KWA MAIAK 25 LAKINI SIJAWAHI KUMPENDA MKE WANGU

Nilibahatika kukutana na baba mwenye umri wa miaka 48.Kwa kuniamini akanieleza tatizo lake kubwa linalomsumbua.Anasema yeye na mkewe wamekuwa pamoja kwa miaka 25 ya ndoa lakini amegundua hajawahi KUMPENDA MKEWE.
Anasema alikutana na mkewe wakiwa shule na wamejaaliwa watoto wawili ambao kwa sasa ni wakubwa kabisa.


Alimpenda mkewe sana walipokutana shule na ilibidi kumuoa kwa vile walikaa muda sana kama wapenzi.
Japo wamekuwa pamoja kwa muda mrefu amegundua hakuwa in love nae.Kila akikaa nae na kumuangalia hafeel chochote kabisa.Anajua ni jinsi gani mkewe anampenda na  lakini anaona hayupo tayari kuendelea kuishi nae mpaka mwisho wa maisha yake.Mkewe ni mtu poa wala hajawahi kumkosea.Yupo yupo tu pia haelewi kama yupo sahihi.


HABARI KWA HISANI YA DINA MARIOS